KINONDONI YAZINDUA ZOEZI LA UGAWAJI VITAMBULISHO TAKRIBANI 5000 KWA WAMACHINGA Posted On: December 11th, 2018 Akizindua zoezi hilo katika soko la Mwenge, Mkuu wa Wilaya ya Kinondonii Mh. Daniel Chongolo amesema, ni katika kutekeleza agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli, la kuwajengea mazingira mazuri wafanyabiashara wadogowadogo kwa kuwatambua na kuwapatia vitambulisho watakavyovitumia katika kazi zao. Amesema ni zoezi endelevu, kwani vitambulisho hivi vilivyotengenezwa na Ofisi ya Rais -TAMISEMI vimelenga wafanyabiashara wenye mtaji chini ya milioni nne na pia ni kwa lengo la kuwawezesha mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwa na idadi na takwimu sahihi itakayowawezesha kwa urahisi kufanya kazi yao ya kukusanya mapato. "Tumefanyia zoezi hili hapa Mwenge, kwani ndiko kuliko na wafanyabiashara wengi na vitambulisho hivi vimetolewa kwa lengo la kuwezesha mamlaka ya mapato Tanzania kutambua wafanyabiashara wadogowadogo, pia litawasaidia wafanyabiashara wetu kufanya biashara bila bugudha yeyote." Amesisitiza Mkuu huyo wa Wilaya. Naye Afisa Biashara wa Manispaa hiyo Bw. Mohamed Nyasama alipotakiwa kuzungumzia swala hilo amesema, hii ni neema kwa wamachinga kwani kitakachofanyika ni kuwatambua, kuwahakiki, na kuwapatia vitambulisho hivyo vitakavyowasaidia kufanya biashara sehemu yoyote nchini bila usumbufu wowote. Amesema kinachotakiwa kufanyika ni kwa wafanyabiashara waliokwisha hakikiwa kujaza fomu za usajili, kuwasilisha picha, na vitambulisho ambavyo walikwishapatiwa na Manispaa awali, ili waweze kupatiwa vipya na kwa wale wamachinga ambao hawana vitambulisho kuhakikiwa upya na kupatiwa vitambulisho kwa mujibu wa sheria. Aidha zoezi hili pia limehusisha wamachinga kutoka masoko ya Bunju A, na B, Morocco, Boko Basihaya, Mbezi samaki, Mbezi ya Chni,Tegeta, Kawe, Mwenge, Makumbusho, Magomeni, Mwananyamala na Tandale. Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wamachinga hao kuhakikisha wanazingatia sheria, kanuni, na taratibu katika matumizi ya vitambulisho hivyo, ili kuepukana na usumbufu wowote unaoweza kutokea na kuhakikisha kila muhusika ananufaika na zoezi hili. Imeandaliwa na Kitengo cha habari na Uhusiano. Manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YAZINDUA ZOEZI LA UGAWAJI VITAMBULISHO TAKRIBANI 5000 KWA WAMACHINGA Posted On: December 11th, 2018 Akizindua zoezi hilo kati... + Read more »
BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LAMPONGEZA RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE.DR.JOHN POMBE MAGUFULI Posted On: December 14th, 2018 NI KUFUATIA MPANGO WA UTOAJI WA VITAMBULISHO KWA WAMACHINGA UTAKAOWARAHISISHIA UFANYAJI KAZI ZAO BILA BUGUDHA. Baraza la Madiwani Manispaa ya Kinondoni chini ya Mwenyekiti wake ambaye pia ni diwani wa kata ya Msasani Mhe. Benjamini Sitta, leo limempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dr.John Pombe Joseph Magufuli, kwa mpango wake mzuri, madhubuti na wezeshi wa kuwapatia vitambulisho wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama wamachinga vitakavyowasaidia katika shughuli zao. Akitoa pongezi hizo kwa niaba ya Baraza hilo, Meya Sitta amesema, mpango huo mkakati wa vitambulisho ni mpango ulio rahisi, rafiki, na wezeshi utakaowawezesha wamachinga kufanya kazi zao mahali popote nchi hii bila kubughudhiwa alimradi wasivunje sheria. Ameongeza kuwa vitambulisho hivyo pia vitawasaidia si tu mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kufanya kazi zao,bali pia kwa wamachinga kutambulika kuthaminiwa na kusajiliwa katika mfumo unaojulikana. Akiainisha viambatishi rejea ili kupata kitambulisho hicho, katibu wa kikao hicho cha baraza, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndg Aron Kagurumjuli amesema, kwa wale waliosajiliwa awali kwa kinondoni wanachotakiwa kufanya ni kurejesha kitambulisho cha awali, picha moja ya passportsize, kujaza fomu yenye taarifa zako, na kiasi cha fedha shilingi elfu ishirini tu. Katika hatua nyingine, Meya Sitta amewataka wamachinga wa Manispaa ya kinondoni kutokutumia vibaya vitambulisho hivyo kwani atakayebainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake. Imeandaliwa na Kitengo cha Uhusiano na Habari. Manispaa ya Kinondoni. BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LAMPONGEZA RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE.DR.JOHN POMBE MAGUFULI Posted On: December 14th, 20... + Read more »
