BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LAMPONGEZA MKURUGENZI KWA UFAULU MZURI WA DARASA LA SABA 2019 Posted On: November 28th, 2019 Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni limempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo , Aron Kagurumjuli kwa jitihada zake zakuwezesha kufanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba. Wakizungumza katika kikao cha robo ya kwanza ya mwaka kilichofanyika leo, madiwani hao wameeleza kuwa Mkurugenzi Kagurumjuli amekuwa na ushirikiano mzuri na watendaji wake na hivyo kufanikisha kufanya vizuri kwenye matokeo ya darasa la saba. Naibu Meya wa Halmashauri hiyo, Mhe. George Manyama amesema kuwa kama halmashauri imejipanga kuhakikisha kuwa wanafunzi wote waliomaliza darasa la saba wanapata nafasi ya kusoma na kwamba hakuna atakaye kaa nyumbani. Amefafanua kuwa ushindi huo uliopatikana ni dira inayoonyesha kuwa hata matokeo ya kidato cha nne yatakuwa mazuri na kwamba Halmashauri ya Kinondoni itaongoza. “ Niseme tu haya ni matokeo mazuri kwetu, baraza limepitisha maadhimio ya kubadili shule ya msingi Kijitonyama kuwa Sekondari, huu ni mpango uliofanywa na wataalamu wa Halmashauri yetu, lakini pia bado tunaendelea kufanya upembuzi yakinifu kuangalia shule nyingine ambazo tunaweza kuzigeuza kuwa Sekondari. Diwani wa Kata ya Mwananyamala Mhe.Songoro Mnyonge amesema kuwa Halmashauri ya Kinondoni katika matokeo yake ya darasa la saba mwaka huu imeshika nafasi ya tatu kitaifa huku kimkoa ikishika nafasi ya kwanza na kuongeza kuwa matokeo hayo yanatokana na jitihada za Mkurugenzi Kagurumjuli kwani amekuwa akiwasimamia vyema watendaji wake sambamba na kutoa ushirikiano jambo ambalo limewezesha kupata matokeo hayo mazuri. Amesema kuwa kama madiwani watashirikiana kuhakikisha kuwa wanafunzi wote waliofaulu wanapata nafasi ya kuingia kidato cha kwanza kwakuwa shule zipo na kwamba hakuna mwanafunzi ambaye atakaa nyumbani kwakukosa nafasi. “ Pamoja na pongezi hizi, ni wakati sasa wakuhakikisha kuwa wote wanakwenda kusoma , kama baraza leo hii tumeadhimia kuwa shule ya msingi Kijitonyama itabadilishwa na kuwa Sekondari, shule hii inavyumba 20 vya madarasa , hivyo wote watapata nafasi ya kusoma” amefafanua Mhe.Songolo. Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kunduchi Michale Urio , amesema kuwa suala la elimu bure lililotolewa na Mhe. Rais Dk. John Magufuli, limewezesha kuwa na idadi kubwa ya watoto wanaosoma, hivyo Halmashauri itaendelea kuweka jitihada za kuhakikisha kuwa wanapata nafasi za kusoma. Imetolewa na Kitengo cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LAMPONGEZA MKURUGENZI KWA UFAULU MZURI WA DARASA LA SABA 2019 Posted On: November 28th, 2019 Baraza la Mad... + Read more »
MADIWANI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA KUJIFUNZA NAMNA YA UKUSANYAJI MAPATO KATIKA HALMASHAURI YA KINONDONI Posted On: November 27th, 2019 Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro wamefanya ziara ya kujifunza namna ya ukusanyaji mapato katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Madiwani hao waliokuwa wameambata na Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Regina Chonjo, Mstahiki Meya Amir Nondo wamepokelewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli na Mstahiki Meya Benjamini Sita. Aidha madiwani hao pia wamepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo , Katibu Tawala Stela Msofe pamoja na watumishi wengine wa Idara na vitengo ambapo pamoja na mambo mengine walipata nafasi ya kutembelea miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo Soko la Kisasa la Magomeni linalojengwa kwa shilingi bilioni 8.9. Awali kabla ya kutembelea miradi hiyo , madiwani hao walipata nafasi ya kujifunza mbinu mbalimbali za ukusanyaji wa mapato zilizotolewa na Msimamizi wa Mapato wa Halmashauri ya Kinondoni Zahoro Rashidi. Akizungumzia ziara hiyo, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Morogoro Mhe. Nondo alisema kuwa wamekuja kujifunza namna ya ukusanyaji wa mapato kwakuwa Halmahauri ya Kinondoni imekuwa ikifanya vizuri kwenye ukusanyaji. “ Tumekuja kujifunza namna ya ukusanyaji mapato, ukiangalia kwenye takwimu zetu sisi tupo nyuma, sasa leo tumekuja kuona wenzetu mnafanyaje hadi mnafikia malengo, wote ni wamoja tunategemeana ,tunaomba mtupatie ujuzi mliokuwa nao” alisema Mhe. Nondo. Kwaupande wake Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Chonjo alisema aliishukuru Manispaa ya Kinondoni kwakuwapokea vizuri na kueleza kuwa wamefurahishwa na ukarimu waliopata kutoka kwa viongozi na watendaji wa Halmashauri hiyo. “ Lengo letu na kuja hapa ni kujifunza, tunawashukuru mmetukaribisha , undugu tuliouanzisha hapa isiwe mwisho, karibuni na nyinyi Morogoro, hili tunalolifanya ndio lile linalotakiwa na Rais Dk. John Magufuli, asanteni kwa ushirikiano wenu” alisema Mhe. Chonjo. Akiwakaribisha Madiwani hao, Mstahiki Meya . Mhe. Sita alisema kuwa Halmashauri ya Kinondoni ipo vizuri kwenye ukusanyaji wa mapato na kwamba anawakaribisha ili waweze kujinza kwa lengo la kutimiza adhma hiyo. Naye Mhe. Chongolo ambaye ni Mkuu wa Wilaya hiyo alisema kuwa ili kufikia malengo ,viongozi hawana budi kuweka juhudi na nia ya dhati katika kutekeleza majukumu yao na kwamba kila mmoja anapaswa kushiriki kikamilifu katika kutekeleza wajibu wake. “ Bila kuweka malengo ya dhati kabisa, tunaweza kufanya ziara za kujifunza tukamaliza maeneo yote, natusipae kitu, kikubwa ni kuweka nia, kama ilivyo kwa wenzetu wa kabila la hehe wakisema wanajinyonga basi wanajinyonga kweli, inamana waliweka nia , kwahiyo nasisi viongozi tuwaige wahehe katika kuweka nia ya kuleta maendeleo. Imetolewa na Kitengo cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. MADIWANI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA KUJIFUNZA NAMNA YA UKUSANYAJI MAPATO KATIKA HALMASHAURI YA KINONDONI Pos... + Read more »
KINONDONI YAPOKEA UGENI TOKA ZANZIBAR KWA LENGO LA KUJIFUNZA MASUALA YA USHIRIKA Posted On: November 25th, 2019 Halmashauri ya Manispaa ya kinondoni imepokea ugeni toka Zanzibar ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya kazi,Uwezeshaji, Wazee,Wanawake na Watoto Bi Maua Rajab, Mrajis wa idara ya Ushirika pamoja na viongozi na watendaji wa FARAJA Union waliofika kwa lengo la kubadilishana uzoefu na changamoto na wenzao wa kinondoni katika kuendesha vyama vya ushirika. Bi Maua amesema wamechagua Kinondoni sababu wanaamini wapo vizuri katika kuendesha vyama vya ushirika hususan kwa kutumia mfumo laini kwaaajili ya usimamizi na upatikanaji wa taarifa za vyama kwa wakati na kwa usahihi. Naye Mrajis wa Idara ya Ushirika Zanzibar Bw Hamis Daudi Simba amesema kuwa Zanzibar wana muungano wa vyama na saccos mbalimbali (FARAJA) hivyo wanaziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ambayo wamefanikiwa katika masuala ya Ushirika ili na wao waweze kuboresha Umoja wao. Awali alitoa taarifa ya vyama vya ushirika kwa Manispaa ya kinondoni, Afisa Ushirika wa Manispaa Bi Scholastica Maganga amesema Kinondoni ina vyama vya ushirika 153 Kati ya hivyo vyama 137 Ni vya akiba na mikopo na 16 ni vya huduma mbalimbali ikiwemo chama Cha ujenzi wa nyumba. Amesema vyama hivi vina jumla ya wanachama zaidi ya 54000 ambao wamewekeza hisa zaidi ya TShs 15 Bilioni na akiba zaidi ya Bilioni 64 na mikopo zaidi ya Bilioni 35. Aidha sehemu ya Ushirika Manispaa ya Kinondoni kwa sasa inakamilisha mfumo laini kwaaajili ya usimamizi na upatikanaji wa taarifa za vyama kwa wakati na kwa usahihi. Ugeni huo umepata fursa ya kutembelea wat saccos na chama Cha ujenzi wa Nyumba Mwenge vyama vya kijamii ambavyo vina mfano mzuri wa kuigwa hivyo ni sehemu nzuri kwao kujifunza Mambo mengi ya ushirika Imeandaliwa na Kitengo Cha habari na uhusiano Manispaa ya kinondoni. KINONDONI YAPOKEA UGENI TOKA ZANZIBAR KWA LENGO LA KUJIFUNZA MASUALA YA USHIRIKA Posted On: November 25th, 2019 Halmashauri ya Manispaa... + Read more »
DC CHONGOLO AKABIDHI MADARASA, OFISI ZA WALIMU KATIKA SHULE YA SEKONDARI TWIGA NA KIGOGO ,AMPONGEZA MKURUGENZI Posted On: November 26th, 2019 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo amekabidhi madarasa sita na ofisi tatu za walimu katika Shule ya Sekondari Kigogo iliyopo Kata ya Kigogo na Shule ya Sekondari Twiga iliyopo Kata ya Wazo ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa kujenga vyumba 100 vya madarasa ili kuondoa tatizo la wanafunzi wanaomaliza darasa la saba kukosa nafasi ya kwenda shule kwa changamoto ya upungufu wa madarasa. Akizungumza katika uzinduzi huo, Mhe. Chongolo amesema ujenzi huo unaendelea kwa juhudi zake binafsi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wapenda maendeleo katika wilaya yake, hivyo anawashukuru wadau hao walioshirikiana naye kwani kukamilika kwa madarasa hayo kutasaidia wanafunzi wote wanaomaliza darasa la saba kuendelea na masomo ya Sekondari badala ya kukaa nyumba. Amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli iliamua kutoa elimu bure kwa kila mmoja ili kuhakikisha kwamba hakuna mtoto anayekaa nyumbani bila kusoma na kwamba atahakikisha madarasa hayo yanakamilishwa ili kutimiza adhma hiyo. Amefafanua kuwa kutokana na mpango wa elimu bure uliotolewa na Rais Dk. Magufuli kumekuwa na ongezeko kubwa la watoto wanaoandikishwa shule hivyo serikali itahakikisha kila mmoja anapata nafasi ya kusoma wakiwa kwenye vyumba vya madarasa. “ Awali tulikuwa na changamoto ya walimu lakini Mhe. Rais amehakikisha kuwa changamoto hiyo imekwisha ,hivi sasa tunachangamoto ya vyumba vya madarasa , hili nalo litakwisha, niwahakikishie serikali ya awamu ya tano ipo pamoja na wananchi wake” amesema Mhe. Chongolo. Nakuongeza kuwa” leo hii nimekuja mwenyewe kuzindua madarasa haya ili kuona ufanisi uliopo, niseme tu kwamba nimeridhishwa na nimefurahi kuona madarasa haya yamekamilika, sasa imebaki viti na meza ili wanafunzi waweze kusoma na nimeambiwa tayari vimeshaagizwa. Aidha amempongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Ndugu Aron Kagurumjuli kwa kuwa begakwabega na yeye katika kusimamia na kuhakikisha lengo la ujenzi wa vyumba 100 vya madarasa kwenye Halmashauri yake linatimia. Katika hatua nyingine Mhe. Chongolo amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao kwani viongozi wamekuwa wakifanya jitihada za kutosha kuhakikisha kwamba wanapata madarasa ya kusomea. Imetolewa na Kitengo cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. DC CHONGOLO AKABIDHI MADARASA, OFISI ZA WALIMU KATIKA SHULE YA SEKONDARI TWIGA NA KIGOGO ,AMPONGEZA MKURUGENZI Posted On: November 26th, ... + Read more »
