KINONDONI YAZINDUA KAMATI YA MAAFA YA WILAYA. Posted On: November 22nd, 2018 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Daniel Chongolo leo, amezindua kamati ya maafa ya Wilaya yenye wajumbe 29 ambapo wajumbe 18 ni kutoka timu ya Manispaa na wajumbe 11 ni wadau kutoka nje ya Halmashauri, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Manispaa. Akizindua kamati hiyo, Mkuu huyo wa Wilaya katika hotuba yake amesema, maafa ni tukio kubwa linalotokea na kuathiri utaratibu wa maisha ya jamii na kusababisha madhara makubwa kwa watu, mali, uchumi na mazingira ambapo huzidi uwezo wa jamii kukabiliana nalo. Ameongeza kuwa kwa Serikali kutambua uwepo wa maafa na majanga Nchini na umuhimu wa kukabiliana nayo, imetunga sheria ya usimamizi wa maafa namba 7 ya mwaka 2015, inayotaka uundwaji wa kamati ufanyike, kwa lengo la kuchukua hatua za kujiepusha nayo na kukabiliana pindi yanapojitokeza. Amesema "Kamati ninayoizindua leo ni utekelezaji wa matakwa ya Sheria, hivyo hatupo hapa kwa bahati mbaya na kamati hii inatambulika kwa mujibu wa sheria tajwa, kifungu cha 15 na 16 hivyo nendeni mkafanye kazi" Amesisitiza Chongolo. Awali akisoma taarifa ya uundaji wa kamati ya usimamizi wa Maafa wa Wilaya kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa, Mratibu wa Maafa wa Manispaa hiyo Bi.Pendo Fred amewataja wajumbe wanaounda kamati kuwa ni wakuu wa idara na vitengo 16 vya Manispaa, Jeshi la zimamoto na uokozi Mkoa wa Kinondoni, TARURA, TANESCO, DART, DAWASCO na vyombo vya habari. Aidha ameainisha mipango na mikakati ya kamati kwa mwaka 2018/2019 kuwa ni kufanya mkutano na wadau, kutoa mafunzo kwa kamati za maafa ndani ya Mtaa na Kata, kuanzisha program ya kutoa mafunzo katika jamii na Halmashauri kutekeleza miradi ya DMDP kwa kujenga barabara zenye mifereji. Naye mratibu wa timu ya wataalam ya uokoaji ya Mkoa wa Dar es Salaam (DARMAERT), Ndg Christopher Mzava, alipokuwa akitoa taarifa yake ameyaainisha majukumu ya kamati iliyozinduliwa kuwa ni kuhuisha masuala ya dharura na maafa katika mipango ya maendeleo, kufuatilia tishio la majanga na maafa na kufanya uchunguzi wa kutokea kwa maafa na uchoraji wa ramani. Nyingine ni kuainisha mahitaji ya mafunzo kwa umma na kutoa elimu, kutafuta rasilimali na kusimamia operesheni za maafa na kuunda timu ya ukabilianaji wa maafa na muundo wa kulinda jamii. Uzinduzi wa kamati hiyo pia umehudhuriwa na wawakilishi kutoka Bank ya Dunia, msalaba mwekundu, wawakilishi kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa na waheshimiwa madiwani. Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Uhusiano. Manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YAZINDUA KAMATI YA MAAFA YA WILAYA. Posted On: November 22nd, 2018 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Daniel Chongolo leo, amezi... + Read more »
BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA KINONDONI LAMPONGEZA MKURUGENZI KWA UTENDAJI. Posted On: November 21st, 2018 Baraza la Madiwani Manispaa ya Kinondoni, chini ya Mwenyekiti wake Mh.Benjamini Sitta, kupitia mkutano wake wa Mwaka uliofanyika leo limempongeza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Ndg Aron Kagurumjuli, pamoja na timu yake nzima kwa utendaji mzuri na ushirikiano mkubwa katika kukusanya mapato, uliopelekea ongezeko la ukusanyaji wake kufikia asilimia 98%. kwa tathmini ya bajeti ya mwaka 2017/2018. Pongezi hizo zimekuja mara baada ya Mkurugenzi huyo kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo, taarifa za utendaji kazi, taarifa za mali za Halmashauri pamoja na tathmini ya bajeti ya mwaka 2017/2018, iliyoonesha kiasi cha bajeti iliyotengwa, makusanyo kutoka vyanzo vya ndani, mapato pamoja na matumizi, huku ikionesha changamoto na mikakati ya kukabiliana nayo katika suala zima la ukusanyaji wa mapato. Amezitaja changamoto hizo kuwa ni baadhi ya vyanzo vikubwa vya mapato kuondolewa katika Halmashauri na kupelekwa Serikali kuu, sheria ndogo zinazotumika