KUELEKEA KILELE CHA SIKU YA MTOTO WA AFRICA, KINONDONI YAADHIMISHA KWA VITENDO Posted On: June 14th, 2019 Kuelekea siku ya kilele cha Mtoto wa Afrika chenye kauli mbiu isemayo "Mtoto ni msingi wa Taifa endelevu tumutunze, tumlinde na kumuendeleza", Kinondoni yaadhimisha kwa kutoa zawadi mbalimbali kwa watoto wenye uhitaji maalumu pamoja na michezo. Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni katika sherehe hizo zilizofanyika Kiwilaya katika shule ya msingi Magomeni, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bi. Stella Msofe amesema watoto ni hazina ya Taifa, hivyo wanapaswa kulindwa, kutunzwa, kuthaminiwa, kuheshimiwa na kubwa zaidi kuwapatia haki za msingi kama elimu na afya. Ameongeza kuwa wakati umefika wa Serikali kutofumbia macho unyanyapaa wa watoto wenye mahitaji maalumu hususani ulemavu wa viungo vya mwili kwani wanayo haki na nafasi sawa katika jamii, hivyo wapewe nafasi wanayostahili na kupatiwa vipaumbele kama watoto kwani ndio warithi wa baadae wa Taifa hili. "Leo hii Tanzania tunajivunia maendeleo yanayosimamiwa na Mh Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli, naye aliwahi kuwa mtoto akakuwa, akatunzwa akapewa haki zake, na leo hii ndiye kiongozi shupavu, yote hii ni kwasabababu aliandaliwa vema mpaka amekuwa na uwezo huo na sisi kama jamii tukitenda haki sawa kwa kuwathamini wote bila kujali hali zao, tutakuwa tunaandaa viongozi bora wa baadae" amesisitiza Bi Stella. Naye Bi. Halima Kahema ambaye ni Mkuu wa Idara ya idara ya maendeleo ya jamii katika Manispaa hiyo akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi amesema Manispaa yake iko tayari kushirikiana na Asas hizi katika kuhakikisha haki ya mtoto inatekelezwa na wahitaji wananufaika nayo. Katika maadhimisho hayo yaliyoambatana na utoaji wa vyeti vya ushiriki za Asas sita, pamoja na zawadi za madaftari na fulana kwa watoto, pia yalipambwa na michezo ya kukimbia, kuruka kamba na kukimbiza kuku . Asas zilizoshiriki katika maadhimisho hayo ni Kihowede, AHRN, Save the children, PDF (peopale development forum), Red cross na Tiba. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni KUELEKEA KILELE CHA SIKU YA MTOTO WA AFRICA, KINONDONI YAADHIMISHA KWA VITENDO Posted On: June 14th, 2019 Kuelekea siku ya kilele cha M... + Read more »
KINONDONI YASAINI MIKATABA NA MAKAMPUNI MAWILI YA TAKRIBANI BILIONI 58 Posted On: June 13th, 2019 NI KWA AJILI YA UJENZI NA MABORESHO YA MTO NG'OMBE NA BARABARA YA SHEKILANGO KWA KIWANGO CHA NJIA NNE. Akisaini mikataba hiyo, kati yake na makampuni hayo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Ndg. Aron Kagurumjuli amesema, mradi wa mto ng'ombe utakaogharimu bilioni 32, utajengwa na kampuni ya China Henan International Cooperation Group CO. LTD na mradi wa barabara ya shekilango wa njia nne utakaogharimu shilingi 26 bilioni, utajengwa na Kampuni ya China road and bridge Cooperation hali itakayosaidia si tu kuboresha maeneo hayo bali pia kuyapandisha hadhi kwa kiwango kusudiwa. Amesema katika mikataba hiyo pia yatajengwa mabwawa ya kukusanyia maji eneo la karibu na chuo cha maji kutoka maeneo mbalimbali na maji hayo yataruhusiwa kuingia taratibu mto ng'ombe hali ambayo itasaidia kupunguza mafuriko. Akishuhudia utilianaji sahihi mikataba hiyo, Mstahiki Meya Wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Benjamini Sitta amesema, Serikali ya awamu ya tano ni Serikali sikivu yenye lengo la kuboresha makazi duni na kuwatoa wananchi kwenye kifungo cha mateso ya mafuriko, na ujenzi huu wa mto ng'ombe utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kadhia hiyo iliyokuwa ikisumbua wananchi wa maeneo ya Tandale na kijitonyama. Aidha Meya Sitta pia amewataka makandarasi wanaojenga miradi hiyo kujenga kwa wakati na kwa ubora stahiki ili waweze kumaliza kero iliyokuwa inawasumbua wananchi kwa muda mrefu. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YASAINI MIKATABA NA MAKAMPUNI MAWILI YA TAKRIBANI BILIONI 58 Posted On: June 13th, 2019 NI KWA AJILI YA UJENZI NA MABORESHO Y... + Read more »