DC CHONGOLO AWAWEKA NDANI WAKANDARASI WA KAMPUNI YA CRJE KWA KUSHINDWA KUKAMILISHA MRADI WA KUCHAKATA TAKA KWA WAKATI Posted On: November 19th, 2019 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni , Mhe. Daniel Chongolo amewashikilia wakandarasi wawili wenye asili ya china wa Kampuni ya CRJE kwa kushindwa kukamilisha mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata taka kilichopo Mabwepande. Mhe. Chongolo amefikia uamuzi huo leo mara baada ya kampuni hiyo kushindwa kukamilisha mradi huo kwa wakati huku Mhandisi mshauri wa Manispaa Emanuel Tilya akisisitiza kuwa wamekuwa hawatoi ushirikiano wowote licha ya kwamba yupo kwenye eneo la mradi. Akizungumza wakati wa ziara aliyoifanya leo ya kukagua miradi inayojengwa na Halmashauri hiyo, Mhe. Chongolo amefafanua kuwa kwa muda mrefu amekuwa akizungumza na mkandarasi huyo kuhusu kukamilisha mradi huo kwa muda uliopangwa lakini hawakufanya hivyo . Ameeleza kuwa halmashauri inahitaji kiwanda hicho haraka ili kiweze kutumiwa na wananchi ambao ndio wanufaika wa mradi huo lakini mkandarasi aliyepewa kazi hiyo anawarudisha nyuma. Ameeleza kuwa halmashauri imeshawalipa fedha kwa ajili ya ujenzi huo lakini kinachofanyika ni fedha hizo kuzipeleka kwenye miradi yao mingine jambo ambalo limefanya hadi sasa kusuasua kwa mradi. “ Nimekuja hapa zaidi ya mara tatu, mara ya kwanza nilikuja nikaongea nao wakaniahidi watakamilisha kwa muda uliopangwa, mara ya pili nilikuja hapa nikafoka hadi nikakasirika lakini hali imeendelea hivi hivi, sasa sijawakamata nimewashikilia hadi pale watakapoleta mpango kazi wao uliojitosheleza.“ amesema Mhe. DC. ”Hatuwezi kukaa na watu wa namna hii, tumetoa pesa nyingi, kwa ajili ya kukamilisha mradi huu mapema halafu wanatuchezea, ,kama wakileta leo, kesho nitawaachia, kadiri watakavyowahi kuniletea huo mpango kazi wao ndio na mimi nitawaachia, Askari kamata hao waweke ndani. Mhe. Chongolo alisisitiza kuwa hajaridhishwa na mwenendo wa ujenzi wa kiwanda hicho na kuagiza wasiachiwe hadi atakapotoa agizo ikiwa ni baada ya kutekeleza walichoambiwa. Awali Mhandisi mshauri wa Manispaa, mhandisi Tilya ,amesema kuwa walikubaliana kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha ujenzi huo kwa wakati lakini kilichotokea ni tofauti huku mafundi wanne tu ndio waliokuwa wanafika eneo hilo la mradi. Alifafanua kuwa “ wakati mwingine huwa tunagombana wenyewe kwa wenyewe, kama angekuwa na uwezo wakufanya kazi kama msambazaji wake ingekuwa sawa, kwani anauwezo wakubeba kiubiki mita. 150 hadi kufikia saa 8.00 mchana, inamana tukifanya kazi usiku na mchana tunaweza kufikia kiubiki mita .300 kwa siku. Alifafanua kuwa eneo la kiwanda hicho kinaukubwa wa mita zaidi ya 4070 ambapo hadi sasa tayari imeshafanyika kiubiki mita 491 sawa na asilimia 12 na kwamba iliaweze kufanikisha hanabudi ndani ya mwezi mmoja kwa usiku na mchana jambo ambalo alisema mkandarasi huyo hawezi kufanya. Mhandisi huyo alifika mbali zaidi nakusema kuwa “ hakuna ushirikiano ambao anapata kutoka kwao , wanachoendelea kukifanya hapa ni kukudanganya mkuu. Imetolewa na Kitengo cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. DC CHONGOLO AWAWEKA NDANI WAKANDARASI WA KAMPUNI YA CRJE KWA KUSHINDWA KUKAMILISHA MRADI WA KUCHAKATA TAKA KWA WAKATI Posted On: November... + Read more »
