KINONDONI YAADHIMISHA SIKU YA MOYO DUNIANI KWA VITENDOPosted On: September 29th, 2020Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), leo wameadhimisha siku ya Moyo Duniani kwa kutoa huduma mbalimbali kwa wanachi.Maadhimisho hayo yaliyoenda kwa kauli mbiu isemayo "Tambua namba yako ya uzito, pressure na Sukari" yamefanyika katika viwanja vya Tanganyika pekers kwa kutoa huduma za kupima uzito, kupima shinikizo la damu, Sukari, kupima moyo pamoja na vipimo vya ECG.Akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo, mratibu katika maadhimisho hayo DR. Omary Mwangaza amesema wameendesha huduma hizi kwani ndio magonjwa yasiyo na dalili zinazoonekana kwa haraka yanayoshambulia nguvu kazi ya Taifa kwa kiwango kikubwa.Amesema " Kila tarehe 29/09 kila mwaka ni siku ya kuadhimisha ugonjwa wa Moyo duniani, na kwa kauli mbiu hii ya mwaka huu inayotutaka kutambua namba yako ya uzito, pressure na Sukari",ni kaulimbiu shirikishi inayomtaka mwanachi kuchukua hatua kwani magonjwa haya dalili zake hazijitokezi kwa haraka na kusababisha tatizo kuwa kubwa kwa kuchelewa kutibiwa pindi inapompasa mtu kufanya hivyo ". DR.OmaryNaye Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI) Prof. Mohamed Janabi amesema ni vema watanzania wakawa na utaratibu wa kupima afya zao hasa vipimo vya moyo kwani moyo ni kiungo kikubwa katika mwili, hivyo kikiwa na tatizo na afya nzima ya mwili itakuwa na tatizo na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Kawe kuadhimisha kwa pamoja siku hii ambapo huduma za vipimo hizo kwa siku ya leo ni bure.Imeandaliwa naKitengo cha Uhusiano na HabariManispaa ya Kinondoni KINONDONI YAADHIMISHA SIKU YA MOYO DUNIANI KWA VITENDO Posted On: September 29th, 2020 Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na Taasisi y... + Read more »
KINONDONI YAWASHUKIA WAUZAJI WA MBWA NA PAKA KIHOLELAPosted On: September 28th, 2020 Kinondoni imetoa onyo kali kwa watu wanaouza wanyama jamii ya mbwa na Paka kiholela kwani kwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria ya ufugaji mjini.Onyo hilo limetolewa leo na katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bi Stella Msofe, alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya kichaa Cha mbwa Duniani yenye kaulimbiu isemayo "TOKOMEZA KICHAA CHA MBWA: TUSHIRIKIANE, KUCHANJA" na kuzindua rasmi chanjo ya ugonjwa wa kichwa cha mbwa hafla iliyofanyika katika viwanja vya Tanganyika Packer's.Amesema sheria hairuhusu mbwa na paka kupangwa barabarani na kuuzwa, wanyama hawa Wana haki zao na kuna maeneo maalum ambayo biashara hii inatakiwa kufanyika, hivyo Wananchi wafuate sheria ili kwa pamoja tuweze kutokomeza magonjwa yanayozeza kutoka kwao wanyama na kuja kwa binaadamu ukiwemo huu wa Kichaa cha mbwa."Napenda kutumia maadhimisho ya siku hii kuwakumbusha wenzetu wanaoishi na mifugo majumbani mwao kufuata sheria za ufugaji mjini ili kudhibiti mbwa wanaozurura na Wananchi waache mara moja biashara ya kuuza mbwa barabarani" Ameongeza Bi Msofe.Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya mifugo na uvuvi Manispaa ya Kinondoni Bi Patricia Henjewele amesema ugonjwa wa kichwa cha mbwa unaowapata mbwa pia unawapata binaadamu, na ni vigumu kutibu binaadamu ambae anakuwa ameambukizwa ugonjwa huu hivyo ni bora zaidi kuchanja mifugo ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa. Amesema zoezi la chanjo kwa mbwa na paka ambalo limezinduliwa leo, litakuwa endelevu kwa kipindi cha mwezi mzima katika kata mbalimbali zilizopo wilaya ya Kinondoni hivyo Wananchi wawasiliane na Maafisa mifugo wa kata husika.Aidha amewashukuru Taasisi ya Every living Things inayojihusisha na haki za wanyama hususani wanyama wanaozurura mitaani kwa kushirikiana na Manispaa ya Kinondoni kutokomeza ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa.Siku ya kichaa cha mbwa duniani huadhimishwa kila ifikapo Tar 28 mwezi Septemba ambapo kwa Kinondoni wameadhimisha kwa kutoa chanjo kwa mbwa na paka dhidi ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa, Kutibu wanyama watakaogundulika na magonjwa ya aina mbalimbali, Kuogesha wanyama kwa lengo la kuua kupe na viroboto na kukata kucha zilizodidi.Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na UhusianoManispaa ya Kinondoni. KINONDONI YAWASHUKIA WAUZAJI WA MBWA NA PAKA KIHOLELA Posted On: September 28th, 2020 Kinondoni imetoa onyo kali kwa watu wanaouza wanyam... + Read more »
BARAZA LA WAZEE KINONDONI KUUNGANA NA WENZAO MKOA WA DAR ES SALAAM KUSHEREKEA SIKU YA WAZEE DUNIANIPosted On: September 26th, 2020Sherehe hizo zinazoambatana na kauli mbiu isemayo "familia na jamii tuwajibike kuwatunza wazee" zinatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi Tar 3 Oktoba katika viwanja vya Mnazi mmoja yakiwa ni makubaliano yaliyofikiwa leo katika kikao cha robo ya kwanza ya mwaka 2020-2021 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa .Akitoa hoja hiyo katika katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Baraza hilo Bw Wallace K. Mwakikalo amesema huo utakuwa wakati mzuri kwao kutoa matamko ya pamoja na kuweka mipaka ya kimajukumu kati ya mabaraza ya wazee na vikundi mbalimbali vya kusaidia wazee.Ameongeza kuwa katika maadhimisho hayo pia itakuwa ni nafasi pekee ya kupanga mikakati yao ya kupambana na changamoto zinazowakabili pamoja kama Mkoa na kubadilishana uzoefu." Kumekuwa na changamoto ya muingiliano wa majukumu Kati ya baraza la wazee na hivi vikundi vya kijamii vinavyofanya kazi na jamii ya wazee, huu utakuwa wakati mzuri kwetu kutoa tamko la mipaka ya kimajukumu tukiwa na viongozi wetu wa mkoa wa Dar es salaam" Kwa upande wake Katibu wa Baraza hilo Bi Neema Mwalubilo amesema Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika tarehe 3 mwezi ujao katika viwanja vya mnazi mmoja ambapo wazee wa kinondoni watajumuika na wazee wengine katika kuhadhimisha siku yao muhimu.Naye Afisa ustawi wa Manispaa ya Kinondoni Bi.Judith Kimaro amelitaka Baraza hilo kuwa balozi kwa wazee kujiunga na mfuko wa (ICHF), ili wawe na uhakika wa matibabu pale wanapoumwa na wazee hao kuwa mabalozi wazuri kwa wenzao wasio na uwezo wa kupata matibabu kwa kuwasaidia waweze kupatiwa kadi za msamaha wa matibabu.Imeandaliwa nakitengo cha habari na UhusianoManispaa ya Kinondoni. BARAZA LA WAZEE KINONDONI KUUNGANA NA WENZAO MKOA WA DAR ES SALAAM KUSHEREKEA SIKU YA WAZEE DUNIANI Posted On: September 26th, 2020 Shereh... + Read more »