UJENZI WA BARABARA YA RASHIDI UMEANZA RASMI MARA BAADA YA KUKAMILIKA KWA ZOEZI LA ULIPAJI FIDIA Posted On: October 3rd, 2019 Ujenzi wa barabara ya Rashidi yenye urefu wa Km 0.85 umeanza rasmi Mara baada ya kukamilika kwa zoezi la ulipwaji wa fidia kwa wananchi ambao watapitiwa na mradi huo. Akikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe Daniel Chongolo amesema Ujenzi wake ni utekelezaji wa agizo la Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli. Mhe Chongolo amesema kuwa akiwa msimamizi mkuu wa shughuli za serikali katika wilaya hii amekuja kuangalia maendeleo ya mradi huo na kuona Kama kuna changoto zozote waweze kuzitatua kwa wakati na hivyo kuwezesha mradi huo kukamilika kwa wakati. Aidha amesema kukamilika kwa mradi huo kutapunguza kero ya mafuriko ambayo yalikua yanatokea katika maeneo hayo msimu wa mvua hapo awali kwani Ujenzi wa barabara hiyo utahusisha Ujenzi wa mifereji mikubwa ya maji itakayosaidia kupeleka maji baharini. Kwa upande wake Msimamizi wa barabara hiyo toka TARURA Mhandisi Lydia Machibya amesema barabara hiyo itajengwa kwa awamu kwani mchoro wa barabara hiyo unaonesha barabara hiyo inamuunganiko na barabara nyingine, hivyo kwasasa ujenzi utaanza kwa awamu ya kwanza. "Nyumba 51 zinatakiwa kupisha mradi huo ili uweze kukamilika kwa wakati ambapo baadhi yao tayari wameshaaanza kubomoa nyumba zao wenyewe kwani tayari wameshapata fidia zao" amesema Mhandisi Lidya Aidha wananchi wanaoishi maeneo hayo wamemshukuru Mkuu wa wilaya ya Kinondoni kwa kuwa nao begakwabega, na kufanya vikao vya marakwamara kupokea maoni ya wananchi katika kuhakikisha ujenzi wa barabara hii unakamilika kwa wakati. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. UJENZI WA BARABARA YA RASHIDI UMEANZA RASMI MARA BAADA YA KUKAMILIKA KWA ZOEZI LA ULIPAJI FIDIA Posted On: October 3rd, 2019 Ujenzi wa ... + Read more »
MKUU WA WILAYA YA KINONDONI ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA NYUMBA ZA MAGOMENI KOTA Posted On: October 2nd, 2019 Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe Daniel Chongolo ameridhishwa na Kasi ya ujenzi unaoendelea wa nyumba za magomeni kota ambao kwa sasa unaenda kwa Kasi. Mhe Chongolo amebainisha hayo leo alipotembelea ujenzi huo kwa lengo la kujionea maendeleo ya ujenzi na kuangalia Kama kuna changamoto zozote zinazoukabili mradi huo. Amesema anawapongeza Sana TBA kwa kutoa ajira kwa vijana zaidi ya 700 wanaoishi maeneo ya karibu ambao wamepata nafasi za ufundi na vibarua, wasambazaji wa vifaa vya ujenzi zaidi ya 30 na watoa huduma wa chakula zaidi ya 38 ambao wanapata mahitaji yao ya kila siku kupitia mradi huo. Aidha Amepongeza juhudi zao za kupunguza matumizi yasiyo ya lazima kwa kuanzisha kiwanda kidogo Cha kutengeneza matofali, matofali ambayo yanatumika katika kukamilisha ujenzi huo. Kwa upande wake msimamizi mkuu wa mradi huo Bw Bernard Manyema amesema mradi huo ambao unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba mwaka huu umekamilika katika hatua ya uwekaji wa miundombinu ya awali ya umeme na maji na sasa wanaendelea na zoezi la kupiga lipu nyumba zote. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. MKUU WA WILAYA YA KINONDONI ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA NYUMBA ZA MAGOMENI KOTA Posted On: October 2nd, 2019 Mkuu wa wilaya ya Kino... + Read more »