DC CHONGOLO AMUAGIZA KAMANDA WA TAKUKURU KINONDONI KUMKAMATA NA KUMCHUNGUZA MKANDARASI ANAYEDAIWA KUIBA MILIONI 54 ZA WANANCHI Posted On: November 22nd, 2019 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo amemuagiza Kamanda wa Takukuru Mkoa maalumu wa Kinondoni kumchunguza Mkandarasi wa Savei anayesimamia urasimishaji makazi ya wananchi kanda ya Madale two , David Emanuel kutokana na tuhuma ya kudaiwa kuiba kiasi cha shilingi milioni 52 fedha zilizochangwa na wananchi. Ameongeza kuwa milioni 52 zimelipwa pasipokufuata utaratibu kutokana na mkandarasi huyo kuwa sehemu ya waweka saini katika akaunti ya wananchi na kwamba alichokuwa anakifanya nikwenda mwenyewe benki na kuchukua fedha.. Mhe. Chongolo amefikia uamuzi huo leo katika kikao chake na Kamati zilizoundwa na wananchi kwa ajili ya kuratibu na kusimamia zoezi la urasimishaji pamoja na wakandarasi waliopewa jukumu la urasimishaji makazi ya wananchi katika Halmashauri hiyo . Mhe. Chongolo ameeleza kuwa mkandarasi huyo alijilipa mwenyewe fedha hizo pasipokufuata utaratibu na kwamba kitendo hicho ni matumizi mabaya ya fedha za wananchi na kuagiza Takukuru Kinondoni kumchukulia hatua pindi atakapobainika ukweli dhidi ya tuhuma hizo. Amefafanua kuwa katika kanda hiyo, viwanja zaidi ya 1800 vimerasimishwa na hivyo wananchi wamechanga kiasi cha shilingi zaidi ya milioni 70 na kwamba hadi sasa mkandarasi huyo ameshalipwa shilingi milioni 62 ambapo kati ya hizo milioni 12 ndio zilizolipwa kwa kufuata utaratibu. “ Sasa ukiona hivi unajua kabisa kunachangamoto ya matumizi yasio yasihi ya fedha za wananchi,nimechukua hatua nimemkabidhi Kamanda wa Takukuru mkoa maalumu wa Kinondoni, wamemchukua wanakwenda kushugulikia kufanya uchunguzi na pale watakapobaini kunaukiukwaji watamchukulia hatua” amesema Mhe. Chongolo. Nakuongeza kuwa” kulingana na changamoto ambayo tumeibaini leo kwenye mtaa mmoja, nimeagiza kitengo cha ukaguzi wa ndani kwenda kukagua akaunti zote za urasimishaji ndani ya Halmashauri yetu ,ili kujiridhisha na yale watakayo yabaini sisi watuletee ripoti ilituweze kuchukua hatua stahiki kwa wakati muafaka”. Awali Mhe. Chongolo amesema kuwa katika mkutano huo wanapokea taarifa ya kila mkandarasi juu ya mwenendo na matumizi ya fedha zinazochangwa kutoka kwa wananchi ilikukamilisha zoezi husika la urasimishaji. Amebainisha kuwa , katika mkutano huo amejifunza kuwepo na changamoto ya usimamizi wafedha za wananchi katika maeneo mengi yanayoendesha zoezi hilo ipo haja ya haraka katika kutatua changamoto hizo. Imetolewa na Kitengo Cha habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. DC CHONGOLO AMUAGIZA KAMANDA WA TAKUKURU KINONDONI KUMKAMATA NA KUMCHUNGUZA MKANDARASI ANAYEDAIWA KUIBA MILIONI 54 ZA WANANCHI Posted On:... + Read more »
