DC CHONGOLO ASIMAMA KIDETE NA WANAOZURUMU NYUMBA , ATOA ONYO KALI KWA WAHUSIKA, BI SHARIFA ARUDISHIWA NYUMBA YAKE Posted On: November 11th, 2019 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo amesimamia haki na hivyo kuwezesha kurudishwa kwa Nyumba ya mkazi wa Magomeni Mzimuni,Bi Sharifa Mbaruku aliyenyang’anywa kwa muda wa miaka mitatu iliyopita. Mhe. Chongolo alichukua maamuzi hayo leo alipofika kwenye nyumba ya Bi Sharifa ikiwa ni baada ya bibi huyo kupeleka malalamiko ya kudai kuzurumiwa na Bi Magrethi ambaye kwa sasa inadaiwa kuwa anaishi nje ya Nchi. Akizungumza na wandishi wa habari mara baada ya kufika katika nyumba hiyo ,Mhe. Chongolo amesema kuwa aliyemuondoa kwenye nyumba hiyo mwaka 2016 alifanya makosa na kwamba hakuwa na haki ya kumiliki nyumba hiyo. Amefafanua kuwa kazi ya serikali ya awamu ya tano ni kutetea wanyonge wanaozurumiwa haki zao na kwamba akiwa Mkuu wa Wilaya hiyo amerudisha umiliki wa nyumba hiyo kwa mhusika ambaye ni Bi Sharifa. “kuanzia hivi ninavyozungumza unarudi kwenye nyumba yako rasmi, wewe ndio mmiliki wa nyumba hii, kwahiyo nendeni mkaondoe mabati yote ambayo yamezungushiwa na sisi kama serikali tutawachukulia hatua wote waliohusika na mchezo huu" Amesisitiza Mhe Chongolo Katika hatua nyingine Mhe. Chongolo ametoa agizo na kuwataka wote wenye tabia ya kupora nyumba za watu hasa masikini na wanyonge kuacha mara moja kwani hatamuonea haya mtu yeyote aliyekuwa kwenye manispaa yake. Kwaupande wake Bi Sharifa aliyezurumiwa nyumba hiyo, amesema kuwa Disemba 27 mwaka 2016 akiwa amelala ilikuja gari ya polisi wakiwa na diwani wa Kata ya Magomeni wakati huo Ally Kondo pamoja na Kuruthumu Ramadhani walimtolea vitu nje na kumtaka kuondoka katika nyumba hiyo bila kutoa maelezo yoyote. “ Mhe. Mkuu wa Wilaya nakupongeza sana baba kwakutujali masikini, mungu akubariki na akupe maisha marefu , hata Mahakama pia inachangia kwakuwa awali ilikuja toleo la kwanza lilionyesha 159 Block four, toleo la pili 159 Block eigth, toleo la tatu halikuwa na namba ya nyumba kwakweli huu ni uonevu” amesisitiza Bi Sharifa. Imetolewa na Kitengo cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni DC CHONGOLO ASIMAMA KIDETE NA WANAOZURUMU NYUMBA , ATOA ONYO KALI KWA WAHUSIKA, BI SHARIFA ARUDISHIWA NYUMBA YAKE Posted On: November 11t... + Read more »
MANISPAA YA KINONDONI YAZINDUA BARAZA LA WAZEE Posted On: November 8th, 2019 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni , leo imezindua Baraza la wazee ikiwa ni baada ya kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi mwezi Juni mwaka huu. Baraza hilo limezinduliwa na Katibu Tawala wa Halmashauri hiyo, Bi Stella Msofe , kwaniaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Daniel Chongolo ambapo ameshauri baraza hilo litumike vema kwa wazee kushauriana namna ya matumizi sahihi ya kadi za msamaha za bima ya afya pamoja na kupaza sauti juu ya changamoto wanazokumbana nazo. Bi Msofe ameongeza kuwa wazee ni hazina inayotakiwa kutunzwa ipasavyo kwakuwa ni chachu ya maendeleo ya nchi jambo ambalo hata serikali ya awamu ya tano imekuwa mstari wa mbele kujali afya zao. Amefafanua kuwa serikali ya awamu ya tano, inawajali wazee na makundi yote ya kila rika, na kwamba kuna haja ya kutoa elimu kuhusu matumizi ya kadi ya afya kwa wazee na hivyo kutoa jukumu hilo kwa wajumbe wa