JAMII YA KINONDONI YATAKIWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUTUMIA MAZIWA ILI KUIMARISHA AFYA YA MWILI NA AKILI KUELEKEA UCHUMI WA KATI WA VIWANDA Posted On: May 24th, 2019 Kauli hiyo imetolewa leo na Mhe Diwani wa kata ya Kunduchi Mh. Michael Urio kwenye hafla ya uzinduzi wa wiki ya unywaji wa maziwa mashuleni inayoratibiwa na Idara ya mifugo na uvuvi kwa Manispaa ya Kinondoni na kufanyika katika Shule ya Sekondari Kondo. Amesema kuwa, serikali ya awamu ya tano inayo nia madhubuti na mwelekeo wa dhati katika kuijenga Tanzania ya Viwanda na uchumi wa Kati, hivyo inahitaji jamii ya watu wenye afya thabiti na akili ya kupambanua mambo kwa ufasaha ili waweze kuendana na sera hiyo. "Maziwa yana virutubisho vyote mhimu vinavyotakiwa katika ujenzi wa mwili na akili hivyo badala ya kunywa pombe na vinywaji vingine tunyweni maziwa kwa wingi ili kuunga juhudi za serikali pia viwanda vyetu vya ndani" ameongeza mhe Urio. Aidha Quenter Mawinda kwa niaba ya msajili wa bodi ya maziwa amewashauri wanafunzi kutumia maziwa kwa wingi ili kuimarisha afya ya akili na mwili na waweze kuendana na Kasi ya Mhe Rais maana anahitaji vijana wachapakazi walioimara. Mara baada ya uzinduzi huo , Manispaa ya Kinondoni kupitia idara ya mifugo na uvuvi imegawa maziwa katika shule tano za Sekondari ambazo ni Shule ya Sekondari Mbopo, Kondo, Mtakuja Beach, Boko na Bunju A, ambapo zaidi ya paketi 350 kwa kila shule zimegawiwa, lakini siku ya pili kwa idadi ya paketi hizo hizo itagawiwa kwa Shule tano za Msingi za Manispaa ya Kinondoni . Uzinduzi huu unatarajiwa kitaifa kufanyika Mkoani Arusha kuanzia tar 28 mwezi wa tano hadi tarehe 1 mwezi wa sita. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. JAMII YA KINONDONI YATAKIWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUTUMIA MAZIWA ILI KUIMARISHA AFYA YA MWILI NA AKILI KUELEKEA UCHUMI WA KATI WA VIWANDA ... + Read more »
KAMATI YA SIASA YA MKOA WA DAR ES SALAAM, YARIDHISHWA NA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA KATIKA WILAYA YA KINONDONI. Posted On: May 24th, 2019 Kamati hiyo Chini ya mwenyekiti wake Bi Kate Kamba imeonesha kuridhishwa na maboresho ya miundombinu ya barabara yanayofanyika maeneo ya katikati hususan Tandale, Kijitonyama na Mwananyamala Manispaa ya Kinondoni. Hali hiyo imedhihirika wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo ukiendelea katika ziara ya Kamati ya katika Manispaa ya Kinondoni, chini ya Mwenyekiti wake Bi. Kate Kamba, iliyofanyika kwa lengo la kujiridhisha na utekelezaji wa ilani unaoenda sambamba na ubora wa miradi inayotekelezwa. Bi Kate amesema kuwa wakati umefika sasa kwa Kinondoni kuelekeza nguvu katika kuboresha makazi holela wanayoishi wananchi kwani wanaamini maboresho ya miundombinu yakienda sambamba na maboresho ya makazi ndipo tija itakapopatokana. Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bw Maduhu Kazi ameishukuru Kamati hiyo kwa kutembelea Kinondoni na kuahidi kufanyia kazi ushauri na maelekezo yote yaliyotolewa na Kamati hiyo ya Siasa. Miradi iliyotembelewa katika ziara hiyo ni pamoja na miradi ya barabara, Shule za Msingi na Sekondari, zahanati pamoja na vituo vya Afya. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. KAMATI YA SIASA YA MKOA WA DAR ES SALAAM, YARIDHISHWA NA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA KATIKA WILAYA YA KINONDONI. Posted On: May... + Read more »