KINONDONI YASAINI MAKUBALIANO YA MASHIRIKIANO NA MJI WA LOUD ULIOPO JIMBO LA HUNAN KUTOKA JAMHURI YA WATU WA CHINA. Posted On: March 29th, 2019 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni leo imetiliana saini makubaliano ya mashirikiano na mji wa Loud uliopo Jimbo la Hunan Kutoka Jamhuri ya watu wa China wenye lengo la kukuza soko la kibiashara na kuimarisha mahusiano ya kirafiki ya pande zote mbili. Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Dkt Patricia Henjewele amesema kuwa ni heshima kubwa kwa Manispaa ya Kinondoni kupokea ujumbe huo kutoka Jimbo la Hunan ukiongozwa na Peng Zheng ambae ni mkuu wa sehemu wa ofisi ya mashirikiano ya idara ya Biashara ya Jimbo la Hunan. Aliuhakikishia ujumbe huo kuwa Kinondoni inamazingira mazuri ya uwekezaji yenye vivutio mbalimbali Katika maeneo ya Afya, mazingira, Uchumi, Kilimo, Mifugo, uvuvi, makazi , Habari na Mawasiliano yatakayowezesha upanuzi wa mji na maendeleo ya mji. Ninaamini mahusiano haya yatakuwa na matokeo makubwa Katika maeneo Muhimu ya uwekaji kama vile shughuli za kibiashara, masoko, makazi, michezo , utalii, utamaduni, Elimu , Afya , Utalii, utumishi, upangaji na uboreshaji wa miji pamoja na shemu za kiburudani. Ameongeza Dkt Henjewele. Kwa upande wake Mstahiki meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamin Kawe Sitta alitoa shukrani za dhati kwa timu nzima iliyoshiriki kufanikisha mashirikiano hayo ikiwa ni pamoja na wizara ya fedha na mipango, idara ya uwekezaji Tanzania pamoja na Wizara ya Mambo ya nje kwa kutenga muda wao kuungana na Manispaa kufanikisha majadiliano yalipopelekea kufikia makubaliano ya mahusiano haya. Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe Daniel Chongolo akishuhudia utilianaji saini makubaliano hayo ametoa shukrani zake za dhati kwa Ndugu Peng Zheng na kuuhakikishia ujumbe toka China kuwa wilaya ya Kinondoni inamazingira tulivu na hali ya hewa safi hivyo wageni waje kuwekeza wilaya ya Kinondoni yenye fursa nyingi za uwekezaji. Amesema yeye kama kiongozi mkuu wa serikali atawapa ushirikiano wa kutosha ili kufikia malengo ya makubaliano haya ya ushirikiano wa kirafiki. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari Mwasiliano na uhusiano Manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YASAINI MAKUBALIANO YA MASHIRIKIANO NA MJI WA LOUD ULIOPO JIMBO LA HUNAN KUTOKA JAMHURI YA WATU WA CHINA. Posted On: March 29th... + Read more »
KINONDONI YAKABIDHIWA APATIMENTI 17 ZA MAJENGO YA UWEKEZAJI KUTOKA KWA MWEKEZAJI WA OSTERBAY VILLA. Posted On: March 18th, 2019 Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh Daniel Chongolo amepokea Apatimenti hizo ikiwa ni baada ya kufikiwa kwa makubaliano ya kimkataba Kati ya Manispaa ya Kinondoni na mwekezaji Osterbay Villa kwa mazungumzo Kati ya pande mbili kutokana na kuondoa kesi iliyodumu kwa zaidi ya miaka 8 mahakamani. Aidha kwa mijibu wa makubaliano ya mradi huu wa uwekezaji asilimia 60 ya mapato yatakuwa Chini ya Manispaa ya Kinondoni na asilimia 40 yatakuwa Chini ya Manispaa ya Ubungo. Amezitaja Apatimenti hizo Kuwa ni zile zilizopo Katika majengo ya 277 MAWENZI RD na 322 RUVU RD. Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni mhe Benjamin Kawe sitta amewapongeza wakuu wa wilaya ya Kinondoni na ubungo kwa kufanikisha makubaliano hayo yaliyowezesha kupatikana mapato yatakayotumika kugharamia huduma mbalimbali za kijamii Katika Manispaa zote mbili. Imeandaliwa na kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YAKABIDHIWA APATIMENTI 17 ZA MAJENGO YA UWEKEZAJI KUTOKA KWA MWEKEZAJI WA OSTERBAY VILLA. Posted On: March 18th, 2019 ... + Read more »
