KUELEKEA KILELE,CHA SIKU YA UKIMWI DUNIANI, KINONDONI YAHAMASISHA VIJANA KUPIMA NA KUJUA AFYA ZAO Posted On: December 3rd, 2018 Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na Asasi ya vijana ya YOP kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi duniani, imehamasisha vijana kupima na kujua afya zao ili waweze kujilinda na kujiepusha na maambukizi dhidi ya VVU. Hayo yamethibitika leo katika tamasha la michezo lililoshirikisha vijana na wadau mbalimbali wanaoshiriki mapambano ya kudhibiti ukimwi ikiwa ni hatua ya maandalizi kuelekea kilele cha maadhimisho hayo ya UKIMWI kwa kuwataka vijana kupima afya zao. Akiongea katika maadhimisho hayo kwa niaba ya mgeni rasmi, Mtendaji wa kata ya Mwananyamala Ndg. Mikidadi S. Ngatupura amesema, afya ndio msingi wa maendeleo, hivyo kwa vijana kujua hali zao mapema itawapa fursa ya kujiwekea malengo yao katika kusukuma gurudumu la maendeleo "Vijana lazima mtambue afya zenu ili muweze kuyaishi malengo yenu, kama si afya bora hamuwezi kufikia malengo mliojiwekea, nawasihi mjiepushe na mambo yote ambayo yanaweza kupelekea kupata maambukizi ya virusi vya UKIMWI."Amesisitiza Mtendaji. Kwa upande wake mwakilishi wa shirika la JHPIEGO Bi Happy Temu akitoa matokeo ya vipimo vya afya vilivyofanyika uwanjani hapo amesema uelewa umekuwa mkubwa kwani kati ya vijana 102, waliojitokeza kupima ambapo wasichana ni 33, na wavulana ni 69, matokeo yanaonesha kutopatikana kwa yeyote mwenye maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Katika hatua nyingine, maadhimisho hayo yalienda sambamba na mashindano ya mpira wa miguu ambapo timu za Mwenge combaini FC na African People zilichuana vikali na Mwenge combaini kuibuka kidedea kwa kumbamiza African people bao 2 kwa 1. Maadhimisho haya pia yalipata ushiriki kutoka shirika la UNA, WAMATA pamoja na baraza la watu wanaoishi na virus vya UKIMWI. Imeandaliwa na kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. KUELEKEA KILELE,CHA SIKU YA UKIMWI DUNIANI, KINONDONI YAHAMASISHA VIJANA KUPIMA NA KUJUA AFYA ZAO Posted On: December 3rd, 2018 Manispa... + Read more »
VIJANA WILAYA YA KINONDONI, WAMETAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA MIKOPO ZINAZOTOLEWA, ILI WAWEZE KUJIKWAMUA KIUCHUMI Posted On: December 3rd, 2018 Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Daniel Chongolo, alipokuwa mgeni rasmi katika semina ya siku mbili iliyofanyika katika ukumbi wa shule ya Msingi oysterbay, ikihusisha wajasiriamali kutoka kata zote 20, kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu katika maswala ya mikopo na fursa zilizopo. Amesema mafunzo haya na mikopo hii iliyo na riba nafuu, ikawe chachu ya kujishughulisha kwani ndio msingi madhubuti wa maendeleo kwa vijana hasa ikizingatiwa Serikali ya awamu ya tano, imelenga kuimarisha uchumi wa vijana na kinamama kwa kujishughulisha na ujasiriamali. "Sitegemei wala sitaki kuletewa kesi za mtu kutaka kuuziwa vitu vyake kwa sababu ya kumdhamini mtu mwingine au kwa kushindwa kurejesha mikopo na wakati serikali imetoa mikopo kwa vijana na wajasiriamali tena bila riba" amefafanua Mhe Chongolo. Akizungumnzia mafunzo hayo Mkurugenzi kutoka TAEDO ndg Kenan Kihongozi amesema semina hii ni madhubuti kwa ajili ya vijana na hata mada zilizoandaliwa ni mahususi kuziendea fursa hasa za kiuchumi, kwani mikopo bila elimu kwaweza kuwa kikwazo cha kujikwamua na fursa hizo. Amezitaja mada zilizofundishwa katika semina hiyo kuwa ni jinsi ya kufanya ufugaji bora wa kuku, utengenezaji wa sabuni za unga, maji na vipande, jiki, mbegu za vitunguu, mbolea ya maji na utengenezaji wa sabuni au dawa za kusafishia sakafu na marumaru. Katika hatua nyingine, wajasiriamali hao wameishukuru Serikali kwa kuwapa mikopo, hali inayotoa hamasa kwao ya kutafuta vitegauchumi mbalimbali kupitia hiyo mikopo. Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kindoni. VIJANA WILAYA YA KINONDONI, WAMETAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA MIKOPO ZINAZOTOLEWA, ILI WAWEZE KUJIKWAMUA KIUCHUMI Posted On: December 3rd,... + Read more »