MWAKYEMBE AIPONGEZA KINONDONI KWA KUFANYA VIZURI KATIKA SEKTA YA MICHEZO Posted On: October 2nd, 2019 Waziri Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe Harrison Mwakyembe ametoa pongezi hizo leo alipotembelea Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kwa lengo la kuwapongeza na kuwatia hamasa viongozi wanaofanya kazi iliyotukuka katika kukuza michezo nchini. Mhe Mwakyembe ameyataja maeneo ambayo Kinondoni kupitia Timu yake ya mpira wa miguu KMC imefanya vizuri kuwa ni pamoja na Kupanda ligi kutoka daraja la kwanza na kumaliza ligi kuu ikiwa nafasi ya nne msimu uliopita. Amepongeza mipango ya kujenga uwanja wa kisasa wa soka katika eneo la Mwenge, Kuanzisha Academy ya kulea vipaji vya soka kwa watoto na kuwa na Jezi bora kabisa ambapo KMC imekuwa timu inayoogopwa nchini. Aidha ameahidi kuwa Wizara yake itakuwa bega kwa bega na Manispaa ya Kinondoni katika kuhakikisha mipango waliyojiwekea ya kuhakikisha Soka linaenda mbele zaidi inafanikiwa. Awali akitoa taarifa mbele ya Mhe Waziri, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe Benjamin Sitta amesema uwanja unaotarajiwa kujengwa katika eneo la mwenge utatumika kama uwanja wa nyumbani kwa timu ya KMC, kutakuwa na hostel za vijana wa Academy na pia kutakuwa na fremu kwaaajili ya biashara nyingine. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. MWAKYEMBE AIPONGEZA KINONDONI KWA KUFANYA VIZURI KATIKA SEKTA YA MICHEZO Posted On: October 2nd, 2019 Waziri Habari, Utamaduni,Sanaa na... + Read more »
WATENDAJI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA USHIRIKIANO NA MSHIKAMANO ILI KUKAMILISHA MIRADI ITAKAYO SOGEZA HUDUMA KWA WANANCHI Posted On: October 1st, 2019 Hayo yamebainishwa leo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Daniel Chongolo alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea Miradi ya ujenzi wa Zahanati wilayani hapa. Akiongea na wajumbe wa kamati ya kuratibu ujenzi wa Zahanati ya Makumbusho Mhe Chongolo amesema kuwa, kila hatua inatakiwa iwe na ushirikiano bainifu na wenye uwazi ambao hauwezi kuleta wasiwasi kwa yeyote. "Hawa Wananchi tunaowahudumia msiwaone kama vile hawajui kitu, wanauelewa na uzoefu uliotukuka, wengine ni mafundi na wajua gharama za vifaa vya ujenzi", Ameongeza Mh Chongolo. Mhe Chongolo amesema kuwa Zahanati za Magomeni na Makumbusho zitasaidia kupunguza msongamano uliopo Mwananyamala na hata ule ambao ungeweza kutokea katika hospitali ya wilaya inayojengwa Mabwepande baada ya kukamilika kwake. Katika hatua nyingine Mh Chongolo ametoa siku 25 kwa mjenzi wa Zahanati ya Magomeni awe amekamilisha hatua ya awali pasipo kuchelewa maana Wananchi wanahitaji kusogezewa huduma ya afya karibu. "Sisi tumepewa jukumu la kuhakikisha ilani ya chama cha mapinduzi inatekelezwa pasipo na dosari yoyote, kesho na keshokutwa hatutakuwa tayari kujibu maswali yenye majibu yake leo" Amesema Mh Chongolo. Miradi iliyotembelewa na mkuu wa wilaya katika ziara hiyo ni pamoja na ujenzi was zahanati za Magomeni na Makumbusho na Mradi wa Hospitali ya wilaya inayojengwa kata ya Mabwepande. Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. WATENDAJI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA USHIRIKIANO NA MSHIKAMANO ILI KUKAMILISHA MIRADI ITAKAYO SOGEZA HUDUMA KWA WANANCHI Posted On: Octobe... + Read more »