TAARIFA KWA UMMA Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni leo Alhamis, March 14, 2019 katika Mkutano wake wa kawaida wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni, pamoja na mambo mengine imethibitisha matumizi ya jumla ya Tshs. 3,675,202,443.90 zilizotumika kutekeleza Miradi ya Maendeleo robo ya pili kwa kipindi cha kuanzia mwezi Octoba hadi Disemba, 2018. Kwa mujibu wa Mchanganuo wa Taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo robo ya pili, kati ya fedha hizo Tshs. 2,678,384,151.30 ni fedha za Mapato ya ndani ya Manispaa, Tshs. 510,438,100.00 ni fedha za Mfuko wa pamoja wa Afya, Tshs.176,006,913.6 ni fedha za Elimu bila malipo Msingi, Tshs. 176,053,020.00 ni fedha za Elimu bila Malipo Sekondari, Tshs. 41,050,000.00 ni fedha za Mfuko wa kuchochea Maendeleo ya Jimbo na Tshs. 93,270,259.00 ni fedha za Michango ya Jamii. Aidha Baraza la Madiwani katika Mkutano huo wa kawaida limethibitisha taarifa za utekelezaji wa kazi za Kamati za kudumu za Halmashari yaani Kamati ya Huduma za Uchumi Afya na Elimu, Kamati ya Mipangomiji na Mazingira, Kamati ya Maadili, Kamati ya Kuthibiti Ukimwi na Kamati ya Fedha na Uongozi zilizofanyika katika robo ya pili kuanzia Mwezi Oktoba hadi Disemba 2018. Imetolewa na kitengo cha Habari na Uhusiano, Manispaa ya Kinondoni. TAARIFA KWA UMMA Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni leo Alhamis, March 14, 2019 katika Mku... + Read more »
WITO WATOLEWA KWA ASASI ZA KIRAIA KUSHIRIKI KAMPENI YA UBORESHAJI MIUNDOMBINU YA ELIMU KINONDONI Posted On: January 30th, 2019 Wito huo umetolewa leo na Afisa maendeleo ya jamii Manispaa hiyo Bi Halima Kahema, alipokuwa akifungua mkutano wa siku moja uliowakutanisha wadau wa maendeleo, maafisa maendeleo ya jamii wa Kata pamoja na Taasisi zisizo za kiserikali zinazofanya shughuli zake katika Manispaa hiyo, kwa lengo la kujadili mstakabali mzima wa maboresho ya miundombinu ya Elimu na utatuzi wa changamoto zilizopo katika sekta hiyo. Amesema katika kumuunga mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye swala zima la elimu, Asasi za Kiraia na Taasisi zisizo za kiserikali ni vema kuwa na mchango wake wa hiari katika hili. "Elimu ni yetu sote, hivyo ninyi Asasi za kiraia mliopo Kinondoni, tukishirikiana kwa pamoja kuongeza nguvu katika hili, hakika tutakuwa tumetatua Changamoto kubwa sana katika sekta hii nyeti, ambayo Rais wetu wa awamu ya tano ameipa kipaumbele cha kutosha" Amesisitiza Bi.Kahema. Awali akifafanua changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa katika Halmasahuri hiyo, Afisa Elimu taaluma Bw Japhet Moshi amesema, upungufu wa vyumba vya madarasa kwa shule za sekondari pekee ni 103, kwani idadi ya wanafunzi waliomaliza kidato cha nne mwaka jana ni 4,054, na waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka huu ni 11,562. Amezitaja changamoto nyingine kuwa ni uhaba wa mabweni, matundu ya vyoo vya wanafunzi, nyumba za walimu, huduma ya maji na chakula mashuleni, mazingira, watoto yatima, watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na huduma za afya. Naye Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Bw Mohammed Yusuph, alipotakiwa kuzungumza aliahidi kushirikiana na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuhakikisha maswala ya miundombinu ya elimu, pamoja na watoto waishio katika mazingira hatarishi yanapatiwa suluhisho kwa kiasi cha kuridhisha, ili miundombinu ya elimu iweze kuboreshwa. Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa shule ya Msingi Oysterbay umekutanisha Asasi za Kiraia zaidi ya 400, kwa lengo la kuelezea na kuainisha mpango wa Halmashauri wa kujenga vyumba 100 vya madarasa ili kupambana na changamoto hiyo ambayo ndio kikwazo kikubwa katika sekta hii. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na uhusiano Manispaa ya Kinondoni. WITO WATOLEWA KWA ASASI ZA KIRAIA KUSHIRIKI KAMPENI YA UBORESHAJI MIUNDOMBINU YA ELIMU KINONDONI Posted On: January 30th, 2019 Wito huo... + Read more »
WANANCHI KINONDONI WAMETAKIWA KUJENGA MAZOEA YA KULIPA KODI KILA MWAKA Posted On: February 3rd, 2019 NI KATIKA KUHAKIKISHA UTAMADUNI WA KULIPA KODI UNAJENGEKA NA KUEPUKA KUJILIMBIKIZA MADENI YASIYO YA LAZIMA. Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Daniel Chongolo alipofanya ziara katika Kata za Manispaa ya Kinondoni, na kuongea na wanachi Katika maeneo mbalimbali inapotekelezwa miradi ya maendeleo. Amesema uzalendo ndio jambo la msingi katika kuhakikisha kodi zinalipwa na miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa kiwango cha ubora uliokusudiwa. "Wananchi jengeni tabia ya kulipa kodi za majengo kila mwaka, jengeni utaratibu na mazoea ya kushiriki utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kwa pamoja tuijenge nchi yetu" Amesisitiza Mh.Chongolo. Ameongeza kuwa yapo madhara yanayoweza kujitokeza kwa mwananchi kutokulipa Kodi hiyo ya jengo kwa muda mrefu anapotakiwa kufanya hivyo kuwa ni pamoja na nyumba kupigwa mnada. Katika ziara hiyo, Mkuu huyo wa Wilaya ametembelea ujenzi wa Shule ya msingi na sekondari za Mivumoni zilizopo kata ya Wazo, Eneo linalotarajiwa kujengwa soko na stendi ya mabasi ya abiria ( daladala) Katika eneo la madale. Miradi mingine ni eneo la soko la Kisanga, Ujenzi wa Bwalo la chakula Katika shule ya sekondari Mbweni teta, Eneo la soko lililopo Mbweni Mpiji pamoja na Ujenzi wa hospitali ya Mabwepande. Katika maeneo yote aliyotembelea Mkuu wa Wilaya, amewahimiza wananchi kushiriki katika kuchangia shughuli za kimaendeleo zinazoendelea Katika maeneo yao. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. WANANCHI KINONDONI WAMETAKIWA KUJENGA MAZOEA YA KULIPA KODI KILA MWAKA Posted On: February 3rd, 2019 NI KATIKA KUHAKIKISHA UTAMADUNI WA... + Read more »
KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA KINONDONI(CMAC),YASHIRIKI MAFUNZO YA SIKU TATU KATIKA UKUMBI WA KARIMJEE Posted On: February 7th, 2019 NI KWA LENGO LA KUWAONGEZEA UELEWA WASHIRIKI KUHUSIANA NA MKAKATI WA NNE WA KITAIFA WA KUPAMBANA NA VVU NA UKIMWI (NMSF IV 2018-2022/2023) Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam, yamelenga kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati ya kudhibiti VVU na UKIMWI ya Manispaa hiyo (CMAC), ikiwa ni pamoja na kukumbushana wajibu na majukumu yao katika harakati za mapambano dhidi ya UKIMWI. Akiongea wakati wa ufunguzi, Mratibu wa kudhibiti UKIMWI upande wa kinga wa Manispaa hiyo(CHAC), Bi Rhobi Gwesso amesema Manispaa imeona ni budi kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati ya kudhibiti UKIMWI ya Manispaa (CMAC) ili waweze kuwa na elimu sahihi watakayoweza kuisamabaza kwa wananchi katika kata zao, na Katika makundi ambayo wanayawakilisha ili waweze kujiepusha na maambukizi na kukabiliana nayo. Akitoa ufafanuzi juu ya mkakati wa nne wa kitaifa wa kudhibiti VVU na UKIMWI Mwezeshaji kutoka Tume ya kudhibiti UKIMWI nchini Tanzania (TACAIDS) Bw Delfinus Kivenule amesema, mkakati huo umeandaliwa ili kutoa miongozo kwa sekta mbalimbali katika kupanga na kutekeleza afua za VVU na UKIMWI pamoja na kutafsiri sera ya Taifa kuhusu VVU na UKIMWI kwa vitendo na kuwaongoza wadau katika mwitikio wa Taifa wa kudhibiti VVU na UKIMWI. Mada mbalimbali ambazo zimewasilishwa Katika mafunzo hayo ni pamoja na Mkakati wa nne wa taifa wa kudhibiti UKIMWI, Muundo wa Kamati ya kudhibiti UKIMWI ngazi ya Mtaa, Kata na Wilaya, Wajibu na majukumu ya Kamati shirikishi za kudhibiti UKIMWI ngazi yamtaa, Kata na Wilaya (MACS, WMACS NA CMAC) , Nyingine ni Uongozi na ubia Katika mwitikio wa VVU, Ukweli kuhusu UKIMWI, kifua kikuu na homa ya ini, mawasiliano kuhusu UKIMWI na tafsiri ya Sheria ya kudhibiti VVU na UKIMWI nchini Tanzania ya mwaka 2008. Mafunzo hayo yaliyoanza tar 4 -6 mwezi wa pili 2019, yamehusisha Kamati shirikishi za kudhibiti UKIMWI ikiwa ni pamoja na waheshimiwa Wabunge, Mstahiki Meya wa Manispaa, Waheshimiwa Madiwani, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa, Wajumbe wakaribishwa toka kwenye uwakilishi wa jamii pamoja na wataalam wa Idara mbalimbali za Manispaa. Imeandaliwa na kitengo Cha Habari na uhusiano Manispaa ya Kinondoni. KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA KINONDONI(CMAC),YASHIRIKI MAFUNZO YA SIKU TATU KATIKA UKUMBI WA KARIMJEE Posted On: February 7th, ... + Read more »
RAI YATOLEWA KWA MASHIRIKA YA UMMA, NA BINAFSI KUSHIRIKI KAMPENI YA UCHANGIAJI UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA KINONDONI Posted On: February 7th, 2019 Rai hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe Daniel Chongolo alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya upokeaji mifuko 200 ya simenti kutoka Shirika la Nyumba la Taifa. Akipokea Mifuko hiyo ya simenti, Mh Chongolo amesema huo ni mfano wa kuigwa kwani kwa kufanya hivyo si tu kuunga mkono Halmashauri ya Kimondoni katika kampeni ya ujenzi wa vyumba 100, vya madarasa, bali pia ni kumuunga mkono Rais wa awamu ya tano, katika falsafa aliyonayo ya kuboresha mazingira ya elimu Nchini Tanzania. Amesema "Wilaya yetu ya Kinondoni, imejiwekea lengo ya kwamba ifikapo mwezi wa tatu, tuwe tumekamilisha kujenga vyumba 40 kwa shule za sekondari, na vyumba 60 kwa shule za msingi, hali ambayo bila mashirika na taasisi binafsi kutuunga mkono si rahisi, kadhalika ni faraja kwetu sote kuona hali hii ya ushirikiano katika kuboresha miundombinu hii ya elimu inaendelea, kwani azma yetu ni kuona vijana wetu wanapatiwa mazingira rafiki ya kusomea na waalimu kufundisha" Mh Chongolo. Naye kaimu mkuu wa kitengo cha huduma za jamii na mawasiliano kwa umma kutoka shirika la nyumba la Taifa Bw Yahya Charahani amesema elimu ndio ufunguo wa Maisha na ukitaka kumkomboa mtoto wa mwananchi aishiye chini ya dola moja yaani masikini mpatie elimu, na ndio maana tumefarijika sana kuungana na Halmashauri yetu hii katika kuhakikisha miundombinu ya elimu inaboreshwa na watoto wanasoma bila bugudha yeyote. Kwa upande wake Afisa elimu sekondari Bw Leonard Msigwa alipotakiwa kuzungumza, amelishukuru shirika la Nyumba la Taifa kwa kujitoa kuchangia Ujenzi wa vyumba vya madarasa kwani kwa kukamilika kwake kutatatua changamoto iliyopo kwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na uhusiano Manispaa ya Kinondoni. RAI YATOLEWA KWA MASHIRIKA YA UMMA, NA BINAFSI KUSHIRIKI KAMPENI YA UCHANGIAJI UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA KINONDONI Posted On: Februar... + Read more »