SEMINA ELEKEZI KWA WAGAWA DAWA ZA KINGATIBA YA MABUSHA, MATENDE NA MINYOO YATOLEWA KINONDONI Posted On: December 14th, 2018 Semina hiyo iliyohusisha wagawa dawa za kingatiba za magonjwa ya mabusha na matende kutoka kata zote 20 za Manispaa ya kinondoni, imefanyika leo katika ukumbi wa Roman Catholic ulioko Manzese. Akieleza malengo ya semina hiyo, mratibu wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele katika manispaa ya Kinondoni Dr. Neema Mlole amesema, lengo ni kuhakikisha elimu iliyosahihi juu ya kampeni hii inatolewa kwa usahihi na kueleweka, lakini pia ni katika kuzingatia baadhi ya vipengele vinavyompasa binadamu yeyote yule kumeza dawa vinafuatwa, kadhalika na kuhakikisha pia malengo yaliyokusudiwa ya kufikia wananchi takribani milioni 1.2 kwa kampeni hii pia yanafikiwa. "Ili tuweze kufikia malengo madhubuti, ni lazima elimu sahihi itolewe, lakini pia tunahitaji kuimarisha na kuhakikisha tunalinda nguvu kazi ya wananchi,na namna pekee ni kuboresha afya zao pale inapobidi kwa kuhakikisha wanashiriki kampeni hizi kwa uhakika a ufasaha mkubwa. Amesisitiza Dr Neema. Ameongeza kuwa kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya afya, maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto kitengo cha magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele itaendesha kampeni kuanzia tarehe 15/12/2018 na kuisha tarehe 20/12/2018 ,,hivyo wagawa dawa hawa ni watu muhimu sana katika kuhakikisha ufanisi huo unakuwepo na unazingatiwa. Katika semina hiyo pamoja na zoezi la usambazaji kingatiba kwa ajili ya kampeni hiyo iliyoambatana na ugawaji wa vifaa vitakavyotumika, pia wamejifunza namna thabiti ya utoaji huduma hiyo, vitu vya kuzingatia kabla na baada ya utoaji wake, na upi umri sahihi wa mtu kumeza dawa ikiwa ni pamoja na kupima urefu. Katika hatua nyingine, wagawa dawa hao wameishukuru Wizara pamoja na Halmashauri kwa kuendesha kampeni hii yenye manufaa kwa afya za wanadamu, na kuahidi ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha hilo linafanikiwa. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano. Manispaa ya Kinondoni. SEMINA ELEKEZI KWA WAGAWA DAWA ZA KINGATIBA YA MABUSHA, MATENDE NA MINYOO YATOLEWA KINONDONI Posted On: December 14th, 2018 Semina hiyo... + Read more »
HATI 93 ZA VIWANJA KWA NJIA YA ELEKTRONIKI ZAKAMILIKA KINONDONI Posted On: December 14th, 2018 Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa kamati ya Mipangomiji na mazingira ambaye pia ni diwani wa kata ya Mwananyamala Mhe. Songoro Mnyonge alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa kamati yake katika kikao cha baraza la madiwani robo ya kwanza kilichofanyika leo . Amesema Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi imeanza utaratibu huo mpya uliorahisi na unaotumia mfumo maalumu wa kuandaa hati na kukamilika kwa siku moja, hali iliyoondoa bugudha na kero kwa wananchi. "Tunaishukuru Wizara ya ardhi kwa kuandaa mfumo rahisi kwa suala zima la uandaaji wa hati, mfumo huo wa elektroniki umesaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa bugudha kwa wananchi, kwani ni mfumo wezeshi, na unatumia muda mchache hali iliyoondoa kero kwa wananchi" Amesisitiza Songoro. Awali akiwakaribisha wajumbe kwenye kikao hicho cha baraza, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Msasani Mhe. Benjamini sitta alisema katika kikao hiko zitapokelewa na kujadiliwa agenda zitakazotokana na taarifa za kamati tano za kudumu za Halmashauri. Agenda hizo ni utekelezaji wa taarifa za kamati ya huduma za uchumi, afya na elimu, kamati ya Mipangomiji na mazingira, Kamati ya maadili, kamati ya kudhibiti ukimwi na kamati ya fedha na uongozi. Katika hatua nyingine baraza hilo pia limempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuwajali wamachinga na kuwatengenezea mazingira wezeshi ya ufanyaji kazi zao kwa kuwapatia vitambulisho. Imeandaliwa na Kitengo cha habari na uhusiano Manispas ya Kinondoni. HATI 93 ZA VIWANJA KWA NJIA YA ELEKTRONIKI ZAKAMILIKA KINONDONI Posted On: December 14th, 2018 Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa kama... + Read more »
