NILAZIMA MUWE WASIMAMIZI WA JUMLA WA SHUGHULI ZA SERIKALI KATIKA MAENEO YENU" Posted On: November 1st, 2018 Ni agizo lake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Daniel Chongolo alipokuwa akiongea na Maafisa Ugani wa Kata ya Bunju katika ziara yake aliyoifanya leo. Amesema Maafisa ugani, watendaji wa Kata na Mitaa katika maeneo yao wanatakiwa kuhakikisha wanawajibika ipasavyo ili kero za wananchi zinazowakabili zitatuliwe kwa ufanisi, umakini, na usawa utakaoleta tija iliyokusudiwa. "Kutenda haki kunajengwa kwa kutimiza wajibu, nilazima muwe wasimamizi wajumla wa shughuli za Serikali katika maeneo yenu, ikiwa ni pamoja na kutoa huduma stahiki kwa wananchi" Amesisitiza Mh.Chongolo. Akisoma taarifa za Kata ya Bunju kwa Mkuu wa Wilaya, Mtendaji wa Kata hiyo Bw.Ibrahim Mabewa amesema Kata yake inamitaa 6, ambayo ni Bunju A, Mkoani, Dovya, Kilungule, Boko, na Basihaya na idadi ya watu kuwa takribani 63,248, na hii ni kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012. Aidha amezitaja changamoto zinazoikabili Kata hiyo ya Bunju kuwa ni Uchimbaji wa kokoto na vifusi, Uchimbaji holela wa mchanga maeneo ya Nyakasangwe, Dampo la taka kuwa mbali na mrundikano wa takataka. Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya ameupongeza uongozi mzima wa Halmashauri kwa ufaulu wa asilimia 95.7, matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2018, uliopelekea Kinondoni kuwa ya kwanza kimkoa, na ya tatu kitaifa. Katika ziara yake hiyo, Mkuu huyo wa Wilaya alitembelea maeneo ya shule ya msingi Mkoani, soko la Bunju A, mifereji ya Basi haya, na baadae kufanya mkutano wa hadhara na wananchi katika viwanja vya shule ya Bunju, kwa lengo la kusikiliza kero zao na kuzipatia majibu. Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Uhusiano. Manispaa ya Kinondoni. NILAZIMA MUWE WASIMAMIZI WA JUMLA WA SHUGHULI ZA SERIKALI KATIKA MAENEO YENU" Posted On: November 1st, 2018 Ni agizo lake Mkuu wa ... + Read more »
DC KINONDONI ATOA SIKU SABA KWA WAKANDARASI WA TAKA KUBORESHA HUDUMA HIYO Posted On: November 7th, 2018 NI KUFUATIA KUKITHIRI KWA MALALAMIKO YA WANANCHI KUHUSIANA NA TAKA ZILIZORUNDIKANA MITAANI. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Daniel Chongolo ametoa siku saba kwa wakandarasi wa huduma ya kuzoa taka pamoja na Manispaa kuhakikisha wanaboresha utoaji wa huduma hiyo kwenye mitaa husika ili kuondokana na kero inayowasumbua wananchi ya mrundikano wa matakataka. Ametoa agizo hilo leo alipokuwa katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijitonyama uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Kijitonyama kisiwani kwa lengo la kusikiliza kero zao na kuzipatia majibu. Amesema iwapo wananchi wanachangia fedha zao kwa ajili ya huduma hiyo, nilazima waipate, kwani kukithiri kwa matakataka mitaani kwaweza kuleta magonjwa ya mlipuko yanayotokana na uchafu. "Natoa agizo, kufika siku ya Jumanne kuanzia leo, kuwe na mwelekeo madhubuti wa kutoa taka kwenye Kata na Mitaa yetu" Ameagiza Chongolo. Akitoa ufafanuzi wa swala hilo, Ndg Peter Abilu ambaye pia ni Afisa Usafishaji wa Manispaa hiyo amesema, kwa sasa Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na Maafisa watendaji wa Kata na Mitaa, pamoja na Wakandarasi wa kuzoa taka tumeandaa mpango mkakati utakaoondoa kero hiyo na mazingira kubaki masafi. Awali akitoa taarifa ya Kata ya Kijitonyama kwa Mkuu huyo wa Wilaya, Mtendaji wa Kata hiyo Bi.Elizabeth Minga amesema Kata yake inajumla ya Mitaa Nane, shule za Msingi 7, Sekondari 4, vituo vya polisi 3, Zahanati 2, Masoko 3, Hotel 18, Nyumba za kulala wageni 31, na Bar 50. Aidha ameainisha changamoto kubwa zinazowakabili katika Kata hiyo kuwa ni wananchi kujimilikisha maeneo ya wazi, ujenzi juu ya mifereji na pembezoni mwa kingo, na uthibiti wa taka ngumu. Akipokea maagizo na maelekezo ya Mkuu wa Wilaya, kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa, Ndg Maduhu Kazi ambaye pia ni Afisa Mipangomiji ameahidi kuyafanyia kazi maagizo na maelekezo yote yaliyotolewa, ikiwa ni pamoja na kutatua kero zinazowakabili wananchi. Hii ni ziara yake ya pili ambapo ametembelea na kukagua miradi inayotekelezwa katika kata ya Kijitonyama, na kufanya mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na wananchi, wakuu wa idara na vitengo pamoja na viongozi mbalimbali wa Kata na Taasisi za Serikali ambapo ziara yake ya kwanza ilifanyika katika kata ya Bunju. Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Uhusiano. Manispaa ya Kinondoni. DC KINONDONI ATOA SIKU SABA KWA WAKANDARASI WA TAKA KUBORESHA HUDUMA HIYO Posted On: November 7th, 2018 NI KUFUATIA KUKITHIRI KWA MALAL... + Read more »