baraza hilo. Viongozi wa baraza hilo waliochaguliwa Juni mwaka huu ni Wallace Mwakikalo kutoka Kata ya Kigogo ambaye ni mwenyekiti, Hapendeki Mshambya Makamu mwenyekiti kutoka Kata ya Kunduchi, Richard Kisika Katibu kutoka Kata ya Mbezi juu. Wengine ni Maua Mtiga ambaye ni Katibu msaidizi kutoka Kata ya Makumbusho, Jaha Kimvuli mtunza hazina kutoka Kata ya Ndugumbi, Mary Kallinga mjumbe kutoka Kata ya Mzimuni na Khalid Mntambo mjumbe kutoka Kata ya Magomeni. Katika hatua nyingine Bi Msofe ameipongeza idara ya afya kwa kazi kubwa walioifanya ya kuendesha zoezi la utoaji chanjo ya surua pamoja na Polio na kusema kuwa huduma hiyo imewafikia wananchi kwa asilimia kubwa. Imetolewa na kitengo cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. MANISPAA YA KINONDONI YAZINDUA BARAZA LA WAZEE Posted On: November 8th, 2019 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni , leo imezindua Baraz... + Read more »
DC CHONGOLO ATEKELEZA AGIZO LA RAIS MAGUFULI LA KUSIMAMIA KURUDISHWA KWA NYUMBA YA BIBI MWENYE MIAKA ZAIDI YA 80 Posted On: November 7th, 2019 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo ametekeleza agizo la Rais Dk. John Pombe Magufuli la kusimamia kurudishwa kwa nyumba ya Bi Amina Muhenga mwenye miaka zaidi ya 80 aliyozurumiwa kwa kipindi cha miaka zaidi ya 30 iliyopita. Rais Dk. Magufuli alitoa agizo hilo zaidi ya miezi miwili iliyopita alipokuwa kwenye ibada ya jumapili katika kanisa la mtakatifu Petro ambapo Bi Amina alimfuata na kumueleza malalamiko yake kuhusiana na nyumba yake kuchukuliwa na mtu mwingine kinyume cha taratibu na hivyo kumsababishia kukosa makazi maalumu ya kuishi. Mhe. Chongolo alieleza kuwa baada ya Rais kutoa maagizo hayo, kwakuwa ni waisaidizi wake ,walilifanyia kazi na hivyo kufanikisha kumrudishia Bi Amina nyumba yake pamoja na hati huku utaratibu mwingine ukiendelea kufanyika. “Baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa Bibi, Mhe rais kwakuwa sisi ni wasaidizi wake, alituagiza kulifanyia kazi na leo hii tumehitimisha kwa kumkabidhi hati za umiliki wa nyumba yake, na mambo mengine tunaendelea kuyakamilisha, kuanzia sasa bibi anarudi kwenye nyumba yake.” Amessema Mhe. Chongolo. Aidha Mhe. Chongolo ameonyesha masikitiko yake ya baadhi ya wananchi wanaoishi katika Wilaya ya Kinondoni kuishi kwa ujanja ujanja na kusema kuwa kunaidadi kubwa ya watu wanaoishi kwenye mfumo huo na hivyo kutoa onyo la kuwataka kuacha mara moja tabia hiyo. Amesema imekuwa ni jambo la kawaida kwa wananchi hao kwani kila siku ofisi yake imekuwa ikipokea malalamiko yanayohusiana na kuzurumiwa kwa nyumba zao kwakutumia kigezo cha hukumu ya Mahakama na hivyo kuacha watu wakiteseka. Ameongeza kuwa,wakitoka Mahakamani wanakuja kuwatoa watu wenye haki, sijui niseme nini ila ukiangalia kunahali ya rushwa, ambayo imekuwa ikiwatesa sana baadhi ya wananchi, kazi yetu sisi ni kusimamia haki,nitahakikisha haki inasimamiwa na inatolewa kwa mwenye haki” amesema Mhe. Chongolo. Kwa upande wake Bi Amina amemshukuru rais Magufuli kwa kumsaidia kupata nyumba yake, na hivyo kusema kuwa anamuombea kwa mungu aendelee kuwatumikia wanyonge. Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. DC CHONGOLO ATEKELEZA AGIZO LA RAIS MAGUFULI LA KUSIMAMIA KURUDISHWA KWA NYUMBA YA BIBI MWENYE MIAKA ZAIDI YA 80 Posted On: November 7th,... + Read more »