KINONDONI YA TUMIA BIL. 1.5 UJENZI WA MADARASA YA SHULE ZA MSINGI Posted On: February 4th, 2020 WALIMU WASEMA MKURUGENZI KAGURUMJULI ANATEKELEZA IPASAVYO SERA YA ELIMU BILA MALIPO. Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imetumia kiasi cha shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi na ukaratabati wa vyumba 107 vya madarasa pamoja na matundu ya choo 157 kwa wanafunzi wa shule za msingi zilizopo katika Halmashauri hiyo. Hayo yamebainisha na Afisa elimu msingi wa Halmashauri hiyo Kiduma Mageni wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya shule iliyokuwa na lengo la kuona maendeleo ya miradi hiyo ambayo inatekelezwa kwa kutumia Force Account. Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa ziara hiyo, Ndugu Mageni amesema kuwa katika fedha hizo zilizotumika kujenga na kukarabati vyumba hivyo vya madarasa pamoja na matundu ya choo, shilingi milioni 771, 520,000 zinatokana na makusanyo ya ndani, shilingi milioni 455,140,000 ni pesa kutoka serikali kuu kupitia mpango wa EP4R. Aidha Mageni ameongeza kuwa katika fedha hizo pia kiasi cha shilingi milioni 210, 004, 726 ni pesa kutoka mpango wa madarasa 100 ya Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Daniel Chongolo, na kiasi cha shilingi milioni 4, 140,000 nipesa zinazotokana na nguvu za wananchi. Sambamba na hivyo, ndugu Mageni amebainisha madarasa yaliyojengwa ni 58, yaliyokarabatiwa ni 42 na kwamba kwa vyumba vilivyokarabatiwa vimeanza kutumika na wanafunzi huku vile vinavyojengwa vikiwa vimekamilika kwa asilimia 95. Mageni amesema Halmashauri ya Kinondoni kupitia Mkurugenzi Aron Kagurumjuli pamoja na Mkuu wa Wilaya Mhe. Daniel Chongolo wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa inajenga na kukarabati madarasa hayo ili wanafunzi waweze kusoma katika mazingira mazuri. Ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya tano inayo ongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli inatoa elimu bure na kwamba viongozi hao Mkurugenzi Kagurumjuli na Mkuuwa Wilaya Chongolo wanaitekeleza kikamilifu sera hiyo. “ Niwapongeze sana kwa kazi nzuri wanayoifanya, tumejionea wenyewe wanafunzi wanakaa kwenye majengo mazuri,ya kisasa ,mengine bado yapo kwenye hatua ya mwisho kukamilika na muda sio mrefu yatakabidhiwa ili watoto wetu wa anze kuyatumia. “Nampongeza sana Mhe. Chongolo, Kagurumjuli na timu yake yote wanafanya kazi kubwa, inaonekana, Rais wetu Dk. Magufuli ametoa elimu bure na sisi tunaitekeleza, nasio kwamba tunaishia hapa, bado tutaendelea kutekeleza zaidi na zaidi ili watoto wetu wasome kwenye majengo safi” amesema Mageni. Mageni amesema ameridhishwa na ujenzi, ukarabati wa majengo hayo na hivyo kuwataka walimu hao kuwa wasimamizi wazuri wa miundombinu hiyo. Kwa upande wa mwalimu hao waliokuwa katika ziara hiyo wamempongeza Mkurugenzi Kagurumli kwa kuwezesha ujenzi wa madarasa hayo na kwamba wanafunzi watasoma kwa nafasi. Mmoja wa walimu hao ambaye ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mwenge, Janeth Mlenge alisema kuwa elimu bure inayotolewa na Rais Dk.Magufuli imetoa hamasa kwa wazazi na hivyo kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi wanaosoma. Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Nyakasanga amesema kuwa kupitia mradi huo katika shule yake amejengewa vyumba nane vya madarasa ofisi ya mwalimu mkuu pamoja na matundu 13 ya choo na hivyo kumpongeza Mkurugenzi Kagurumjuli,Mhe. Chongolo kwa kuwapatia majengo hayo. Hata hivyo walimu hao wameonyesha kufurahishwa na huduma hiyo ya kujengewa madarasa katika shule zao, sambamba na kukarabatiwa na kusema serikali kupitia Halmashauri ya Kinondoni inatekeleza vema sera ya Elimu bila malipo. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YA TUMIA BIL. 1.5 UJENZI WA MADARASA YA SHULE ZA MSINGI Posted On: February 4th, 2020 WALIMU WASEMA MKURUGENZI KAGURUMJULI AN... + Read more »
