WITO WATOLEWA KWA WAZAZI NA WALIMU WA SHULE ZA SERIKALI MANISPAA YA KINONDONI. NI KATIKA MWENDELEZO WA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA MITIHANI YA PAMOJA KWA WANAFUNZI WA DARASA LA SABA. Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kupitia idara ya elimu Msingi imeendelea na mpango wa kuandaa mitihani ya pamoja kwa wanafunzi Wa darasa la saba, ambapo leo imetangaza matokeo ya mtihani wa jaribio la pamoja uliofanyika tarehe 02-03/05/2019. Akitangaza matokeo hayo kwa niaba ya Afisa Elimu Msingi Bi Fatuma Mwiru, amewasihi Walimu na Wazazi wa shule za serikali kutilia mkazo fursa hii kwani ni maandilizi sahihi na kipimo tosha kuelekea mtihani wa Taifa. Ametoa nasaha hiyo baada ya kubaini kuwa idadi ya wanafunzi waliofanya vizuri na kupata zawadi imetawaliwa na watoto kutoka shule binafsi. "Napenda kuwasihi Wazazi na Walimu Wa shule za serikali wawe msitali wa mbele kuhakikisha watoto wanafanya vizuri katika mitihani hii maana ni dira tosha kuelekea mtihani wa Taifa" ameongeza Bi Fatuma. Aidha Bi Fatuma amesema kuwa ofisi ya Mkurugenzi kupitia idara ya Elimu Msingi ipo bega kwa bega kuhakikisha matokeo chanya yatapatikana katika mtihani wa Taifa na ndio maana Zawadi zinatolewa kwa wanaofanya vizuri ili kuleta hamasa kwa wanafunzi kusoma kwa bidii. Akitangaza matokeo hayo, amesema jumla ya wanafunzi 270 walifanya jaribio hilo la pamoja ambapo waliopata daraja A ni wanafunzi 112, daraja B ni wanafunzi 150 na daraja C ni wanafunzi 08. Katika hatua nyingine Bi Fatuma amekiri kuwa ushindani ni wa hali ya juu sana maana mtoto aliyeongoza mtihani uliopita amekosekana kumi bora lakini aliyeongoza leo mtihani uliopita hakuwepo kumi bora. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. WITO WATOLEWA KWA WAZAZI NA WALIMU WA SHULE ZA SERIKALI MANISPAA YA KINONDONI. NI KATIKA MWENDELEZO WA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA MITIHANI ... + Read more »
KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU KINONDONI, YATAKIWA KUBUNI MBINU MBADALA ZA KUONGEZA VYANZO VYA MAPATO KATIKA HALMASHAURI YAO Ushauri huo umetolewa leo na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mh.Benjamini Sitta katika kikao cha majumuisho ya ziara hiyo baada ya kutembelea miradi ya elimu kilichofanyika katika ukumbi w mikutano wa Manispaa. Amesema kamati ya huduma za uchumi, afya na elimu ndio injini ya Halmashuri kwani inagusa sekta muhimu za uchumi na afya ambazo moja kati yake isipoenda sawia basi hakuwezi kuwa na mafanikio. Amesema" Hii kamati ya Huduma za Uchumi ni ya muhimu sana, lakini mmejikita sana kwenye miradi ya elimu, mnasahau sekta muhimu ya uchumi na afya, mimi nadhani wakati umefika sasa muje na mikakati mipya ya kukuza uchumi kwa kuibua vyanzo vipya vya mapato" Mh Sitta. Akipokea ushauri huo kutoka kwa mstahiki Meya, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Thadeus Massawe ameahidi kuufanyia kazi, yeye pamoja na timu yake nzima, na kumshukuru Mstahiki Meya kwa ushauri huo wenye tija kwa Halmashauri yetu. Kamati hiyo katika ziara yake, imetembelea na kukagua miradi mitatu ya shule ambayo ni ; shule ya Msingi na awali Liberman iliyopo Kawe, Shule ya awali Del Paul iliyopo Wazo na Shule ya awali Mbweni Heights iliyopo Mbweni. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU KINONDONI, YATAKIWA KUBUNI MBINU MBADALA ZA KUONGEZA VYANZO VYA MAPATO KATIKA HALMASHAURI YAO Us... + Read more »