CHONGOLO AAGIZA KUCHUKULIWA HATUA WATAKAOCHIMBA MCHANGA KWENYE MITO. Posted On: April 8th, 2020 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo ameliagiza Jeshi la Polisi Wilayani hapo kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika kuingia kwenye mito na kuchimba mchanga katika bonde la mto Salasala, bonde la mto Mbezi na bonde la mto Tegemeta. Mhe. Chongolo ametoa agizo hilo leo wakati alipofanya ziara na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na kushuhudia vitendo hivyo vikiendelea ikiwa ni takribani miezi miwili imepita tangu kuendesha zoezi la upandaji miti ya mianzi na magugu pamoja na kusitishwa kwa vibali vya uchimbaji wa mchanga vilivyotolewa na Bodi ya Maji Bonde la Ruvu. Amesema kuwa licha ya kutoa maelekezo pamoja na kusitishwa kwa vibali hivyo lakini bado wananchi wanaendelea kuchimba mchanga jambo ambalo amesema linahatarisha nyumba za makazi ya watu na hivyo kulisisitizia jeshi hilo kuwachukulia hatua wananchi hao ambao wanajihusisha na shuguli hizo. “Tulishazuia hii mito isichimbwe mchanga, tumepita mto Salasala, Mbezi kule kwenye daraja la Malechela, pamoja na huku juu mpakani mwa eneo la jeshi la Lugalo, bado vitendo hivi vinaendelea nasisitiza naninaagiza jeshi la polisi kwenye Wilaya ya Mabwepande na Kawe ambayo ndio inahusika, niliagiza na leo narudia kwa mara ya pili hatutakuwa na msamaha kwenye jambo hili. Amefafanua kuwa “mtu yeyote ambaye ataonekana analea vitendo vya uharibifu huu wa mazingira, tukimkuta na kumkamata tutamchukulia hatua kali za kisheria kwasababu jukumu letu sisi viongozi ni kusimamia na kuilinda sheria. Mhe. Chongolo amesisitiza kuwa“ Hatuko hapa kuwaonea watu, wala kuwaacha wananchi waharibikiwe na nyumba zao kwasababu ya maslahi na uroho wa watu wachache, kufanya hivi ni kuhujumu maslahi ya nchi hatuwezi kuendelea kuwaacha watu wanamna hii kwa hiyo nilazima tuchukue hatua kwa kila tutakaye mbaini anafanya shughuli hii. Aidha Mhe. Chongolo amesema kuwa baada ya ziara hiyo ataunda timu ya kufuatilia mwenendo wa watu hao kwa kuwa alishatoa maagizo ya kuwashugulikia wote wanaohusika na kufanya shuguli za kuchimba mchanga kwenye mito hiyo. Mapema mwaka huu, Mhe. Chongolo alisitisha vibali vya uchimbaji mchanga vilivyotolewa na Bodi ya Maji Bonde la Ruvu kutokana na kuleta madhara ya uharibifu wa mito na kusababisha athari kwenye makazi ya watu katika Halmashauri hiyo. Vibali vilivyositishwa ni vile vilivyotolewa kufanya shughuli hizo katika Bonde la mto Salasala, Mto mbezi, Ndumbwi, Nyakasangwe, na kusema kuwa mito hiyo inapita katikati ya makazi ya watu na kwamba baada ya kufanyika marekebisho utawekwa utaratibu upya wa kufanya shughuli hizo. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na uhusiano Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. CHONGOLO AAGIZA KUCHUKULIWA HATUA WATAKAOCHIMBA MCHANGA KWENYE MITO. Posted On: April 8th, 2020 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel... + Read more »
DC CHONGOLO APOKEA VIFAA VYA KUJIKINGA NA CORONA KUTOKA KAMPUNI YA SPORT PESA Posted On: March 30th, 2020 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imepokea vifaa vya kunawia mikono (zaidi ya ndoo 100) pamoja na Vitakasa mikono kutoka mtandao wa kubashiri wa SportPesa kwa lengo la kuwasaidia wananchi kujikinga na maambukizi ya homa ya mapafu inayosababishwa na Virusi vya COVID 19 (Corona). Vifaa hivyo vya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona vimepokelewa na Mkuu wa Wilaa hiyo Mhe. Daniel Chongolo ,akiwa ameambatana na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Dk. Patricia Henjewele, Mganga Mkuu Samweli Laizre pamoja na Katibu Tawala Bi Stella Msofe. Akizungumza wakati wakupokea vifaa hivyo, Mhe. Chongolo amesema kuwa Kinondoni imepokea vifaa hivvyo na kwamba wataendelea kuhamasisha wadau wengine waweze kuchangia ili kuendelea kudhibiti ugonjwa huo usisambae kwenye maeneo mengine. Amefafanua kuwa Virusi vya Corona vimekuwa janga kubwa Duniani na kwamba Wilaya hiyo imejipanga kuhakikisha kuwa kila mmoja anatumia vitakasa hivyo ili kujikinga na maambukizi ya Virusi hivyo pasipo kuambukiza wengine. “Kama mkuu wa Wilaya ninashukuru kwa msaada huu, kwetu utasaidia kwa sababu ofisi zote za Serikali za mitaa na Kata