ALAT YAIPONGEZA MANISPAA YA KINONDONI KWA KUTEKELEZA MIRADI MIKUBWA KWA KUTUMIA FORCE ACCOUNT, YATAKA HALMASHAURI NYINGINE ZIIGE Posted On: November 21st, 2019 Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania ( ALAT) imeipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kwa kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati kwakutumia Local Fundi (Force Account). Akizungumza na watendaji wa Halmashauri hiyo mara baada ya kukamilisha ziara ya kukagua miradi ya Halmashauri hiyo, Makamu Mwenyekiti wa ALAT , Stephano Mhapa amesema kuwa Mkurugenzi Mtendaji Aron Kagurumjuli na timu yake wamefanikisha kujenga miradi mikubwa ya maendeleo kwa kutumia mafundi wa kawaida jambo ambalo limeonyesha nizamu ya matumizi mazuri ya fedha za serikali. Amefafanua kuwa mradi wa Zahanati ya Mikoroshini iliyopo Kata ya Msasani imejengwa kwa shilingi milioni 400.8 kwa kutumia mafundi wa kawaida wakati kwa mkandarasi wakutangaza tenda ingetumia milioni 700 na kwamba Halmashauri hiyo imeokoa kiasi cha shilingi milioni 300. Aidha Mhapa amesema kuwa“ ukiangalia Zahanati hii imekamilika vizuri na imara , tumejionea wenyewe, Mkurugenzi na timu yako tunakupongeza sana, na halmashauri nyingine ziige mfano huu kutoka kwako, kazi ni kubwa uliyoifanya lakini gharama yake ni ndogo, haya ni matumizi mazuri ya fedha za serikali.” Akizungumzia mradi wa Soko la kisasa la Magomeni, linalojengwa kwa shilingi zaidi ya bilioni 8.9 na Kituo cha Afya kilichopo Kigogo kinachojengwa kwa shilingi milioni 700 , Mhapa amesisitiza kuwa Halmashauri ya Kinondoni inapaswa kuigwa na Halmashauri nyingine kwa kazi kubwa wanayoifanya sambamba na kuwa na matumizi mazuri ya serikali. “ Halmashauri ya Kinondoni tangu mwaka 2015 imekuwa ikipata hati safi na hiyo ni kutokana na kuwa na nidhamu ya matumizi mazuri ya fedha za serikali, hati safi inamanisha kwamba mnapokea pesa za serikali lakini pia mnakusanya mapato ya ndani na kuyatumia vizuri” ameongeza. Kuhusu asilimia 10 ya fedha kwa ajili ya mikopo ya vijana , wakina mama na walemavu,ambayo ni bilioni tatu, Katibu wa ALAT Elirehema Kaaya ameipongeza Halmashauri kwakufanya vizuri kwani kiasi hicho cha fedha ni sawa na bajeti nzima ya Halmashauri nyingine. Kaaya amesisistiza kuwa kazi anayoifanya Mkurugenzi Kagurumjuli ndio inayotakiwa na Rais Dk. John Magufuli na hivyo kuagiza Halmashauri nyingine ziige mfano wake. “ Umefanya matumizi mazuri na sahihi ya fedha ambazo ni kodi za wananchi wanyonge, kilichofanyika na Mkurugenzi mtedaji wa Kinondoni ni kwamba , Mhe. Rais Magufuli na Waziri wa Tamisemi Suleman Jafo wanasisitiza kutumia local fundi (Force Account) ninashauri wakurugenzi wengine wasikilize maagizo yanatotolewa na serikali.” Amesisitiza Kaaya. Awali akizungumza na viongozi wa ALAT, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Ndg Aron Kagurumjuli amesema kuwa Halmashauri imefanikiwa kupata bilioni 32.8 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa miradi mitatu ya kimkakati ambayo itaongeza mapato kwa kiasi kikubwa. Kagurumjuli alitaja miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa soko la kisasa la Magomeni, wenye thamani ya shilingi bilioni 8.9, ujenzi wa soko la kisasa la Tandale wenye thamani ya shilingi bilioni 8.7 na uboreshaji wa fukwe ya Osterbay (Coco Beach) wenye gharama ya shilingi bilioni 13. Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni ALAT YAIPONGEZA MANISPAA YA KINONDONI KWA KUTEKELEZA MIRADI MIKUBWA KWA KUTUMIA FORCE ACCOUNT, YATAKA HALMASHAURI NYINGINE ZIIGE Posted O... + Read more »