KINONDONI YAUNDA BARAZA LA WAZEE LA WILAYA Posted On: June 21st, 2019 Baraza hilo lenye wajumbe saba akiwemo Mwenyekiti na msaidizi, Katibu na Msaidizi wake, mtunza fedha na wawakilishi wawili, limeundwa kwa uchaguzi uliofanyika kwa wazee wawakilishi kutoka kata 20, za Manispaa hiyo kupiga kura katika kikao kilichofanyika katika moja ya kumbi za Kanisa katoliki Manzese. Akiongoza zoezi hilo, kwa niaba ya Maganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Bi Nusura Kessy amesema, wazee ni hazina ya Taifa, hivyo yapaswa kupaza sauti juu ya maswala yanayowahusu na kuwasemea haki zao za Msingi pale inapobidi ili waweze kutatuliwa. "Wazee ni hazina ya Taifa, nilazima walindwe, waheshimiwe watunzwe, na mashauri yao yasikilizwe, hivyo kwa baraza hili la wazee wa Wilaya mtakaloliunda kwa kufanya uchaguzi huru na wa haki unaozingatia vigezo leo, mtakuwa mmejitendea haki lakini pia baraza hilo likawe kisemeo katika yale yanayowapasa kusema " Bi. Nusura Kessy. Awali akitaja majukumu ya baraza hilo la wazee la Wilaya, Bi. Judith Kimaro ambaye pia ni mkuu wa Kitengo cha ustawi wa jamii amesema Baraza linalo majukumu yake ya msingi ambayo ni kupitia majumuisho ya kero za wazee zilizoletwa na wawakilishi, kufanya mkutano wa baraza la wazee la Wilaya kila baada ya miezi mitatu, kuwasilisha kero za wazee kwenye baraza la madiwani, kuchagua wawakilishi wawili kwenye baraza la madiwani, kushawishi Halmashauri kutenga bajeti kwa ajili ya miradi ya uzalishaji ya wazee pamoja na kuratibu mabaraza ya wazee ya Kata. Naye mratibu wa wazee Manispaa ya Kinondoni Bi Neema Mwalubilo alipokuwa akitoa taarifa ya hali ya wazee Manispaa ya Kinondoni amesema ni ya kiridhisha kwani wameweza kuunganishwa kwenye huduma za afya kwa kutengenezewa vitambulisho takribani 11,340 vya msamaha . Aidha ameainisha mikakati iliyopo ya kuinua hali ya wazee katika Manispaa hiyo kuwa ni kuhakikisha wote wanapata kadi za matibabu, kuwaongezea na kuwajengea uwezo wa kujikwamua kiuchumi pamoja na kuwaunganisha na wadau mbalimbali kwa ajili ya misaada. Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Uhusiano. Manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YAUNDA BARAZA LA WAZEE LA WILAYA Posted On: June 21st, 2019 Baraza hilo lenye wajumbe saba akiwemo Mwenyekiti na msaidizi, K... + Read more »
TAMISEMI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA DMDP NA TARURA KINONDONI. Posted On: June 21st, 2019 Hayo yamethibitika leo wakati Waziri wa TAMISEMI Mhe. Suleiman Jafo alipofanya ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo kwa lengo la kujiridhisha na ubora wake ikiwa ni pamoja na kuangalia hatua za utekelezaji zilizofikwa. Amesema utekelezaji wa miradi hii kwa mkoa wa Dar es salaam ni ya muhimu sana kwani itatatua kero kubwa walizokuwa wakizipata wananchi hasa yale maeneo waliyokuwa wakisumbuliwa na mafuriko na zile zilizokuwa na uharibifu mkubwa. "Miradi hii ni muhimu sana kwani inaenda kubadilisha sura ya Dar es salaam, tunachotaka kama Serikali ni kuhakikisha kero kwa wananchi zinaondolewa na hata wale walioko masomoni wakirudi, tuwashike mikono, taswira ibadilike "Amesisitiza Jafo. Naye Mratibu wa DMDP Manispaa ya Kinondoni Ndg. Mkelewe Tungaraza alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya DMDP amesema dhamira yao kubwa ni kuhakikisha wanaisimamia na kuitekeleza kwa kiwango kinachotakiwa ili ilete tija kwa wananchi husika. Katika hatua nyingine, Waziri Jafo amewataka wananchi kuhakikisha wanazitunza na kuzifanyia usafi barabara hizo, ikiwa ni pamoja na kuepuka kutupa taka kwenye mitaro kwani kwa kufanya hivyo kutaathiri ubora na Mazingira kwa ujumla. Kadhalika amewataka wakandarasi kuhakikisha wanakamilisha suala la uwekaji wa alama za barabara hizo,, ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa weledi, kwa kuzingatia vigezo na viwango vya ubora ili miundombinu hiyo iweze kudumu kwa muda mrefu huku ikiendelea kusaidia wananchi. Katika ziara hiyo aliyotembelea barabara ya Mbezi Makonde, Kilongawima, akachube na makanya pia imehudhuriwa na wakuu wa wilaya ya Ubungo na Kinondoni, wakurugenzi, wakandarasi pamoja na waratibu wa TARURA na DMDP. Imeandaliwa na Kitengo cha Uhusiano na Habari. Manispaa ya Kinondoni. TAMISEMI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA DMDP NA TARURA KINONDONI. Posted On: June 21st, 2019 Hayo yamethibitika leo wakati Waz... + Read more »