ZOEZI LA UGAWAJI WA HATI ZA VIWANJA KWA WANANCHI WA NYAKASANGWE KUANZA RASMIPosted On: June 17th, 2020Zoezi hilo la ugawaji wa hati za viwanja kwa wakaazi wa maeneo ya Nakasangwe ni kufuatia ukamilishaji wa upimaji viwanja 9741vya wananchi hao walioendeleza maeneo kiholela hali iliyopelekea tatizo sugu la uvamizi.Zoezi hilo limetangazwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Daniel Chongolo alipokuwa akiongea na wananchi wa Nakasangwe, katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo viwanja vya shule ya msingi Nakasangwe.Amesema kwa kuwamilikisha Wananchi maeneo yao kisheria kutapunguza na kumaliza kabisa migogoro ya ardhi iliyokuwa ikiwakabili siku za nyuma."Ninafahamu Katika kata hizi za pembezoni hususani Mabwepande kumekuwa na watu wachache wanaojishughulisha na uvamizi wa maeneo na kuwauzia Wananchi hali inayopelekea migogoro, Nipende tuu kuwakumbusha kuwa magereza zetu nchini zinahitaji nguvu Kazi, serikali haitokubali kuwaacha watu Hawa waendelee kusababisha migogoro kwenye maeneo yetu."Naye mkuu wa Idara ya Ardhi na Mipango Miji Manispaa ya Kinondoni Ndg. Maduhu Kazi amesema ugawaji huo wa hati ni kufuatia utekelezaji wa maagizo ya Serikali yanayozitaka Manispaa kupima meneo yote yalioendelezwa kiholela.Amesema viwanja vilivyopimwa ni 9741 ambapo kulikuwa na makundi ya wenye migogoro na wasio na migogoro na kuwataka wanachi kufahamu kuwa ugawaji wa hati unaoanza kesho utahusisha maeneo ambayo hayakuwa na changamoto za migogoro.Katika hatua nyingine, Mhe.Chongolo ameagiza wataalamu wa Manispaa kuanza kupima mtaa wa Mbopo uliopo Kata ya Mabwepande ndani ya siku 14, na kuwataarifu wanachi wanaosababisha migogoro kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.Zoezi la upimaji wa viwanja ni endelevu na litafanyika kwa awamu likihusisha maeneo yote yaliyoendelezwa kiholela.Imeandaliwa naKitengo Cha habari na uhusianoManispaa ya Kinondoni. ZOEZI LA UGAWAJI WA HATI ZA VIWANJA KWA WANANCHI WA NYAKASANGWE KUANZA RASMI Posted On: June 17th, 2020 Zoezi hilo la ugawaji wa hati za viw... + Read more »
MKURUGENZI KINONDONI AWATAKA BVR KITS OPERATORS, KUZINGATIA KANUNI NA TARATIBU ZA UBORESHAJI DAFTARI AWAMU YA PILIPosted On: May 1st, 2020Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imeanza zoezi la uboreshaji awamu ya pili wa daftari la kudumu la mpiga kura ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ambaye ndio Afisa mwandikishaji bwana Aron Kagurumjuli amesema wamejipanga vilivyo katika uboreshaji huo.Kagurumjuli ametoa kauli hiyo wakati wamafunzo ya kuwajengea uwezo mbalimbali kuhusu namna ya kuwahudumia wananchi wanaokuja kuboresha taarifa zao sambamba na namna ya kutumia mashine wakati wa kuchukua picha kwa ajili ya kutoa vitambulisho. Kagurumjuli amesema kuwa Halmashauri yake imejipanga vizuri katika mchakato huo na kwamba inategema matokeo mazuri ya mwitikio wa wananchi kama ilivyokuwa kwa awamu ya kwanza kutokana na kuwepo kwa ushirikiano madhubuti baina ya AROKATA pamoja na watendaji wengine wa Hamashauri hiyo.Ameongeza kuwa mchakato huo ni mahususi kwa ajili ya kuwapatia wananchi vitambulisho vyao na kuwataka wale ambao walipitwa na mchakato huo kwa awamu ya kwanza kujitokeza sasa ili waweze kupata vitambulisho vyao. “ Nawapongeza wote mliopata nafasi hii, kiapo mlichokula hapa ni cha uaminifu na uadilifu, mnakwenda kuwahudumia wananchi, niwasihi hatuhitaji muende kinyume na maelekezo ambayo mnapewa na watalaamu wetu kwenye mafunzo haya, wahudumieni wananchi vizuri” amesema Kagurumjuli.Aidha Kagurumjuli amewataka watumishi hao kuzingatia maelekezo wanayopewa na watalaamu kuhusu namna ya kumuhudumia mwananchi hasa katika kipindi hiki cha ugonjwa wa mlipuko wa homa ya mapafu unaosababishwa na Virusi vya COVID 19 (Corona) ikiwemo kunawa mikono na maji tiririka pamoja na kupaka vitakasa mikono (Sanitizer).Amesema kuwa katika kila kituo kutakuwa na watu ambao watakuwa ni mahususi kwa ajili ya kuwanawisha mikopo pamoja na kuwapaka vitakasa mikono ili kuwakinga na maambukizi ya ugonjwa huo.Kagurumjuli amefafanua kuwa zoezi hilo la uandikishaji litaanza rasmi Mei mbili na kumalizika Mei Nne mwaka huu na kwamba wote ambao hawakupata nafasi ya kujiandikisha awamu ya kwanza wanaruhusiwa kwenda kwenye vituo vyao kwa ajili ya kujiandikisha. Imeandaliwa na kitengo cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni MKURUGENZI KINONDONI AWATAKA BVR KITS OPERATORS, KUZINGATIA KANUNI NA TARATIBU ZA UBORESHAJI DAFTARI AWAMU YA PILI Posted On: May 1st, 2020 ... + Read more »