DC CHONGOLO ATAKA USAWA KWA WATU WENYE ULEMAVU, ASEMA WASINYANYAPALIWE Posted On: November 15th, 2019 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo ameiasa jamii kutojihusisha na tabia ya kuwanyanyapaa watu wenye ulemavu kwakuwa na wao wana haki ya kupata haki zote kama ilivyo kwa watu wengine. Mhe. Chongolo ametoa kauli hiyo leo wakati wa uzinduzi wa kamati ya watu wenye ulemavu uliofanyika Manispaa ya Kinondoni ambapo pamoja na mambo mengine amesema ipo dhana iliyojengeka ya kuwanyanyapaa watu hao na hivyo kueleza kuwa kufanya hivyo ni makosa na kusisitiza kuwa nilazima itendeke haki na usawa. Amesisitiza kuwa watu wenye ulemavu wanahaki ya kupewa nafasi mbalimbali na kusema kuwa wote wenye dhamana ya uongozi katika Halmashauri hiyo ni lazima kuangalia makundi hayo kwa upekee zaidi kwa kutenda haki na usawa. Mhe. Chongolo amefafanua kuwa ili kufikia malengo hayo kila mmoja hakuna budi kushirikiana na kamati hiyo iliyoundwa kuweka miundombinu sawia itakayowezesha walemavu kuishi kwa kupata haki zao na usawa pamoja na kuepusha kunyanyapaliwa kama ilivyo kwa sasa. “ Nawashukuru sana kwakunipa heshima hii ya kuzindua kamati hii ambayo inalenga kusimamia, kushughulikia ipasavyo kutetea haki na usawa wawatu wenye ulemavu” amesema Mhe. Chongolo. Mhe. Chongolo hakusita kueleza changamoto mbalimbali zilizopo katika Halmashauri ya Kinondoni na kusema kuwa sio vijijini tu hata mijini wapo baadhi ya watu wanao wanyanyapaa walemavu kwakuwatenga, kuwaficha pamoja na kuwanyima fursa yakupatiwa huduma kama watu wengine. “ Jamii imekuwa na taswira mbaya yakuona kwamba ulemavu ni changamoto iliyokuwa na madhara , na hivyo kujikita kunyanyapaa, kamati hii imepewa mamlaka, sasa nendeni mkajenge timu nzuri itakayoleta sura ya kubadilisha mtazamo uliopo hivi sasa na kuleta matunda na faida kwao. Awali taarifa ya watu wenye ulemavu, ilieleza kuwa halmashauri inajumla ya kata 20 ambazo zinahudumia watu hao wapatao 1239 ambapo kati yao wanaume ni 724 na wanawake 515. Aidha taarifa hiyo ilieleza kuwa kati ya watu hao wakubwa ni 973 huku watoto wakiwa 266 na kwamba huduma hizo zinatolewa kwakuzingatia sera ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2004, sheria namba 9 ya mwaka 2010 pamoja na mikataba mbalimbali inayohusu watu wenye ulemavu. Ameeleza kuwa , Halmashauri imekuwa ikiviwezesha vyama vya watu wenye ulemavu kwa kuvipatia vifaa saidizi kulingana na aina ya ulemavu sambamba na kuwapatia misaada au kujikimu kwa walio na mazingira hatarishi. Aidha ameeleza kuwa , Kinondoni imekuwa ikiwaunganisha na asasi za kiraia ili waweze kujipatia ujuzi , ajira na misaada ya kujikumu palipo na uhitaji pamoja na kuwawezesha maadhimisho ya watu wenye ulemavu yanayofanyika kila mwaka. Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. DC CHONGOLO ATAKA USAWA KWA WATU WENYE ULEMAVU, ASEMA WASINYANYAPALIWE Posted On: November 15th, 2019 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe.... + Read more »
MEYA SITA ASHAURI WANANCHI KUPENDA BIDHAA ZINAZO ZALISHWA NCHINI, ASEMA ZINA UBORA WA HALI YA JUU Posted On: November 15th, 2019 Mstahiki Meya wa Manispaa ya kinondoni, Mhe. Benjamini Sita ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akikagua mabanda ya maonesho ya wajasiriamali yaliyoandaliwa na Manispaa ya Kinondoni na kuwezeshwa na Mamlaka ya Biashara Tanzania Tan Tredi. Amesema upo mtazamo kwa wananchi waliowengi kuwa bidhaa zinazozalishwa nchini hazina ubora, lakini zipo bidhaa za ngozi zinazozalishwa nchini zenye ubora hivyo amefurahishwa na Manispaa kuandaa maonesho hayo kwani kufanya hivyo ni njia mojawapo ya kuwatia moyo wajasiriamali na hivyo kupata fursa ya kutangaza bidhaa zao. "Tanzania inauwezo mkubwa wa kuzalisha bidhaa za ngozi zenye ubora kutoka kwa wajasiriamali wa ndani na hivyo wananchi waondoe dhana ya watu kwenda kununua bidhaa hizo nje ya nchi" Amesisitiza Mstahiki Meya Kwaupande wake Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi,Dk. Patricia Henjewele alisema kuwa maonesho hayo yamekwenda sambamba na mafunzo ya utangazaji wa bidhaa ambapo wajasiriamali kutoka Manispaa ya Kinondoni wameshiriki