Top ad

Top ad

TATHMINI YA MATOKEO YA MTIHANI WA KWANZA WA UTAMILIFU (MOCK) DARASA LA SABA KINONDONI YATOLEWA

Posted On: April 12th, 2019
Akitoa tathmini hiyo leo,  Afisa elimu msingi Manispaa ya Kinondoni Bw.Kiduma Mageni amesema,  jumla ya shule 138, zenye wanafunzi  12, 622, walifanya mtihani huo ambao ni sawa na asilimia 99.33% na kati yake waliofaulu ni 9,302, sawa na asilimia 74.20%
Amesema lengo la mtihani huu ni kutekeleza mkakati maalum wa kuhakikisha inaendelea kufanya vizuri kitaaluma hasa ikizingatiwa Kinondoni ilishika nafasi ya tatu Kimkoa kwa ufaulu wa asilimia 95.70%, matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi (PSLE) 2018.
"Kinondoni iliandaa mkakati maalumu wa kuendelea kufanya vizuri zaidi kitaaluma kwa kuhakikisha inaendesha mitihani miwili ya utamilifu kiwilaya kwa wanafunzi wa darasa la saba 2019 na mtihani huo ulifanyika tarehe 27-28/03/2019" Amefafanua Mageni.
Aidha amezitaja shule tatu za serikali zilizofanya vizuri kuwa ni   Msisiri, Victoria na Lugalo na shule za binafsi ni Royal Elite, Mother's of Mercy na Libermann.
 Amewataka walimu kutumia Matokeo haya kama chachu ya kurekebisha changamoto ndogondogo zilizoonekana ili kuweza kufanya vizuri mitihani ijayo ya ngazi ya Mkoa na Taifa.
Katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Oysterbay na kuenda sambamba na ugawaji zawadi kwa shule zilizofanya,vizuri kutoka  CRDB Bank, pia imehudhuriwa na  waalimu wakuu, waratibu wa Elimu Kata pamoja na waalimu wa darasa la saba.
Imeandaliwa na  
Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.

0 comments:

Post a Comment

 
Top