zitapata seti za vifaa hivi, tutakuwa huru kwa kuendelea kutoa huduma kwa wananchi kama kawaida, ndio mana mmeona hapa kila anaeingia ana nawamikono yake kabla ya kuingia kupatiwa huduma” amesema Mhe. Chongolo. Mhe. Chongolo ameongeza” kwetu sisi hatupambani kama Kinondoni, tunapambana kama mkoa ,nandio jukumu tulilopewa , hivyo hivyo nitumie fursa hii kuwaalika wadau wengine wenye mapenzi mema kutupatia vifaa vingine. Mhe. Chongolo ameeleza kuwa Wilaya hiyo imejipanga vizuri katika kupambana na virusi vya Corona ikiwemo kuendelea kutoa matangazo ya kuhamasisha na kuelimisha wananchi namna ya kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo. Kwaupande wake Mkurugenzi wa uendeshaji kampuni ya SportPesa nchini, Abbas Tarimba, amesema kuwa ndoo hizo zakunawia mikono zitasaidia wananchi ikiwa ni hatua ya kujikinga na virusi hivyo vya homa ya mapafu inayosababishwa na Covid 19. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. DC CHONGOLO APOKEA VIFAA VYA KUJIKINGA NA CORONA KUTOKA KAMPUNI YA SPORT PESA Posted On: March 30th, 2020 Halmashauri ya Manispaa ya Ki... + Read more »
DC CHONGOLO AAGIZA WATA ALAMU WA AFYA KUTOA ELIMU YA KUJIKINGA NA CORONA KWA WANANCHI Posted On: March 19th, 2020 NI KATIKA VITUO VYA DALADALA, NYUMBA ZAIBADA Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo, amewaagiza wata alaamu wa Afya Wilayani hapo kuanza mara moja kutoa elimu ya kujikinga na virusi vya Corona kwenye nyumba za Ibada ikiwemo Makanisani na Misikitini. Aidha Mhe. Chongolo ameagiza pia elimu hiyo kutolewa kwenye vituo vya daladala ili kuwasaidia wananchi kutambua namna ya kutumia na kujikinga na Virusi hivyo. Mhe. Chongolo ametoa agizo hilo leo katika kikao cha zarura kilichofanyika katika ukumbi wa Afya ambapo kimehusisha Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Idara ya Afya, watendaji pamoja na viongozi wa Dini . Amesema kuwa lengo la kikao hicho cha zarura ilikuwa ni kujadili namna na hatua zitakazo chukuliwa katika kudhibiti virusi hivyo ili visiweze kusambaa pamoja na kutoa elimu ya kutosha kwa watumishi sambamba wananchi katika Wilaya hiyo. Amesema kutokana na kuingia kwa Virusi hivyo vya Corona katika jiji la Dar es Salaam, wataalamu hao wa Afya wa Wilaya hiyo wanapaswa kutoa elimu madhubuti kwenye maeneo ambayo ni lazima wananchi kuyatumia kama vile Vituo vya daladala ikiwemo vya mwendokasi, nyumba zaibada kuhusu namna ya kujikinga na virusi hivyo. Amefafanua kuwa katika elimu hiyo pia itajikita katika kuelimisha wananchi namna ya kutumia vifaa vya kujikinga na maambukizi hayo kama vile vifaa vya kusafishia mikono, Gloves na Barakoa (Mask ) za kufunika pua na mdomo. “ Hili jambo tunapaswa kulichukulia kwa tahadhari kubwa, muwaelimishe wananchi kuhusu namna ya kujikinga na Virusi hivyo, pamoja na kutumia hivyo vifaa ,mnapopita kwenye hayo maeneo hakikisheni kwamba mnawaelimisha vizuri ili wajue ni wakati gani wanapaswa kuvitumia, pia kusafisha miko mara kwa mara” amesema Mhe. Chongolo. “ Lakini pia tuwasaidie wananchi kutoka kwenye presha waliyo kuwa nayo hivi sasa, tunafahamu kuwa watanzania wengi wamepata taharuki juu ya Vizuri hivi, tusipojitahidi tutajikuta tatizo la presha lina adhiri wananchi kuliko Vizuri vya Corona. Katika hatua nyingine Mhe. Chongolo amewaeleza viongozi wadini kwamba mikusanyiko isiyokuwa ya lazima haipaswi kuwepo ila kwa ambao wanataka kufunga ndoa wafungishwe lakini kwa kufuata utaratibu ambao utaepusha mikusanyiko ya watu. Awali Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo, John Kijumbe amesema kuwa hadi sasa wameshachukua tahadhari na kama vile kutoa elimu katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwa watumishi na wahudumu wa Afya pamoja na kugawa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo. Hata hivyo Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imejidhatiti kikamilifu katika kujikinga na virusi hivyo kwakuweka visafisha mikono kwenye mageti yote ya kuingia ikiwa ni katika kuhakikisha kuwa kila mwananchi anayefika kupata huduma mbalimbali wanakuwa salama. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. DC CHONGOLO AAGIZA WATA ALAMU WA AFYA KUTOA ELIMU YA KUJIKINGA NA CORONA KWA WANANCHI Posted On: March 19th, 2020 NI KATIKA VITUO VYA D... + Read more »