KINONDONI YAPOKEA UJUMBE TOKA JIJI LA ARUSHAPosted On: December 16th, 2020NI KWA LENGO LA KUBADILISHANA UZOEFU KATIKA UTEKELEZAJI WA MKOPO WA ASILIMIA KUMIManispaa ya Kinondoni imepokea ujumbe wa watu watano kutoka Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika utendaji wa shughuli za Serikali hasa utekelezaji wa mikopo ya asilimia kumi kwavijana walemavu na wanawake.Ujumbe huo uliohusisha Naibu Meya wa Jiji la Arusha, wataalamu kutoka Idara ya maendeleo ya Jamii akiwemo mkuu wa Idara hiyo, Afisa vijana, Mratibu wa dawati la uwezeshaji Wananchi kiuchumi na Afisa maendeleo ya jamii kata umepata fursa ya kutembelea vikundi vilivyopata mikopo na kujionea wanavyotekeleza majukumu yao na suala la urejeshaji wa mikopo hiyo.Vikundi vilivyotembelewa ni kikundi cha usindikaji wa viungo mbalimbali cha vijimambo group kilichopo Kigogo pamoja na kikundi cha EZEMA watengenezaji wa bidhaa z ngozi kilichopo Mbezi Makonde.Jiji la Arusha limefurahishwa na elimu waliyoipata ya utekelezaji wa mikopo ya asilimia kumi na jinsi Kinondoni inavyotoa mikopo ya mashine za kufanyia kazi zinazowezesha utekelezaji wa kuingia uchumi wa Kati wa viwanda.Imeandaliwa naKitengo Cha Habari na Uhusiano.Manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YAPOKEA UJUMBE TOKA JIJI LA ARUSHA Posted On: December 16th, 2020 NI KWA LENGO LA KUBADILISHANA UZOEFU KATIKA UTEKELEZAJI WA MKO... + Read more »
WAVAMIZI ENEO LA KIWANDA CHA KUCHAKATA TAKA MABWEPANDE WATAKIWA KUONDOKA MARA MOJAPosted On: December 14th, 2020Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es salaam Mhe.Abubakar Kunenge leo alipofanya ziara ya ukaguzi wa kiwanda cha kuchakata taka kilichopo Kata ya Mabwepande Manispaa ya Kinondoni.Amesema eneo hilo enye ekari 14, lilitengwa kwa ajili ya shughuli za uchakataji wa taka ikiwa ni hatua za Serikali za kuhakikisha inatatua kero za uchafu zinazowakabili wananchi katika maeneo yao, lakini pia ni moja ya kitega uchumi kwa kuzalisha mbolea isiyo na kemikali itakayoweza kuuzwa kwa wanachi na wadau mabilimbali na si kwa ajili ya makazi. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Abubakar Kunenge na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo wakikagua mradi."Ninaagiza wale wote waliovamia eneo hilo kuondoka mara moja ili kuepukana na adha ya kubomolewa na kuharibiwa mali zao na ninyi Manispaa wekeni mipaka katika eneo hili ili ijulikane mwanzo na mwisho wake. Nilazima wana Dar es salaam mjifunze kufuata Sheria, kuitii Sheria na si vinginevyo." Ameagiza RC Kunenge.Katikati ni Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Songoro MnyongeNaye Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe.Songoro Mnyonge alipokuwa akitoa ufafanuzi amesema kiwanda hiki kinachojengwa kwa ufadhili kutoka jiji la Humburg Nchini Ujeruman, kinauwezo wa kuchukua tani 50 za taka kwa siku na kuzichakata hadi kufika tani 30 kwa siku moja kwa kutumia mitambo ya kisasa itakayofungwa katika eneo hilo.Amesema mitambo ya kuchakata taka tayari imefika bandarini ikisubiri ukamilishwaji wa taratibu za kiserikali ili iweze kufungwa tayari kwa kuanza kazi.Akitoa ufafanuzi wa kiwanda hicho, Afisa Usafishaji wa Manispaa hiyo Ndg Alban Mugyabuso amesema mfumo mzima wa uchakataji taka hadi kukamilika kwake unatumia siku 14, na kwamba tayari masoko yameshaanza kutafutwa kwajili ya ununuzi wa mbolea isiyo na kemikali itakayopatikana baada ya uchakataji.Aidha ameeleza kuwa takataka zinazochukuliwa kwa ajili ya uchakataji ni zile zinazotoka masokoni zenye kuoza kwa haraka na siyo chupa za maji wala mifuko ya plastiki.Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amewataka TRA na Bandari kushughulikia kwa haraka mitambo hiyo iliyoko bandarini iweze kutoka ili ifungwe na kiwanda kiweze kufanya kazi.Imeandaliwa naKitengo Cha Uhusiano na Habari.Manispaa ya Kinondoni. WAVAMIZI ENEO LA KIWANDA CHA KUCHAKATA TAKA MABWEPANDE WATAKIWA KUONDOKA MARA MOJA Posted On: December 14th, 2020 Agizo hilo limetolewa na... + Read more »
KINONDONI YAPONGEZWA KWA UBORA NA UTEKELEZAJI WA MIRADIPosted On: December 14th, 2020NI ULE WA UJENZI WA HOSPITAL YA MABWEPANDE KWA GHARAMA YA TSH BIL 2.5, MAPATO YAKE YA NDANI HADI KUKAMILIKA KWAKE.Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Abubakar Kunenge alipofanya ziara katika Manispaa hiyo ya Ukaguzi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo hususan ujenzi wa hospital ya Mabwepande iliyopo katika eneo la Mabwepande Manispaa ya Kinondoni.Amesema Manispaa hiyo ndiyo pekee kwa Mkoa wa Dar es salaam iliyoweza kujenga Hospital kubwa yenye kiwango kinachoridhisha itakayokuwa na uwezo wa kutoa huduma kwa wananchi kwa kutumia mapato yake ya ndani .Amesema "Kinondoni mnafanya vizuri kwa habari ya miradi, mnatafsiri vizuri maagizo ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dr.John Pombe Joseph Magufuli kwa kusogeza huduma karibu na wananchi, kwa ujenzi wa hospital hii, inabidi Halmashauri nyingine zije kujifunza hapa kwenu, hii ndio Halmashauri ya mfano, ninayotamani Halmashauri nyingine ziwe" Amesema KunengeNaye Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe. Songoro Mnyonge alipotakiwa kufafanua Jambo amesema kuwa Hospital hiyo ya Mabwepande inayo uwezo wa kuudumia wagonjwa wa nje 400 Hadi 700 kwa siku na wagonjwa wa kulazwa 187 Hadi 224 kwa siku.Aidha Meya huyo pia ameahidi kuyatekeleza maagizo yote aliyopewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe.Kunenge kwa kushirikiana na watendaji pamoja na kutekeleza mikakati kwa kutenga fedha katika bajeti ya 2021/2122.Alipotakiwa kuzitaja changamoto zinazokabili hospital hiyo ya Mabwepande, Mganga mfawidhi wa hospital hiyo Dr.Christowelu Mande amesema ni ukosefu wa gari ya kubebea wagonjwa hali inayopelekea mazingira magumu wakati wa uhitaji wake.Katika hatua nyingine Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo Dr. Samweli Laiza amesema, hospital hiyo ya Mabwepande inatarajiwa kutumia kiasi Cha shilingi takribani Bilioni 2.5 hadi kukamilika kwake.Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ametembelea mradi wa Hospitali na kiwanda cha kuchakata taka kilichopo mabwepande pamoja na Zahanati ya Bunju.Imeandaliwa naKitengo Cha Uhusiano na Habari.Manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YAPONGEZWA KWA UBORA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI Posted On: December 14th, 2020 NI ULE WA UJENZI WA HOSPITAL YA MABWEPANDE KWA GHA... + Read more »
