TAMISEMI KWA KUSHIRIKIANA NA WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA YAUNGA MKONO JITIHADA ZA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU KINONDONI Posted On: July 10th, 2019 NI KUPITIA MPANGO WA LIPA KUTOKANA NA MATOKEO (EP4R), KWA KUTOA MILIONI 75, KUKAMILISHA UJENZI WA MIUNDOMBINU SHULE YA MSINGI KISAUKE. Akifafanua mpango huo wenye dhamira ya dhati ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Halmashauri kuboresha miundombinu ya elimu katika kikao cha wazazi kilichofanyika shuleni hapo, Kaimu Afisa Elimu msingi Bi Chitegetse Dominik amesema TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na teknolojia imefikia uamuzi huo baada ya kuridhishwa na juhudi za Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni katika azma yake ya ujenzi na uboreshaji wa vyumba 100,vya madarasa kwa kushirikiana na wadau pamoja na wananchi katika Wilaya yake. Amesema miundo mbinu ya shule ya msingi kiasuke haikuwa rafiki kwa mfumo mzima wa elimu, kwani changamoto kubwa ilikuwa ni upungufu wa vyumba vya madarasa, vyoo vya waalimu na wanafunzi, pamoja na ofisi ya waalimu. "Kutokana na adha hiyo imemlazimu mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Daniel Chongolo kuleta mradi wa kujenga vyumba sita vya madarasa, ofisi ndogo ya mwalimu mkuu ikiwa na choo chake pamoja na vyoo viwili vya walimu ili aweze kupunguza msongamano wa wanafunzi kwenye darasa Moja na kupunguza usumbufu wa wanafunzi kuvuka barabara mara kwa mara kwenda kusomea kwenye madarasa yaliyoazimwa toka shule ya sekondari ya jirani".Amefafanua Chitegetse. Naye Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bi. Pellagia Mdimi akitoa taarifa ya shule yake amesema inayo jumla ya wanafunzi 1886, ambapo wanaume ni 915 na wanawake ni 971 na kuainisha changamoto zilizopo kuwa ni msongamano wa wanafunzi kwenye madarasa, upungufu wa vyoo pamoja na ofisi ya waalimu. Kwa nyakati tofauti wazazi wa wanafunzi wanaosoma shule ya Msingi kisauke wamepongeza juhudi za Serikali pamoja na Mkuu wa wilaya ya Kinondoni kuona changamoto zilizopo mashuleni na kufikia hatua ya kuzifanyia kazi, ikiwa ni pamoja na kupunguza changamoto zilizokuwa zinawakabili watoto wao. Miradi hiyo inatarajiwa kufikia mwezi wa tisa iwe imekamilika ili wanafunzi pamoja na waalimu waweze kunufaika kwa kuwapatia elimu iliyobora na sio bora elimu. Imeandaliwana Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni TAMISEMI KWA KUSHIRIKIANA NA WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA YAUNGA MKONO JITIHADA ZA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU KINONDONI ... + Read more »