KINONDONI YAZINDUA ZOEZI LA UGAWAJI VITAMBULISHO TAKRIBANI 5000 KWA WAMACHINGA Posted On: December 11th, 2018 Akizindua zoezi hilo katika soko la Mwenge, Mkuu wa Wilaya ya Kinondonii Mh. Daniel Chongolo amesema, ni katika kutekeleza agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli, la kuwajengea mazingira mazuri wafanyabiashara wadogowadogo kwa kuwatambua na kuwapatia vitambulisho watakavyovitumia katika kazi zao. Amesema ni zoezi endelevu, kwani vitambulisho hivi vilivyotengenezwa na Ofisi ya Rais -TAMISEMI vimelenga wafanyabiashara wenye mtaji chini ya milioni nne na pia ni kwa lengo la kuwawezesha mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwa na idadi na takwimu sahihi itakayowawezesha kwa urahisi kufanya kazi yao ya kukusanya mapato. "Tumefanyia zoezi hili hapa Mwenge, kwani ndiko kuliko na wafanyabiashara wengi na vitambulisho hivi vimetolewa kwa lengo la kuwezesha mamlaka ya mapato Tanzania kutambua wafanyabiashara wadogowadogo, pia litawasaidia wafanyabiashara wetu kufanya biashara bila bugudha yeyote." Amesisitiza Mkuu huyo wa Wilaya. Naye Afisa Biashara wa Manispaa hiyo Bw. Mohamed Nyasama alipotakiwa kuzungumzia swala hilo amesema, hii ni neema kwa wamachinga kwani kitakachofanyika ni kuwatambua, kuwahakiki, na kuwapatia vitambulisho hivyo vitakavyowasaidia kufanya biashara sehemu yoyote nchini bila usumbufu wowote. Amesema kinachotakiwa kufanyika ni kwa wafanyabiashara waliokwisha hakikiwa kujaza fomu za usajili, kuwasilisha picha, na vitambulisho ambavyo walikwishapatiwa na Manispaa awali, ili waweze kupatiwa vipya na kwa wale wamachinga ambao hawana vitambulisho kuhakikiwa upya na kupatiwa vitambulisho kwa mujibu wa sheria. Aidha zoezi hili pia limehusisha wamachinga kutoka masoko ya Bunju A, na B, Morocco, Boko Basihaya, Mbezi samaki, Mbezi ya Chni,Tegeta, Kawe, Mwenge, Makumbusho, Magomeni, Mwananyamala na Tandale. Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wamachinga hao kuhakikisha wanazingatia sheria, kanuni, na taratibu katika matumizi ya vitambulisho hivyo, ili kuepukana na usumbufu wowote unaoweza kutokea na kuhakikisha kila muhusika ananufaika na zoezi hili. Imeandaliwa na Kitengo cha habari na Uhusiano. Manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YAZINDUA ZOEZI LA UGAWAJI VITAMBULISHO TAKRIBANI 5000 KWA WAMACHINGA Posted On: December 11th, 2018 Akizindua zoezi hilo kati... + Read more »
WAKAZI WA TANDALE WAMETAKIWA KUHAKIKISHA WANAJIIMARISHA KIUCHUMI, KIJAMII NA KIAFYA KWA KUHAKIKSHA WANAZINGATIA AFYA YA UZAZI Posted On: December 11th, 2018 Hayo yamebainishwa leo na Mratibu wa ICHF Manispaa ya Kinondoni Bi.Joyce John, katika mdahalo wa afya ya uzazi kwa jamii, uliofanyika katika kituo cha afya cha Tandale. Amesema suala la uzazi wa mpango ni suala mtambuka linalomtaka baba na mama kijadiliana kwani watoto wanaozaliwa wanahitaji elimu ili waweze kujikwamua kimaendeleo, kiuchumi, na kifikra kuelekea uchumi wa Kati wa viwanda. "Tunahitaji watu au uzao wenye fikra yakinifu na uwezo wa kupambanua mambo kwa weledi ili kutoa ufumbuzi wa mahitaji ya jamii yetu, hata hivyo hayo yanawezekana ikiwa afya ya uzazi itazingatiwa ipasavyo maana ndiyo msingi imara wa jamii inayojitosheleza" Ameeleza Mratibu Joyce. Akifafanua umuhimu wa afya ya uzazi kwa jamii Bi Fatma Juma Watanga ambaye pia ni muuguzi msaidizi wa kituo cha afya Tandale, amesema mtoto aliyenyonya ziwa la mama kwa miaka miwili mfululizo, anakuwa na afya njema ya akili, ikiwa ni pamoja na kusukuma gurudumu la maendeleo, tofauti na ambaye hakunyonya kwa muda huo. Katika mdahalo huo pia umehudhuriwa na wananchi kutoka kata na mitaa ya tandale, pamoja na wauguzi kutoka kituo cha tandale, na kujadili nini maana ya afya ya uzazi, namna na njia za kufuata ili kuwa na afya ya uzazi na umhimu wake. Aidha washiriki wa mdahalo huo pia wameushukuru uongozi kwa kuwapatia mada hizo zilizotoa mwanga wa nini kifanyike katika kurudisha upendo uliokuwa umepotea katika jamii. Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Uhusiano. Manispaa ya Kinondoni. WAKAZI WA TANDALE WAMETAKIWA KUHAKIKISHA WANAJIIMARISHA KIUCHUMI, KIJAMII NA KIAFYA KWA KUHAKIKSHA WANAZINGATIA AFYA YA UZAZI Posted On: ... + Read more »