KINONDONI YASAINI MAKUBALIANO YA MASHIRIKIANO NA MJI WA LOUD ULIOPO JIMBO LA HUNAN KUTOKA JAMHURI YA WATU WA CHINA.
Posted On: March 29th, 2019
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni leo imetiliana saini makubaliano ya mashirikiano na mji wa Loud uliopo Jimbo la Hunan Kutoka Jamhuri ya watu wa China wenye lengo la kukuza soko la kibiashara na kuimarisha mahusiano ya kirafiki ya pande zote mbili.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Dkt Patricia Henjewele amesema kuwa ni heshima kubwa kwa Manispaa ya Kinondoni kupokea ujumbe huo kutoka Jimbo la Hunan ukiongozwa na Peng Zheng ambae ni mkuu wa sehemu wa ofisi ya mashirikiano ya idara ya Biashara ya Jimbo la Hunan.
Aliuhakikishia ujumbe huo kuwa Kinondoni inamazingira mazuri ya uwekezaji yenye vivutio mbalimbali Katika maeneo ya Afya, mazingira, Uchumi, Kilimo, Mifugo, uvuvi, makazi , Habari na Mawasiliano yatakayowezesha upanuzi wa mji na maendeleo ya mji.
Ninaamini mahusiano haya yatakuwa na matokeo makubwa Katika maeneo Muhimu ya uwekaji kama vile shughuli za kibiashara, masoko, makazi, michezo , utalii, utamaduni, Elimu , Afya , Utalii, utumishi, upangaji na uboreshaji wa miji pamoja na shemu za kiburudani. Ameongeza Dkt Henjewele.
Kwa upande wake Mstahiki meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamin Kawe Sitta alitoa shukrani za dhati kwa timu nzima iliyoshiriki kufanikisha mashirikiano hayo ikiwa ni pamoja na wizara ya fedha na mipango, idara ya uwekezaji Tanzania pamoja na Wizara ya Mambo ya nje kwa kutenga muda wao kuungana na Manispaa kufanikisha majadiliano yalipopelekea kufikia makubaliano ya mahusiano haya.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe Daniel Chongolo akishuhudia utilianaji saini makubaliano hayo ametoa shukrani zake za dhati kwa Ndugu Peng Zheng na kuuhakikishia ujumbe toka China kuwa wilaya ya Kinondoni inamazingira tulivu na hali ya hewa safi hivyo wageni waje kuwekeza wilaya ya Kinondoni yenye fursa nyingi za uwekezaji.
Amesema yeye kama kiongozi mkuu wa serikali atawapa ushirikiano wa kutosha ili kufikia malengo ya makubaliano haya ya ushirikiano wa kirafiki.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari Mwasiliano na uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
0 comments:
Post a Comment