Top ad

Top ad

 

KINONDONI YAHAMASISHA USAFI WA FUKWE KUELEKEA KILELE CHA MAADHIMISHO YA MAZINGIRA

Posted On: May 29th, 2021

 Kuelekea kilele hicho chenye kauli mbiu isemayo "Tutumie nishati mbadala kuongoa mfumo ikolojia" kinachotarajiwa kufanyika Juni  5 mwaka huu, Manispaa ya Kinondoni imeadhimsha kwa kufanya  usafi Katika fukwe ya Jangwani Beach iliyopo Kata ya Kunduchi.

Zoezi hilo la usafi lililoratibiwa na Diwani wa Viti maalum Mhe Jackline Kweka limefanyika wakati ambapo Kinondoni imeweka mpango mkakati wa kuhakikisha fukwe zinalindwa kwa maslahi mapana ya wananchi  kwa kuhakikisha ufukuaji wa taka zilizojifukia katika eneo la fukwe unafanyika ikiwa ni pamoja na kuzisafirisha kwenda dampo.

Amesema Kinondoni imejikita katika kuhakikisha suala la usafi wa Mazingira ni jukumu la kila mwananchi na kwamba kauli mbiu ya mwaka huu ikawe sehemu ya chachu katika kuhakikisha inatekelezeka.

Nae Mkuu wa Idara ya Usafishaji na Mazingira Ndg Shedrack Maximilian amewasihi wananchi wanaoishi maeneo ya fukwe kujijengea utaratibu wa kusafisha maeneo hayo na kuahidi ushirikiano kutoka  Manispaa  wa utoaji wa vifaa na magari ya kuzolea taka pale ambapo eneo husika litahitaji.

Maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani yanatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja ambapo viongozi mbalimbali wa vyama na Serikali wanatarajiwa kuhudhuria.

Imeandaliwa na

Kitengo cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni.

0 comments:

Post a Comment

 
Top