DC CHONGOLO ASITISHA VIBALI VYA UCHIMBAJI MCHANGA MABONDENI Posted On: February 4th, 2020 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo amesitisha vibali vya uchimbaji mchanga vilivyotolewa na Bodi ya Maji Bonde la Ruvu kutokana na kuleta madhara ya uharibifu wa mito na kusababisha athari kwenye makazi ya watu katika Halmashauri hiyo. Vibali vilivyositishwa katika ni vile vilivyotolewa kufanya shughuli hizo katika Bonde la mto Salasala, Mto mbezi, Ndumbwi, Nyakasangwe, na kusema kuwa mito hiyo inapita katikati ya makazi ya watu na kwamba baada ya kufanyika marekebisho utawekwa utaratibu upya wa kufanya shughuli hizo. Akizungumza mara baada ya kufanya ziara katika Bonde la mto Salasala (Mto Tegeta) Mhe. Chongolo amesema kuwa amefikia uamuzi huo baada ya wakandarasi waliopewa vibali hivyo kuharibu mto huo na hivyo kuamuru kupandwa kwa Miti hiyo ambayo itasaidia kuzuia mmomonyoko wa udongo. Amesema kuwa kinachofanyika hivi sasa ni kurekebisha mito hiyo kwa kupanda miti, magugu pamoja na mianzi inayoshika ardhi ili kuzuia mmomonyoko wa undongo na hivyo kuweka mkakati wa kuratibu shughuli za utoaji mchanga kufanyika katika maeneo hayo. Mhe. Chongolo amesena kuwa katika Halmashauri hiyo ameruhusu kibali hicho kutolewa katika bonde la Mpigi kwa maelekezo ya kuhakikisha kuwa shughuli hizo zifanyike kwa ajili ya kusafisha mto ili kuondosha adhari kwani mchanga ukijaa sana husababisha maji kusambaa nje. “ Wakati tunafanya haya ni lazima tusitishe shughuli zote zinazofanyika hapa, tulifanya tathimini ya kuangalia athari kwa kuunda timu ambayo ilikamilisha majukumu yake na kuleta ripoti hiyo Disemba mwaka jana, mwezi wa kwanza mwaka huu tulianza mjadala na wale ambao walipewa kandarasi ya kutoa mchanga kwenye mito hii” amesema Mhe. Chongolo Nakuongeza kuwa “ baada ya majadiliano hayo, tulikubaliana nao kupanda Miazi, Miti na Magugu, na watu ambao mnawaona hapa asilimia 90 niliagiza kila mwenye kibali cha bonde anayekuja aje na watu 10 kwa ajili ya kushirikiana kupanda miti, na hii miti inayopandwa hapa sijanunua wameleta wao” ameongeza Mhe. Chongolo. Mhe. Chongolo amesisitiza kuwa “ kwanza mchanga usiondolewe kibiashara ,tutoe mchanga sehemu ambayo tunaona kuwa kunaongezeko ambalo linaweza kusababisha athari, ili turuhusu maji yapite bila kuleta madhara kwa wananchi waliopo pembezoni mwa mto na huyo anayetoa ahakikishe anafanya marekebisho ikiwemo kupanda miti, magugu na mianzi. Katika hatua nyingine Mhe. Chongolo amesema kuwa " Tunachangamoto ya watu kufanya shughuli za kibinadamu kwenye maeneo ya maji, Serikali imeshaelekeza watu ambao wapo kwenye maeneo haya wanatakiwa kuwa umbali wa mita 60 kwa 60 , lakini hatufuati hiyo Sheria ya mazingira. Wananchi mliopo katika maeneo haya, niwasihi sana acheni kufanya shughuli hapa, leo tunapanda miti ili kunusuru bonde hili lisiendelee kukua, mchanga utatolewa kwa kibali kwa ajili ya kusafisha mto ila sio kuchimba mchanga kwa shughuli ya kibiashara ama nyingine, " amesema Mhe. Chongolo. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni DC CHONGOLO ASITISHA VIBALI VYA UCHIMBAJI MCHANGA MABONDENI Posted On: February 4th, 2020 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chong... + Read more »