KAMATI YA FEDHA NA UONGOZI KINONDONI YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO NA THAMANI YA FEDHA ILIYOTUMIKA Posted On: November 29th, 2018 Kamati hiyo iliyoongozwa na Naibu Meya wa Manispaa, ambaye pia ni diwani wa Kata ya Kigogo Mh George Mangalu Manyama imetembelea miradi mitatu ya maendeleo kwa lengo la kujiridhisha ubora unaoenda sambamba na thamani ya fedha iliyotumika. Katika ziara hiyo iliyohusisha wajumbe wa kamati ambao ni Wah.madiwani, wakuu wa idara na vitengo pamoja na wataalam, imekagua mradi wa ujenzi wa kituo kidogo cha afya kigogo, ujenzi wa soko la sinza 11 kijitonyama, na ujenzi wa barabara ya salasala kinzudi kiwango cha lami, yenye urefu km 0.7 inayojengwa na TARURA . Mh.Mangalu amesema hatua iliyofikiwa miradi hii ni nzuri na ya kuridhisha, inayoonesha mwelekeo wa dhamira ya dhati ya utekelezaji na ukamilishaji wake ili kutoa huduma bora kwa wananchi. "Miradi hii inaendelea vizuri, chamsingi ni kwamba juhudi zaidi ziongezeke kwa miradi hii kukamilika, ili wananchi waweze kupata huduma bora na pia ni vyanzo vizuri vya mapato",Amesisitiza Mangalu. Aidha amewataka wananchi kuwa wazalendo kwa kuhakikisha wanaitunza na kuithamini miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika kata zao, ikiwa ni pamoja na kuwa walinzi wa uchafuzi wa mazingira na kuhakikisha wanaitunza mitaro ili iweze kutumika kwa makusudi kamili. Imeandaliwa na Kitengo cha Uhusiano na habari. Manispaa ya kinondoni. KAMATI YA FEDHA NA UONGOZI KINONDONI YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO NA THAMANI YA FEDHA ILIYOTUMIKA Posted On: November 29th, 2018 Kamati ... + Read more »
MADIWANI KINONDONI WASHIRIKI MAFUNZO YA UANDAAJI BAJETI RAFIKI KWA MTOTO Posted On: November 28th, 2018 Mafunzo hayo yaliyoendeshwa na shirika lisilo la kiserikali la Save the children, kwa kushirikiana na PDF yaliyolenga kutoa upeo na kuainisha umuhimu wa watoa maamuzi, kushiriki katika uaandaaji na upitishaji wa bajeti yenye vipaumbele vya mtoto, yamefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa. Akifafanua mafunzo hayo mratibu wa usalama wa mtoto kutoka shirika la Save the Children, Bi.Haika Harrison amesema, mafunzo haya yamelenga mpango madhubuti wa maandalizi ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2019/2020, iliyorafiki kwa mtoto, inayozingatia huduma muhimu zihusuzo haki ya kuishi na kuendelezwa, elimu, afya, ulinzi pamoja na usalama. Aidha ameeleza pia umuhimu wa kuandaa bajeti kwa kuzingatia vipaumbele vya watoto na kuvitaja kuwa ni kurahisisha utekelezaji wa mipango inayowahusu watoto, kuratibu shughuli mbalimbali, ni nyenzo ya mawasiliano pamoja na kuwa sehemu ya udhibiti wa rasilimali. Naye Bi Neema Bwaira ambaye ni mtaalam wa haki za watoto na utawala bora kutoka shirika la Save the children alipokuwa akitoa mada kuhusiana na uandaaji wa bajeti iliyorafiki kwa mtoto amesema, zipo kanuni za kuzingatia wakati wa uandaaji bajeti iliyorafiki kwa mtoto ambazo ni kutobaguliwa kwa mtoto, kuweka mbele maslahi ya mtoto na umuhimu wa mtoto kujieleza na kutoa maoni. Ameainisha pia sifa ya bajeti ambayo ni rafiki kwa mtoto kuwa ni ile inayotekeleza sera za kiuchumi na za jamii ambazo ni rafiki na zinamaslahi mapana kwa watoto, inayoangalia mahitaji yao muhimu hasa waishio katika mazingira magumu. Nyingine ni ile inayogusa sekta muhimu kama vile elimu, afya, maji safi, usafi wa mazingira, ni ile inayotoa fursa sawa za maendeleo na kuheshimu haki za watoto bila kujali makabila, dini, mikoa au rangi, na yenye kutengeneza mfumo bora na wezeshi katika mtiririko wa rasilimali unaomfikia mtoto kwa wakati. Akichangia mada hiyo ya uaandaaji wa bajeti, Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni Naibu Meya wa Manispaa Mh.Manyama Mangalu amesema, swala hili ni la kisera zaidi, na ni vema ikatolewa elimu ya kutosha juu yake, ili upatikane ufumbuzi wa kudumu unaomjali na kumthamini mtoto. Mafunzo haya yamepata uwakilishi kutoka WAMATA, Right to Play, SISEMA na waku wa Idara na vitengo. Imeandaliwa na Kitengo cha Uhusiano na Habari. Manispaa ya kinondoni. MADIWANI KINONDONI WASHIRIKI MAFUNZO YA UANDAAJI BAJETI RAFIKI KWA MTOTO Posted On: November 28th, 2018 Mafunzo hayo yaliyoendeshwa na ... + Read more »
KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU YAKAGUA MIRADI YA SHULE Posted On: November 29th, 2018 Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Thadei Massawe imetembelea miradi mitano ya shule za awali, msingi na sekondari kwa lengo la kujiridhisha na ukamilishaji wa vigezo vya usajili pamoja na hatua za utekelezaji zilizofikiwa kwa ujenzi wa shule za msingi na sekondari. Akiiongoza kamati hiyo Mhe.Thadei amesema kuboreshwa kwa miundombinu ya elimu ndio msingi imara wa upatikanaji wa elimu iliyo bora, hivyo kama kamati hatuna budi kujiridhisha na swala hilo muhimu kuelekea uchumi wa kati wa viwanda, unaowataka watanzania kijiajiri kupitia elimu. "Miundo mbinu ya elimu pamoja na mazingira vikiboreshwa, hakika vijana wetu watapata elimu iliyobora, kuelekea uchumi wa kati wa viwanda, Serikali yetu ya sasa inathamini sana elimu, na sisi kinondoni tunatekeleza hilo."Ametanabaisha Mhe.Thadei Aidha kamati wamesisitiza ukaguzi wa mara kwa mara wa taasisi binafsi na shule ili kujiridhisha si tu ubora wake, bali hata elimu inayotolewa pale kwani wataalamu wa elimu wapo na hasa ikizingatiwa jamii imara hujengwa na taasisi imara. Shule zilizotembelewa ni shule ya awali na msingi Kisanga iliyopo Wazo, Shule ya awali Jubilation iliyopo Bunju, Shule ya awali na Msingi Erastus iliyopo Mabwepande, Shule ya Sekondari crown iliyopo Mbezi beach Makonde, na Shule ya awali na msingi Readers Rabbits iliyopo Msasani. Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Uhusiano. Manispaa ya Kinondoni. KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU YAKAGUA MIRADI YA SHULE Posted On: November 29th, 2018 Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake M... + Read more »
KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA KINONDONI, YABAINI UTORO KWA WALENGWA WA DAWA ZA KUFUBAZA VVU(ARV) Posted On: November 28th, 2018 Kamati ya kudhibiti UKIMWI Manispaa ya Kinondoni (CMAC) chini ya mwenyekiti wake ambae pia ni naibu Meya wa Manispaa hiyo Mhe. George Manyama imebaini kuwepo kwa utoro wa walengwa wa dawa za kufubaza VVU, hali ambayo inahatarisha usalama wa afya za wagonjwa hao. Hayo yamebainika leo wakati wa ziara ya kutembelea vituo vya kutolea huduma kwa Watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi ( CTC) , vilivyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala na kituo Cha afya Tandale kwa lengo la kuona hali halisi ya utoaji wa huduma, upatikanaji wa huduma kwa WAVU pamoja na Changamoto. Akizungumnzia swala hilo la utoro, Mh.Manyama amesema " Hali hii inatishia mapambano yanayoendelea ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya UKIMWI, hivyo ni lazima kwa watoa huduma na wadau mbalimbali tushirikiane na serikali Katika kuongeza juhudi za utoaji wa elimu kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI ili waelewe umuhimu wa kuhudhuria cliniki kikamilifu". Awali akitoa taarifa yake mbele ya kamati, Mkuu wa kitengo Cha Watu wanaoishi na virusi vya ukimwi Katika hospitali ya mwananyamala Dkt Rehema Mzalau amesema, kwa kipindi Cha mwaka mmoja uliopita idadi ya wagonjwa watoro ni 400, na kubainisha mikakati itakayowawezesha kupatikana kwa wagonjwa hao ili kuzuia uwezekano wa kuambukiza wengine. Dkt Rehema pia, ameainisha mafanikio yaliyopo kwenye kituo hiko hadi sasa kuwa ni kufanikiwa kupunguza ongezeko la maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto (PPMCTC) Kwani kwa kipindi Cha Mwaka mmoja uliopita kituo kimepata maambukizi 0. Kwa upande wake mratibu wa Kudhibiti maambukizi ya UKIMWI Manispaa ya Kinondoni Bi Rhobi Gwesso amewasihi wanakamati kuwa sehemu ya uwakilishi katika kutoa elimu kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI juu ya umuhimu wa kuendelea kutumia dawa za VVU, kwani dawa hizi zinafubaza virusi na si kuua virusi. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na uhusiano Manispaa ya Kinondoni. KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA KINONDONI, YABAINI UTORO KWA WALENGWA WA DAWA ZA KUFUBAZA VVU(ARV) Posted On: November 28th, 2018 ... + Read more »