kutoza ushuru kwenye masoko kupitwa na wakati, kuwepo mikataba isiyozingatia maslahi ya Halmashauri, na kuwepo migogoro ya vibanda katika masoko na maeneo ya wazi. Aidha Mkurugenzi huyo pia ameainisha mikakati ya kukabiliana na changamoto hizo kuwa ni kuziba pengo la vyanzo vya mapato lililofutwa kwa kuanzisha daftari la walipakodi, kuwepo mchakato wa sheria ndogo zilizopitwa na wakati kufanyika upya, kutambua maeneo ya wazi na vibanda vya biashara vilivyopo katika maeneo ya Umma na kisimamia utozaji wake, kuimarisha mfumo wa upatikanaji wa takwimu za walipakodi na kufanya mapitio ya mikataba ya sasa ya uwekezaji. Katika hatua nyingine katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni Bi Stella Msofe, katika kikao hicho, amemtangaza rasmi Diwani wa Kata ya Kigogo Mh Mangalu George Manyama kuwa Naibu Meya wa Manispaa hiyo, kwa awamu nyingine tena. Imeandaliwa na Kitengo cha Uhusiano na habari. Manispaa ya Kinondoni. BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA KINONDONI LAMPONGEZA MKURUGENZI KWA UTENDAJI. Posted On: November 21st, 2018 Baraza la Madiwani Manispa... + Read more »
TAMISEMI YAENDESHA MAFUNZO YA SIKU MOJA KWA KAMATI YA LISHE KINONDONI Posted On: November 16th, 2018 NI KUHUSIANA NA UANDAAJI WA MIPANGO YA HUDUMA ZA LISHE KWA MWAKA WA FEDHA 2019/2020. Ofisi ya Raisi -TAMISEMI kupitia kitengo cha lishe imeendesha mafunzo kwa Kamati ya lishe ya Manispaa ya Kinondoni, yahusuyo mipango ya utekelezaji wa huduma za lishe kwa watoto umri chini ya miaka mitano, ikiwa ni pamoja na kuongeza uelewa katika swala zima la utekelezaji wake, hasa uwekaji wa vipaumbele katika bajeti ya 2019/2020. Akifungua mafunzo hayo ya siku moja yaliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Manispaa, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Bi Stella Msofe amesema mafunzo haya ni muhimu, na yakawe chachu ya utekelezaji wa jambo hili, hasa ikizingatiwa azma ya Serikali ni kuhakikisha inaepukana na madhara yanayoweza kutokea kwa watoto wetu pindi wanakosa lishe bora Naye mkufunzi kutoka ofisi ya Rais -TAMISEMI Bi.Mary Kibona, alipokuwa akiwasilisha mada ihusianayo na mpango mkakati wa utekelezaji,amefafanua maana halisi ya lishe kuwa ni mchakato wa tangu chakula kinapoliwa mdomoni, kinasagwa na kuingia mwilini na kuanisha madhara ayapatayo mtoto anapokosa lishe bora kuwa ni kupata upungufu wa madini na Vitamini mwilini. Akiainisha mafanikio ya Kamati ya lishe kwa Manispaa ya kinondoni tangu kuundwa kwake, Afisa lishe wa Manispaa hiyo Bi Emiliana Sumaye amesema , kamati hiyo imefanikiwa kupeleka shughuli za lishe kwa idara mtambuka, imefanikiwa kukaa vikao vitatu vya kujadiliana mwelekeo mzima wa lishe na kuainisha njia sahihi za kuhakikisha lengo linafikiwa, imefanikiwa pia kuhakikisha vituo 65 vya kutolea huduma za afya vilivyoko Manispaa vinatoa elimu ya lishe, na kufikia wazazi takribani 19,399 kwa elimu hiyo ya lishe kwa watoto na wajawazito. Pia ameainisha changamoto zinazowakabili kuwa ni Jamii kushindwa kutumia huduma ya uzazi kikamilifu, watoa huduma kutowajibika ipasavyo, kuwepo na upungufu wa watoa huduma ngazi ya jamii, na watoa huduma kutopata elimu ya utoaji wa vidonge vya folic Acidi. Mafunzo haya yaliyohudhuriwa pia na wawakilishi kutoka Ofisi ya Mkoa wa Dar es salaam Bi Janeth Mzava, Mwakilishi kutoka, UNICEF Bi.Joyce Ndeba, Mwenyekiti wa huduma za Uchumi Afya na Elimu Mh.Thadei Masawe, kamati ya lishe ya Manispaa, pamoja na wakuu wa idara na vitengo, yamejadili mada zihusuzo uwasilishaji wa taarifa za utekelezaji wa shughuli za lishe. Nyingine ni Mpango na bajeti ya lishe kwa kutumia planrep, shughuli za lishe/afua za lishe zinazoweza kupangwa ngazi ya vituo vya afya na upatikanaji wa rasilimali watu na fedha. Imeandaliwa na, Kitengo cha Habari na Uhusiano. Manispaa ya Kinondoni. TAMISEMI YAENDESHA MAFUNZO YA SIKU MOJA KWA KAMATI YA LISHE KINONDONI Posted On: November 16th, 2018 NI KUHUSIANA NA UANDAAJI WA MIPAN... + Read more »