MEYA SITA ASHAURI WANANCHI KUPENDA BIDHAA ZINAZO ZALISHWA NCHINI, ASEMA ZINA UBORA WA HALI YA JUU
Posted On: November 15th, 2019
Mstahiki Meya wa Manispaa ya kinondoni, Mhe. Benjamini Sita ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akikagua mabanda ya maonesho ya wajasiriamali yaliyoandaliwa na Manispaa ya Kinondoni na kuwezeshwa na Mamlaka ya Biashara Tanzania Tan Tredi.
Amesema upo mtazamo kwa wananchi waliowengi kuwa bidhaa zinazozalishwa nchini hazina ubora, lakini zipo bidhaa za ngozi zinazozalishwa nchini zenye ubora hivyo amefurahishwa na Manispaa kuandaa maonesho hayo kwani kufanya hivyo ni njia mojawapo ya kuwatia moyo wajasiriamali na hivyo kupata fursa ya kutangaza bidhaa zao.
"Tanzania inauwezo mkubwa wa kuzalisha bidhaa za ngozi zenye ubora kutoka kwa wajasiriamali wa ndani na hivyo wananchi waondoe dhana ya watu kwenda kununua bidhaa hizo nje ya nchi" Amesisitiza Mstahiki Meya
Kwaupande wake Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi,Dk. Patricia Henjewele alisema kuwa maonesho hayo yamekwenda sambamba na mafunzo ya utangazaji wa bidhaa ambapo wajasiriamali kutoka Manispaa ya Kinondoni wameshiriki na baada ya kumalizika kwa mafunzo na maonesho hayo, Halmashauri imeandaa maonesho mengine yatakayofanyika Disemba 12 hadi 15 katika viwanja vya Tanganyika Pekazi ambapo wajasiriamali kutoka sehemu mbalimbali watashiriki.
Kwa upande wao washiriki wa maonesho hayo wameipongeza manispaa ya Kinondoni kwakuandaa mafunzo hayo kwani imekuwa fursa kutangaza bidhaa ambazo wamezizalisha wenyewe na hivyo kuomba wananchi kuwaunga mkono.
Imetolewa na
Kitengo cha habari na uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
0 comments:
Post a Comment