Top ad

Top ad

 

MAFUNZO YA SIKU TATU YATOLEWA KWA WAJUMBE WA KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI KINONDONI

Posted On: May 29th, 2021

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo shirikishi, Mwenyekiti wa Kamati ya kudhibiti UKIMWI Kinondoni ambaye pia ni Naibu Meya wa Manispaa hiyo Mhe.Herri Misinga amesema  mafunzo haya ni kwa lengo la kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati hiyo ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Amesema lengo pia ni kuwaandaa wajumbe kuwa mabalozi wazuri na ndio maana Serikali kupitia mpango wakuthibiti maambukizi ya virusi vya Ukimwi imekuwa ikisisitiza  utoaji wa elimu kwa wananchi.

“ Nimeambiwa mafunzo haya ni ya siku tatu, ninaamini kuwa wawezeshaji ambao wamekuja leo hii, watatoa elimu nzuri ambayo kwetu sisi itatusaidia kwenda kuwaelimisha wananchi ambao tumewawakilisha hapa, nimpongeze Mkurugenzi kwakutuandalia mafunzo haya” amesema Mhe. Misinga.

Awali akimkaribisha Naibu Meya, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Bi Sipora Liana amesema kuwa anatambua umuhimu wa Kamati hiyo na kwamba anaamini elimu  ya siku tatu  itakayotolewa kupitia mafunzo hayo itakuwa chachu ya mafanikio katika kuhakikisha maambukizi ya virusi vya Ukimwi yanaendelea kupungua katika Manispaa hiyo hasa ikizingatiwa kwamba kunajumla ya vituo vya kupimia maambukizi ya VVU 240, ambapo kati ya hivyo vya Serikali ni 27 na vya binafsi ni 213.

Kwaupande wake mratibu wa kudhibiti UKIMWI Manispaa ya Kinondoni Bi.Robby Gwesso amesema mafunzo hayo, yamehusisha warataibu kutoka TACAIDS, Manispaa ya Kinondoni, wataalamu kutoka Taasisi binafsi, Madiwani, wawakilishi kutoka makundi ya Vijana, Wazee, Asasi za kiraia, Viongozi wa dini,Watu wenye ulemavu, Watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya ukimwi pamoja na watendaji wa Manispaa ya Kinondoni.

 Mada zilizofundishwa ni pamoja na UKIMWI mahala pa Kazi, Sera ya taiga ya kudhibiti UKIMWI Tafsiri ya sheria ya kudhibiti UKIMWI, Sera na miongozo inayosimamia ithibiti wa VVU na UKIMWI Katika Jamii, Muundo wa kamati ya kudhibiti UKIMWI ngazi ya wilaya, kata na mtaa/ vijiji, Wajibu na majukumu ya kamati shirikishi za kudhibiti UKIMWI ngazi ya wilaya, kata na mitaa/vijiji.

Nyingine ni Ukweli Kuhusu UKIMWI, kifua kikuu na Homa ya ini, Mawasiliano Kuhusu UKIMWI, utoaji wa taarifa za VVU na UKIMWI, Mpango shirikishi, ufuatiliaji na tathmini pamoja na Uongozi na ubia Katika mwitikio wa VVU na UKIMWI

Imeandaliwa na

Kitengo cha Habari na Mahusiano

Manispaa ya Kinondoni.

0 comments:

Post a Comment

 
Top