KAMATI YA MIPANGOMIJI NA MAZINGIRA MANISPAA YA KINONDONI YAKAGUA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO Posted On: November 28th, 2018 Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake ambaye pia ni diwani wa Kata ya Mwananyamala Mhe. Songoro Mnyonge, leo imekagua miradi mitatu ya maendeleo kwa lengo la kujiridhisha utekelezaji wake, ikiwa ni pamoja na kukagua hatua za utekelezaji zilizofikiwa. Akikagua miradi hiyo, Mhe.Songoro amesema kukamilika kwake kwa wakati ndio lengo lililokusudiwa, kwani maeneo haya ya mradi ni ya kimkakati, na wananchi wanahitaji huduma bora na zenye viwango. "Haya yote ni maeneo ya kimkakati kwa maendeleo ya Halmashauri yetu, hivyo yatupasa kufanya na kupanga mikakati hii ili iendane sambamba na mabadiliko ya jamii yetu."Amesisitiza Mnyonge Miradi hiyo iliyotembelewa ni mradi wa ujenzi wa kiwanda cha uchakataji taka Mabwepande chini ya mkandarasi CRJE, mradi wa ujenzi wa barabara ya Tegeta nyuki urefu wa km 2.2 unaojengwa na TARURA, kwa kiwango cha lami, na mradi unaojishughulisha na utoaji wa namba za Mitaa (Post Code), ulioko Kijitonyama chini ya Manispaa kwa kushirikiana na TCRA. Katika hatua nyingine, wajumbe wa kamati wameushukuru uongozi wa Manispaa, kwa uibuaji na utekelezaji mzuri wa miradi ya kimkakati na kuelekeza ufanyikaji mzuri wa maboresho utakaoleta tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla. Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Uhusiano. Manispaa ya Kinondoni. KAMATI YA MIPANGOMIJI NA MAZINGIRA MANISPAA YA KINONDONI YAKAGUA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO Posted On: November 28th, 2018 Kama... + Read more »
SEMINA ELEKEZI KUHUSIANA NA MAANDALIZI YA BAJETI 2019/2020 PAMOJA NA VIPAUMBELE VILIVYORAFIKI KWA MTOTO YAENDESHWA KINONDONI Posted On: November 27th, 2018 Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na maswala ya usalama wa mtoto liitwalo Save the Children kwa kushirikiana na PDF, leo limeendesha semina yenye lengo la kutoa elimu ihusuyo uandaaji wa bajeti na vipaumbele vyake kwa mwaka wa fedha 2019/2020, kwa maswala mbalimbali ya watoto. Akiendesha semina hiyo mwakilishi kutoka shirika la Save the children Bi Neema Bwaira amesema maswala yahusuyo watoto katika vitengo na idara ni mtambuka, na hivyo hatuna budi kuweka bajeti inayomgusa mtoto katika utekelezaji wa majukumu ya kilasiku. Bi Neema pia ameainisha sifa ya bajeti ambayo ni rafiki kwa mtoto kuwa ni ile inayotekeleza sera za kiuchumi na za jamii ambazo ni rafiki na zinamaslahi mapana kwa watoto na inaangalia mahitaji muhimu ya watoto waishio katika mazingira magumu. Ameendelea kuziainisha kuwa ni ile inayogusa sekta muhimu kama vile elimu, afya, maji safi, usafi wa mazingira, ni ile inayotoa fursa sawa za maendeleo na kuheshimu haki za watoto bila kujali makabila, dini, mikoa au rangi, na yenye kutengeneza mfumo bora na wezeshi katika mtiririko wa rasilimali unaomfikia mtoto kwa wakati. Akianisha mpango wa bajeti na mchakato wa uandaaji wake kwa Manispaa ya kinondoni, Bi.Febronia Luyagaza, kwa niaba ya mchumi amesema, kabla ya mchakato wa bajeti kuanza yapo mfunzo yanayotolewa kwa lengo la kumsaidia Mkuu wa idara na Afisa bajeti kuibua vipaumbele atakavyovitekeleza ikiwa ni pamoja na kumsaidia muandaaji kuibua majukumu katika maeneo yake. Aidha amewasisitiza wakuu wa idara na vitengo kuhakikisha wanashiriki mchakato wa uandaaji wa bajeti ili kuepukana na malalamiko yanayotokea kuhusiana na kuondolewa baadhi ya kazi au kupunguzwa kwa fedha kwenye kazi iliyobajetiwa. Semina hii imepata uwakilishi kutoka WAMATA, Right to Play, SISEMA na waku wa Idara na vitengo. Imeandaliwa na Kitengo cha Uhusiano na Habari. Manispaa ya kinondoni. SEMINA ELEKEZI KUHUSIANA NA MAANDALIZI YA BAJETI 2019/2020 PAMOJA NA VIPAUMBELE VILIVYORAFIKI KWA MTOTO YAENDESHWA KINONDONI Posted On: N... + Read more »