WAJUMBE WA MABARAZA YA KATA MANISPAA YA KINONDONI WATAKIWA KUSIMAMIA SHERIA KATIKA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHIPosted On: June 12th, 2020WAJUMBE WA MABARAZA YA KATA MANISPAA YA KINONDONI WATAKIWA KUSIMAMIA SHERIA KATIKA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI. Wajumbe wa Mabaraza ya Kata Manispaa ya Kinondoni wametakiwa kusimamia sheria ikiwa ni pamoja na kutoa haki kwa Wananchi kuhusiana na masuala ya migogoro ya Ardhi yanapoletwa kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi. Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo jana alipokutana na wajumbe wa Mabaraza hayo kikao kilichokuwa na lengo la kujadili changamoto mbalimbali zinazo wakabili ambapo pamoja na mambo mengine amewakumbusha kutambua wajibu na majukumu yao.Alisema katika kutambua wajibu wao ni vema wakajiepusha kujihusisha na vitendo vya rushwa kwakuwa vinaweza kuharibu uaminifu waliopewa na Halmashauri pamoja na kusababisha migogoro kwa Wananchi.Katika kikao hicho pia Mhe. Chongolo na wajumbe wa Mabaraza hayo wamejadili hatua zitakazo wawezesha kupunguza kama sio kumaliza kabisa migogoro katika Wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto za wananchi na hivyo kuleta tija na ufanisi wa utendaji wa kazi zao.Aidha amewataka wajumbe hao kuweka utaratibu wa kutembelea maeneo ambayo yanashukiwa kuwa na migogoro na kwamba kwakufanya hivyo itakua ni njia sawia katika kukabiliana na changamoto ambazo wananchi wanakutana nazo. “Mabaraza haya yapokisheria, mnanguvu ya kuwachukulia hatua wale ambao wanakiuka sheria zilizoweka, kukaidi maelekezo mnayotoa, msiwe wanyonge fanyeni kazi kwakusimamia haki na sheria kama ambavyo siku zote Rais wetu Dk. John Pombe Joseph Magufuli anatuelekeza” alisema Mhe. Chongolo. Katika hatua nyingine Mhe. Chongolo ameipongeza Idara ya sheria ya Manispaa hiyo kwakufanyakazi bega kwa bega na Mabaraza hayo na hivyo kuleta mafanikio makubwa ya utatuzi wa migogoro ya Ardhi. Wajumbe wa Mabaraza ya Kata wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya Mhe. Daniel Chongolo. Imeandaliwa na Kitengo Cha habari na MahusianoManispaa ya Kinondoni. WAJUMBE WA MABARAZA YA KATA MANISPAA YA KINONDONI WATAKIWA KUSIMAMIA SHERIA KATIKA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI Posted On: June 12th, 2020 WAJU... + Read more »
KINONDONI YATEKELEZA MIRADI YA TAKRIBANI BIL. 242.8 KWA KIPINDI CHA MIAKAMITANO YA RAIS DK.MAGUFULIPosted On: June 10th, 2020KINONDONI YAWEKA HISTORIAYATEKELEZA MIRADI YA TAKRIBAN BILIONI 242.8 KWA KIPINDI CHA MIAKA MITANO, ALAT YATOA TUZO. Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imeweka historia katika suala la utekelezaji wa miradi ya maendeleo na ile ya kimkakati kwa kipindi cha miaka mitano iliyogharimu takribani shilingi bilioni 242.8 fedha zilizotokana na vyanzo vya mapato ya ndani, Serikali kuu na wadau wengine wa maendeleo.Taarifa hii imetolewa wakati wa uwasilishaji wa taarifa za utekelezaji wa shughuli za Serikali kwa kipindi cha miaka mitano katika kikao cha mwisho cha Baraza la Madiwani kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa. Akitoa taarifa hiyo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Ndg.Aron Kagurumjuli amesema Kinondoni imefanikiwa kugusa sekta zote muhimu zinazomuhusu kila mwananchi zikiwemo za uchumi, kisiasa, kijamii pamoja na miradi ya Maendeleo na kuitaja kuwa ni ujenzi na ukarabati wa Vyumba vya Madasara, Vyoo kwa shule za msingi na Sekondari, ununuzi wa madawati kwa shule hizo, ujenzi, ukarabati na upanuzi wa Zahanati , Vituo vya Afya na