Top ad

Top ad

KUJIANDIKISHA KUHUDHURIA MNADA WA VIWANJA VYA BIASHARA  KATIKA MRADI WA BUNJU/MABWEPANDE

                                                                  Bonyeza link hiii

KUAHIRISHWA KWA MNADA WA MAUZO YA VIWANJA MABWEPANDE

MKURUGENZI WA MANISPAA YA KINONDONI ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE KUWA, MNADA WA HADHARA WA MAUZO YA VIWANJA ULIOPANGWA KUFANYIKA TAREHE 30/05/2015 SIKU YA JUMAMOSI SAA TATU (3.00) ASUBUHI UMEAHIRISHWA HADI TAREHE 6/06/2015 SIKU YA JUMAMOSI SAA TATU (3.00) ASUBUHI.
MNADA HUO UTAFANYIKA NDANI YA UKUMBI WA MIKUTANO KATIKA MANISPAA YA KINONDONI

RAMANI ZA UPIMAJI WA VIWANJA HIVYO ZITAKUWEPO KATIKA OFISI YA ARDHI YA MANISPAA KWA AJILI YA KUCHAGUA VIWANJA KABLA YA SIKU YA MNADA.
MSHINDI KATIKA MNADA HUO, ATALIPA PAPO HAPO FEDHA TASLIM ASILIMIA ISHIRINI NA TANO (25%) YA MAUZO NA KUMALIZIA ASILIMIA SABINI NA TANO (75%) NDANI YA SIKU KUMI NA NNE (14) KUTOKA SIKU YA MNADA.
ENDAPO MALIPO YALIYOSALIA HAYATALIPWA KWA WAKATI, MALIPO YA AWALI HAYATAREJESHWA KWA MLIPAJI.
VIWANJA HIVYO VIPO ENEO LA MABWEPANDE UMBALI WA KILOMITA 4 KUTOKA BUNJU ‘B’ BARABARA BAGAMOYO.
MNADA HUO UTAFANYIKA NDANI YA UKUMBI WA MIKUTANO KATIKA MANISPAA YA KINONDONI


RAMANI ZA UPIMAJI WA VIWANJA HIVYO ZITAKUWEPO KATIKA OFISI YA ARDHI YA MANISPAA KWA AJILI YA KUCHAGUA VIWANJA KABLA YA SIKU YA MNADA. MSHINDI KATIKA MNADA HUO, ATALIPA PAPO HAPO FEDHA TASLIM ASILIMIA ISHIRINI NA TANO (25%) YA MAUZO NA KUMALIZIA ASILIMIA SABINI NA TANO (75%) NDANI YA SIKU KUMI NA NNE (14) KUTOKA SIKU YA MNADA. ENDAPO MALIPO YALIYOSALIA HAYATALIPWA KWA WAKATI, MALIPO YA AWALI HAYATAREJESHWA KWA MLIPAJI. VIWANJA HIVYO VIPO ENEO LA MABWEPANDE UMBALI WA KILOMITA 4 KUTOKA BUNJU ‘B’ BARABARA BAGAMOYO.WASHIRIKI WOTE WANATAKIWA KULIPIA KIASI CHA ELFU HAMSINI ( 50,000/=) KAMA ADA YA USHIRIKI .
RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Dr JAKAYA MRISHO KIKWETE AWAPA POLE WAATHIRIKA WA MVUA ZINAZOENDELEA KUSHESHA KATIKA MANISPAA YA KINONDONI .

Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametembelea wilaya ya Kinondoni kujionea hali halisi ya athari za mafuriko katika kata ya kunduchi eneo la Basihaya na Dawasco.Pamoja nae katika tukio hilo alikuwepo Mkuu wa wilaya Poul Makonda,Mstahiki Meya wa Kinondoni Yusuph Mwenda,Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mussa Natty na baadhi ya watendaji wa Manispaa ya Kinondoni.Sababu mbalimbali za mafuriko hayo zimetajwa ambapo Mheshimiwa Rais ameagiza matatizo hayo yashughulikiwe haraka kwani tatizo hilo ni dharula ili kuokoa maisha ya wananchi wanaotangatanga na kukosa sehemu ya kuishi kutokana na nyumba zao kukumbwa na mafuriko.Pamoja na hayo amewapa pole waathirika hao na kuwaahidi kwamba matatizo yao yatashughulikiwa mara moja na watendaji.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh Yusuph Mwenda akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Munngano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa ziara hiyo 

 

Raisi akiwa anaangalia hali halisi ilivyo katika maeneo yaliyoadhiriwa na maji katika Eneo la Basi haya Katika Manispaa ya Kinondoni


msafara wa Rais ulipokuwa unawasili katika maeneo yaliyopata athari za mvua 


Mkuuu wa wilaya ya Kinondoni akitoa maelezo kwa Rais ya hali halisi ya maafuriko huku Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Eng Mussa Natty  (mwenye shati la bluu)  akimsikiliza kwa makini   Raisi akimuelekeza jambo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda 

 
Hali halisi ya Maafuriko kama inavyoonekana katika picha Ghorofa ikiwa imezingirwa na maji 


Watu wamehama makazi 


Baadhi ya wahanga wa Mafuriko wamehamia Katika Vituo vya Mabasi eneo la jangwani 


Raisi Akiwa anatoa agizo kwa uongozi mzima wa Manispaa kuanzia Kulia ni Engineer mkuu wa Manispaa Ndugu Baraka Mkuya, Akiwafuatiwa na Mstahiki Meya Mh yusuph Mwenda, Mkuu wa wilaya ya kinondoni Mh Paul Makonda na Mkurugenzi wa Manispaa Eng Mussa natty aliyevaa shati la blue 


0 comments:

Post a Comment

 
Top