KINONDONI YAADHIMISHA SIKU YA WAZEE DUNIANI KWA KUTOA HUDUMA ZA UPIMAJI WA AFYA BILA MALIPO Posted On: October 1st, 2019 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imeadhimisha siku ya wazee duniani iliyoambatana na kauli mbiu isemayo "Tuimarishe usawa kuelekea maisha ya uzeeni" kwa kutoa huduma za Upimaji afya kwa wazee zaidi ya 200. Maadhimisho hayo yamefanyika leo katika viwanja vya mwinjuma vilivyoko katika Kata ya Makumbusho ambapo mgeni rasmi alikuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh.Benjamin Sitta. Katika kuadhimisha siku ya wazee, Meya Sitta amesema changamoto kubwa inayowakabili wazee ni changamoto ya afya, hivyo Manispaa imeamua kupima afya za wazee hao na kutoa ushauri wa masuala ya afya kwa wazee ili kuweza kuimarisha afya zao. Pia ameitaja mikakati iliyowekwa na Manispaa ya kinondoni katika kuimarisha afya za wazee kuwa ni pamoja na kuhakikisha wanapata kadi za msamaha wa matibabu zitakazowapa uhakika wa matibabu bure katika vituo vyote vya afya na zahanati zote za serikali. Naye Afisa ustawi wa jamii wa Manispaa hiyo amesema Manispaa katika kuhakikisha inawapatia wazee matibabu bure, Tayari imeshagawa vitambulisho 12,183 vya matibabu bure kwa wazee wa kuanzia umri wa miaka 60 na zoezi hili ni endelevu. Katika hatua nyingine mwakilishi wa wazee amebainisha changamoto mbalimbali zinazowakabili kuwa ni pamoja na kukosa baadhi ya dawa katika baadhi ya vituo vya afya, uchache wa vituo vya kulelea wazee wenye mahitaji maalum, posho ya kujikimu ya kila mwezi na kutokuwepo kwa miradi ya wazee ili iweze kuwasaidia kiuchumi. Huduma za afya zilizotolewa katika maadhimisho hayo ni pamoja na kupima pressure, kisukari, macho, elimu ya lishe, pamoja na kuandikisha kadi za msamaha wa matibabu. Imetolewa na Kitengo cha Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YAADHIMISHA SIKU YA WAZEE DUNIANI KWA KUTOA HUDUMA ZA UPIMAJI WA AFYA BILA MALIPO Posted On: October 1st, 2019 Halmashauri ya... + Read more »
JAMII YATAKIWA KUJENGA MAZOEA YA KUCHANJA MBWA NA PAKA ILI KUWAKINGA DHIDI YA UGONJWA HATARI WA KICHAA CHA MBWA Posted On: September 28th, 2019 Wito huo umetolewa na Tabibu wa mifugo mkoa wa Dar es salaam Dr Senorina Mwingira katika kilele cha maadhimisho ya siku ya kichaa cha Mbwa Duniani yanayofanyika kila Tar 28 Septemba ambayo kwa wilaya ya Kinondoni yamefanyika viwanja vya Mbezi Ndumbwi. Dr Senorina amesema Kichaa cha mbwa ni hatari sana kwa binaadamu na wanyama kwani hakina tiba zaidi ya kinga hivyo niwapongeza sana Kinondoni kwa hamasa yenu kuhamasisha wananchi kuchanja Mifugo yao kwani si tu mnailinda jamii bali mnalinda haki za wanyama hawa pia. Naye Afisa Mifugo toka wilaya ya Kinondoni Bi Bertilla Lyimo kwa niaba ya Mkuu wa idara ya Mifugo wa Manispaa hiyo amesema chanjo hiyo itakuwa endelevu na zoezi hilo litafanyika kata kwa kata hivyo amewasihi wanajamii ya Kinondoni kufanya mwendelezo wa chanjo hii kwa manufaa yao na wanyama wao. Aidha amebainisha kuwa, waathirika wakubwa wa athari za kichaa cha mbwa ni watoto chini ya miaka 15, hivyo jamii itakapochukua hatua stahiki itakuwa imewalinda wahanga hao ambao ni watoto. Katika hatua nyingine kabla ya maadhimisho hayo, Manispaa ya Kinondoni ilionesha onesho la sinema kwa wanafunzi zaidi ya 800 toka shule ya msingi Mbezi Ndumbwi linaoelezea madhara ya ugonjwa wa Kichaa cha mbwa kwa binaadamu, ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa wanafunzi hatua za kuchukua endapo itatokea akang'atwa na mbwa au paka ili asiweze kupata ugonjwa hatari wa kichaa Cha mbwa. Manispaa ya Kinondoni imelenga kuchanja mbwa takribani 1342 na paka 246 katika kata zote 20 na hii ni dhamira ya kuendana na kauli mbiu ya mwaka huu isemayo "UGONJWA WA KICHAA CHA MBWA: CHANJA MIFUGO YAKO ILI KUTOKOMEZA UGONJWA HUU(RABIES VAAACCINATE TO ELIMINATE) Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni JAMII YATAKIWA KUJENGA MAZOEA YA KUCHANJA MBWA NA PAKA ILI KUWAKINGA DHIDI YA UGONJWA HATARI WA KICHAA CHA MBWA Posted On: September 28th... + Read more »