MATUKIO KATIKA PICHA -SEMINA YA BARAZA JIPYA LA MADIWANIPosted On: December 9th, 2020Baraza jipya la Madiwani lililoapishwa tarehe 07/12/2020 katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa limeendelea kupata semina ihusuyo uelewa wa uendeshaji wa Serikali za Mitaa.Afisa Utumishi Mkuu Bi.Fauzia Nombo akifafanua jamboMada zinazofundishwa katika Semina hiyo ni Uongozi na Utawala Bora, Uwajibikaji, Majukumu haki na stahiki za Madiwani, Sheria za Serikali za Mitaa pamoja Sheria za Manunuzi.Watoa mada katika Semina hiyo ni Sekretarieti ya maadili ya Utumishi wa Umma pamoja na Wataalamu kutoka Chuo Cha Hombolo.Imeandaliwa naKitengo Cha Habari na UhusianoManispaa ya Kinondoni MATUKIO KATIKA PICHA -SEMINA YA BARAZA JIPYA LA MADIWANI Posted On: December 9th, 2020 Baraza jipya la Madiwani lililoapishwa tarehe 07/12... + Read more »
BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LAANZA KAZI RASMIPosted On: December 7th, 2020Baraza hilo chini ya Mstahiki Meya wake Mhe.Songoro Mnyonge limeanza kazi kwa kupitisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Halmashauri katika kipindi cha kuanzia Julai hadi Octoba 2020.Akitoa hoja ya kupitisha na kuungwa mkono kwa taarifa hiyo ya utekelezaji kwa Baraza la madiwani Meya Songoro amesema taarifa hiyo ni kielelezo tosha cha majukumu yanayompasa kila diwani kwenye kata yake kuhakikisha anayasimamia na kuyatekeleza kwa maslahi mapana ya wananchi."Waheshimiwa madiwani niwahakikishie Jambo moja, kipindi kilichopita tulifanya kazi kubwa Sana, kwahiyo awamu hii pia tutaendelea pale ambapo tuliishia, kunamiradi mikubwa ambayo inaendelea hivi Sasa, tumeingia rasmi kufanya kazi" Mhe. Songoro Mnyonge.Awali akiisoma taarifa hiyo ya utekelezaji kwa Baraza la Madiwani, Katibu wa Baraza hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Ndg Aron Kagurumjuli amesema taarifa hii ni ya utekelezaji wa shughuli za Halmashauri zilizofanywa kipindi ambacho baraza hilo halikuwepo.Ameongeza kuwa mara baada ya kuvunjwa kwa Baraza la Madiwani Julai mwaka huu, Halmashauri iliendelea na utekelezaji wa mpango wa bajeti ya mwaka 2020/2021 na hivyo kufanikisha shughuli mbalimbali za maendeleo hususani katika miradi mikubwa na ya kimkakati.“ Waheshimiwa madiwani, taarifa hii imeeleza namna ambavyo miradi imefanikiwa na vitu ambavyo vimefanyika katika kipindi ambacho hamkuwepo, kikubwa ni kwamba tumefanya mambo makubwa na hivyo tunawaahidi kushirikiana kwa pamoja kuyaendeleza yale ambayo yamefanyika” amesema Kagurumjuli.Katika hatua nyingine Baraza hilo lenye madiwani 30 limeteua wenyeviti na wajumbe wa kamati za kudumu ambazo ni kamati ya huduma za uchumi afya na elimu, kamati ya fedha na uongozi, kamati ya Mipangomiji na Mazingira, Kamati ya maadili na kamati ya UKIMWI. Imeandaliwa naKitengo cha Habari na MahusianoManispaa ya Kinondoni. BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LAANZA KAZI RASMI Posted On: December 7th, 2020 Baraza hilo chini ya Mstahiki Meya wake Mhe.Songoro Mnyonge l... + Read more »