na baada ya kumalizika kwa mafunzo na maonesho hayo, Halmashauri imeandaa maonesho mengine yatakayofanyika Disemba 12 hadi 15 katika viwanja vya Tanganyika Pekazi ambapo wajasiriamali kutoka sehemu mbalimbali watashiriki. Kwa upande wao washiriki wa maonesho hayo wameipongeza manispaa ya Kinondoni kwakuandaa mafunzo hayo kwani imekuwa fursa kutangaza bidhaa ambazo wamezizalisha wenyewe na hivyo kuomba wananchi kuwaunga mkono. Imetolewa na Kitengo cha habari na uhusiano Manispaa ya Kinondoni. MEYA SITA ASHAURI WANANCHI KUPENDA BIDHAA ZINAZO ZALISHWA NCHINI, ASEMA ZINA UBORA WA HALI YA JUU Posted On: November 15th, 2019 Mstahi... + Read more »
DC CHONGOLO AWAFUNDA VIJANA WAJASIRIAMALI WA BIDHAA ZA NGOZI KUCHANGAMKIA FURSA ZA MIKOPO YA HALMASHAURI Posted On: November 14th, 2019 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo amewataka vijana kutumia fursa inayotolewa na serikali kupitia halmashauri kupata mikopo isiyokuwa na riba ili waweze kujikwamua kiuchumi. Mhe. Chongolo alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua mafunzo kwa vijana wajasiriamali wanaotengeneza bidhaa za ngozi waliopo katika Manispaa ya Kinondoni ambapo miongoni mwao walipata fursa ya kushiriki maonesho ya wakulima nanenane. Mhe. Chongolo alisema kuwa Manispaa ya Kinondoni inafungu la bajeti kwa ajili ya kutoa mikopo kwa Vijana, wakina mama na watu wenye ulemavu kwa lengo la kuwasaidia kujikwamua katika umasikini hivyo vijana wanapaswa kutumia nafasi hizo wanazozipata kwani itawawezesha kukuza mitaji yao na hivyo kufikia lengo la kuwa na viwanda huku akitolea mfano wa mfanyabiashara mkubwa Marehemu Dk. Reginal Mengi ambaye alifanikiwa kuwa na viwanda kupitia ujasiriamali. Alifafanua kuwa iwapo watatumia vizuri mafunzo hayo yataleta tija katika kukuza uchumi wa ndani na kwamba serikali kupitia halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni itasimamia kupata mikopo hiyo na hivyo kuwawezesha kupata mashine pamoja na eneo la kujenga kiwanda chakutengeneza bidhaa za ngozi. “ Nawapongeza sana idara husika ambayo imeandaa haya mafunzo sambamba na maonyesho ya bidhaa za ngozi, vijana mliopo hapa ,tumieni hii fursa mliyoipata, hakuna mafanikio ya siku moja, wote waliofanikiwa walianza kama nyie hapa” alisema Mhe. Chongolo. “ Tunahitaji watu ambao watakuwa na nia ya kweli ya kujikwamua kiuchumi, inawezekana kuzalisha bidhaa za ngozi kwakuwa Tanzania tunaongoza kwakuwa na mifugo, ukiangalia Dar es Salaam ndio inaongoza kwa kula nyama,kwahiyo tunazana za kutengenezea bidhaa zetu” alifafanua. Kwaupande wake , Meneja ukuzaji Bidhaa kutoka Tan Tredi , Masha Husein alisema kuwa wataendelea kushirikiana na manispaa ya Kinondoni katika kuwaelimisha wajasiriamali namna ya kufanya biashara kwenye maonesho kwani hiyo imekuwa ni changamoto kubwa kwao. Alifafanua kuwa, wajasiriamali wengi hawana uelewa wa kutosha kuhusiana na namna ya kushiriki kwenye maonesho mbalimbali wanapopata nafasi jambo ambalo kama Tan Tredi imeliona na hivyo kusisitiza kuwa watahakikisha wanatoa elimu hiyo ili waweze kunufaika. Naye Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Dk. Patricia Henjewele alimpongeza Mhe. Chongolo kwakujali vijana na kusema kuwa katika maonesho ya nane nane waliona umuhimu wakukutana na wajasiriamali hao na hivyo kuandaa semina hiyo iliyoambatana na maonesho. Aidha aliwapongeza Tan Tredi kwakuwezesha maonesho hayo na hivyo kuahidi kuendeleza ushirikiano zaidi katika kutoa elimu kwa wajasiriamali hao. Imetolewa na Kitengo cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. DC CHONGOLO AWAFUNDA VIJANA WAJASIRIAMALI WA BIDHAA ZA NGOZI KUCHANGAMKIA FURSA ZA MIKOPO YA HALMASHAURI Posted On: November 14th, 2019 ... + Read more »