Hospitali, ujenzi wa miradi ya Masoko na uwekezaji.Ametaja maeneo mengine kuwa ni miradi ya barabara kwa kiwango cha lami km. 189 kutoka km. 134, kupitia mradi wa DMDP, TARURA, uendelezaji wa miradi ya kilimo na mifugo, ujenzi wa kiwanda cha kuchakata taka na kuzalisha mbolea mboji, hali ya ukusanyaji wa mapato ya ndani na utoaji wa asilimia 10 ya mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu.Aidha amefafanua kuwa Halmashauri katika kipindi cha miaka mitano hadi kufikia Juni mwaka huu imetumia kiasi cha shilingi Bil. 3.3 kwa ajili ya kugharamia Elimu ya Msingi bila malipo, Bil. 2.2 Elimu ya Sekondari na hivyo kumpongeza Rais Magufuli kwa kuleta mpango huo.Mbali na fedha hizo, lakini pia Manispaa imefanikiwa kujenga shule nne za Msingi, ujenzi wa vyumba vya madarasa kutoka 983 Oktoba 2015 hadi kufikia 1147, ukarabati wa vyumba 111, matundu ya choo kutoka 686 hadi 1167, ununuzi wa Madawati kutoka 12,962 hadi kufikia 28,705, Maktaba kutoka 13 hadi 22, majengo ya utawala sita pamoja na ofisi za walimu kutoka 49 hadi 62.Kwa upande wa shule za Sekondari Manispaa imefanikiwa “kujenga vyumba vya madarasa 48, katika shule mpya za Mzimuni, Kijitonyama, Magomeni, Mbezi juu, Mivumoni, Shule mpya mbili za Alevel, ukarabati wa vyumba 21, Matundu ya choo kutoka 389 hadi 473, Viti na Meza kutoka 19,353 hadi 25,067, Hosteli moja, Nyumba nne, Walimu maabara kutoka 63 hadi 120, majengo ya utawala saba” ameeleza Kagurumjuli.“ Kwa upande wa Afya tumefanikiwa kujenga Zahanati Nne, vituo vya Afya vitatu ambapo kimoja ni kituo cha Afya Kigogo chenye Ghorofa tano, Hospitali mbili za Ghorofa, upanuzi na ukarabati wa Zahanati sita, Magari ya kubebea wagonjwa matatu, Nyumba za watumishi mbili, Wodi ya Baba, Mama na Mtoto (RCH) 14” ameeleza Kagurumjuli.Kwa upande wa Masoko, amesema “tumekuwa na miradi ya kimkakati na uwekezaji ambayo ni Soko la kisasa la Magomeni, Tandale, vituo vya ukusanyaji wa mapato sita, uwanja wa mpira Mwenge pamoja na Stendi ya daladala ya Mwenge” ameongeza Kagurumjuli.Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala na Serikali za Mitaa (ALAT), Bwana Elirehemu Kaaya akitoa salamu ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kufanya kazi nzuri na kusema kuwa ndio Halmashauri pekee Tanzania iliyoweka historia ya utekelezaji wa miradi yake kwa wakati.Amesema kuwa Halmashauri hiyo pia imeweka historia ya kuwa na Mkurugenzi mchapa kazi, mwadilifu, msikivu, na mwenyekusimamia maendeleo iliyopelekea kutunukiwa cheti cha shukrani ikiwa ni katika kutambua mchango wake katika utekelezaji wa miradi kwa wakati .Naye Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe. Benjamini Sita amesema kuwa Halmashauri hiyo kupitia Mkurugenzi Kagurumjuli imeweka historia Tanzania nzima kwani imefanya mambo makubwa katika kipindi cha uongozi wao na hivyo kumtunuku tuzo ya kutambua mchango wake.Amefafanua kuwa pamoja na mambo mengine wanaondoka wakiwa wameacha alama kubwa ambayo imeacha alama na kusema kuwa iwapo watakuwa na nafasi nyingine ya kurudi watafanya mambo makubwa mengine kwa ajili ya kuwaletea maendeleo Wananchi wa Kinondoni.“Mkurugenzi hongera sana, umefanya mambo makubwa, kwenye uongozi huu tumeshirikiana kama timu, hukujali itikadi za vyama, umewavumilia madiwani wangu, mwisho wa siku umefanya jambo ambalo historia yake tunaiandika leo hii” amesema Mhe. Sita.Mstahiki Meya Benjamini Sitta akimkabidhi Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Aron Kagurumjuli tuzo ya heshima na kutambua mchango wake katika shughuli za utekelezaji wa Serikali katika kipindi cha miaka mitano.Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo akimkabidhi Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe. Benjamini Sitta tuzo ya heshima ya usimamizi wa utekelezaji wa shughuli za Serikali kwa kipindi cha uongozi wake.Imeandaliwa naKitengo cha Habari na UhusinoManispaa ya Kinondoni KINONDONI YATEKELEZA MIRADI YA TAKRIBANI BIL. 242.8 KWA KIPINDI CHA MIAKAMITANO YA RAIS DK.MAGUFULI Posted On: June 10th, 2020 KINONDONI YAW... + Read more »