KINONDONI YAPONGEZWA KWA UBORA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI
NI ULE WA UJENZI WA HOSPITAL YA MABWEPANDE KWA GHARAMA YA TSH BIL 2.5, MAPATO YAKE YA NDANI HADI KUKAMILIKA KWAKE.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Abubakar Kunenge alipofanya ziara katika Manispaa hiyo ya Ukaguzi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo hususan ujenzi wa hospital ya Mabwepande iliyopo katika eneo la Mabwepande Manispaa ya Kinondoni.
Amesema Manispaa hiyo ndiyo pekee kwa Mkoa wa Dar es salaam iliyoweza kujenga Hospital kubwa yenye kiwango kinachoridhisha itakayokuwa na uwezo wa kutoa huduma kwa wananchi kwa kutumia mapato yake ya ndani .
Amesema "Kinondoni mnafanya vizuri kwa habari ya miradi, mnatafsiri vizuri maagizo ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dr.John Pombe Joseph Magufuli kwa kusogeza huduma karibu na wananchi, kwa ujenzi wa hospital hii, inabidi Halmashauri nyingine zije kujifunza hapa kwenu, hii ndio Halmashauri ya mfano, ninayotamani Halmashauri nyingine ziwe" Amesema Kunenge
Naye Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe. Songoro Mnyonge alipotakiwa kufafanua Jambo amesema kuwa Hospital hiyo ya Mabwepande inayo uwezo wa kuudumia wagonjwa wa nje 400 Hadi 700 kwa siku na wagonjwa wa kulazwa 187 Hadi 224 kwa siku.
Aidha Meya huyo pia ameahidi kuyatekeleza maagizo yote aliyopewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe.Kunenge kwa kushirikiana na watendaji pamoja na kutekeleza mikakati kwa kutenga fedha katika bajeti ya 2021/2122.
Alipotakiwa kuzitaja changamoto zinazokabili hospital hiyo ya Mabwepande, Mganga mfawidhi wa hospital hiyo Dr.Christowelu Mande amesema ni ukosefu wa gari ya kubebea wagonjwa hali inayopelekea mazingira magumu wakati wa uhitaji wake.
Katika hatua nyingine Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo Dr. Samweli Laiza amesema, hospital hiyo ya Mabwepande inatarajiwa kutumia kiasi Cha shilingi takribani Bilioni 2.5 hadi kukamilika kwake.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ametembelea mradi wa Hospitali na kiwanda cha kuchakata taka kilichopo mabwepande pamoja na Zahanati ya Bunju.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Uhusiano na Habari.
Manispaa ya Kinondoni.
0 comments:
Post a Comment