Top ad

Top ad

 
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ali Salum Hapi, ametoa wito kwa Waalimu wakuu wa Shule za Sekondari pamoja na waratibu wa Elimu Manispaa ya Kinondoni kujiepusha na udanganyifu wa takwimu za shule, pamoja na kuzingatia sheria, taratibu, kanuni na umakini katika kazi yao ili kuwapatia watoto wetu msingi mzuri wa Elimu, ujuzi na marifa.
Ametoa wito huo leo alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuwapongeza waalimu wakuu wa shule za Sekondari ambao shule zao zimefanya  vizuri katika mitihani ya kidato cha pili na cha nne kwa mitihani ya Taifa iliyofanyika mwaka 2015, katika ukumbi wa Shule ya sekondari oysterbay ,ambapo pia hafla hiyo  imehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mh Hamphrey Polepole.
Amesema kwa shule za Kinondoni kufaulu kutoka 54 asilimia kwa mwaka 2014 hadi kufikia 70 asilimia kwa mwaka 2015, ni kutokana na nidhamu ya kazi, umakini na uwajibikaji wa waalimu pamoja na juhudi za wanafunzi.
Amewataka waalimu wakuu wa shule pamoja na waratibu wa Elimu kutimiza wajibu wao , kuwajibika katika maukumu yao, na kuhakikisha wanajiepusha na udanganyifu wa takwimu za waalimu pamoja na wanafunzi .
Amekabidhi zawadi kwa shule zilizofanya vizuri kwa mwaka 2015, shule zilizoongoza kwa baadhi ya masomo ambayo ni Biology ,chemistry,na Kiingereza, na  kwa waalimu wa masomo hayo, pia ametoa zawadi kwa waalimu wanaohudhuria vizuri na kuwahi kazini kwa mwaka mzima pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri kwa mwaka 2015.

0 comments:

Post a Comment

 
Top