MSTAHIKI MEYA MANISPAA YA KINONDONI APOKEA UJUMBE KUTOKA HONG KONG POLYTECHNIC UNIVERSITY (HKPU) Posted On: January 25th, 2019 HALMASHAURI YA MANIPAA YA KINONDONI Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Benjamin Kawe Sitta leo amepokea ujumbe kutoka Hong Kong Polytechnic University ( HKPU) ambapo wamekutana na kufanya mazungumzo yenye lengo la kuanzisha Ushirikiano wa Kitaasisi utakaosaidia kuimarisha uwezo wa Taasisi zetu mbili za Kilimo Malolo na ufundi Wazo katika kutoa taaluma bora zaidi na hatimaye kuweza kufikia malengo ya manispaa ya Kuwawezesha Wanufaika wa Mikopo ya Wanawake na vijana kunufaika na Tekinolojia itakayotolewa katika vyuo hivyo. Ujumbe huo wa Chuo Kikuu cha HKPU Umeongozwa na Ndugu CHAN Stephen ,Mkuu wa Idara ya Mafunzo kwa njia ya kujitolea na Profesa Grace Ngai ,Mkuu wa Idara ya Komputa ambapo Mstahiki Meya wa Kinondoni Pamoja na Mambo mengine ametumia fursa hiyo kuwakaribisha Tanzania na kuwashukuru kwa nia na dhamira ya Chuo hicho kuanzisha Ushirikiano wa Kitaasisi na vyuo vya Tanzania ikiwemo Kituo cha Mafunzo Malolo na Chuo cha Ufundi Wazo kinachotarajia kufunguliwa mwezi Februari mwaka huu 2019. Akizungumza na Ujumbe huo Mstahiki meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Benjamini Kawe Sitta, amewataka Wakazi wa Manispaa ya Kinondoni hususani wanufaika wa Mikopo ya Wanawake na Vijana inayotolewa na Manispaa kujiunga kwa mafunzo mbalimbali ya ufundi katikia vituo hivyo viwili ili waweze kunufaika na ushirikiano wa Manispaa ya Kinondoni na chuo hiki Maarufu cha Hong Kong Polytechnic University. Kiongozi wa Ujumbe huo Ndugu CHAN Stephen Mkuu wa Idara ya mafunzo kwa njia ya kujitolea, katika mazungumzo yake amesema kuwa ziara yake hapa Nchini Tanzania inatokana na Fursa zilizopo za kutoa Huduma za Kijamii katika Nyanja za Kiteknolojia na ufundi kama wanavyofanya Nchini Rwanda hivyo ujio wake ni mwanzo mpya wa Mashirikiano katika nyanya hizo .Pia amewawakikishia Watanzania Kunufaika na Ushirikiano wa Kihistoria uliopo kati ya Tanzania na China. IMETOLEWA NA: KITENGO CHA HABARI, MAWASILIANO ITIFAKI NA MAHUSIANO HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI. MSTAHIKI MEYA MANISPAA YA KINONDONI APOKEA UJUMBE KUTOKA HONG KONG POLYTECHNIC UNIVERSITY (HKPU) Posted On: January 25th, 2019 HALM... + Read more »
WAKULIMA KINONDONI WAMETAKIWA KUELEWA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIA NCHI KATIKA SEKTA YA KILIMO ILI WAWEZE KUKABILIANA NAZO Posted On: January 18th, 2019 Rai hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bi.Stella Msofe, alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tatu yaliyoendeshwa katika kituo cha kilimo malolo kwa lengo la kutoa elimu mahususi juu ya mabadiliko ya tabia nchi katika sekta ya kilimo na jinsi ya kukabiliana nayo. Amesema ni lazima wakulima hawa wapatiwe elimu ya kutosha itakayowawezesha kuepukana na athari hizo, kwani kilimo ndio uti wa Mgongo wa Taifa letu, hasa ikizingatiwa tunahitaji malighafi za kutosha kuendeshea viwanda vyetu, ambayo kwa sasa ndio sera ya Serikali ya awamu ya tano, Serikali ya viwanda. Amesema "Bahati nzuri Kinondoni tunayohazina ya wataalam wa sekta hii, tunacho kituo bora kabisa kwa ajili ya elimu hiyo, kwanini tushindwe kutoa elimu kwa walengwa?, kwanini wakulima wetu wasipate elimu, wataalam hawa wapo, na wanalipwa kwa kazi hiyo, hivyo watumieni, kwani jukumu lao ni kurudisha ujuzi, elimu na maarifa kwa jamii husika." Bi.Msofe. Awali akiainisha lengo zima la mafunzo hayo kwa Katibu Tawala huyo, Mkuu wa Idara ya kilimo na mifugo Manispaa ya Kinondoni, ambaye pia ni msimamizi wa kituo cha kilimo Malolo, Bw Salehe Hija amesema, mafunzo haya yaliyohusisha wakulima 40, kutoka Kata tano za Manispaa hiyo, yamelenga si tu kutoa uelewa, bali pia kuainisha njia sahihi za kupambana na changamoto zake, ili wakulima waweze kufanya kilimo chenye tija. Amezitaja Kata zilizoshiriki mafunzo hayo kuwa ni kata ya Mbweni, Bunju, Mabwepande, Wazo na Kunduchi, na kuwataka wakulima hao kuwa mabalozi kwa wakulima wengine kwa elimu waliyoipata, ili elimu ienee na kuweza kuleta tija. Akishukuru uongozi wa Manispaa ya kinondoni kwa kuendesha mafunzo hayo, kwa niaba ya wakufunzi wengine, Mwenyekiti wa wakulima waliopatiwa mafunzo hayo Bw John Malekela amesema elimu hii ni hazina tosha kwa sekta nzima kwa Wilaya yetu, kwani tunaahidi kuitendea kazi ili waweze kuepukana na changamoto hizo za mabadiliko ya tabia nchi na waweze pia kujiongezea thamani ya mazao yao. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. WAKULIMA KINONDONI WAMETAKIWA KUELEWA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIA NCHI KATIKA SEKTA YA KILIMO ILI WAWEZE KUKABILIANA NAZO Posted On: Ja... + Read more »