MARUFUKU KUKATA MITI BILA KIBALIPosted On: December 2nd, 2020Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Daniel Chongolo alipokuwa akiongea na wadau wa sekta binafsi katika Mkutano wa Baraza la Biashara lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa.Amesema ukataji miti kiholela ni hatari kwa uhai wa binadamu, lakini pia unapunguza uwezo wa ufyonzaji hewa ya ukaa unaopelekea athari za kiafya na kusababisha uharibifu wa mazingira, na kuwataka wahusika waache mara moja kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya yeyote atakayefanya hivyo.Amesema" Mti unakuwa wako unapoupanda, lakini ukishakuwa, sio wako, hivyo ni marufuku kukata miti bila kibali, lazima upate kibali Cha kufanya hivyo kwa Taasisi husika" Mhe. Daniel Chongolo.Amezitaka Taasisi, mashirika, mwananchi mmoja mmoja na sekta binafsi kuhakikisha zinapanda miti katika maeneo yao na kuilinda kwa kuitunza ili kuboresha mazingira lakini pia kuimarisha hewa Safi kwa ajili ya afya ya binadamu.Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wamiliki wa kumbi za burudani kuhakikisha wanazingatia sheria na misingi ya uendeshaji wa biashara zao kwa kutokuwa kero kwa wengine na kuwataka waache mara moja kupiga kelele za muziki kwani wasipotekeleza hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.Imeandaliwa naKitengo Cha Habari na Uhusiano.Manispaa ya Kinondoni. MARUFUKU KUKATA MITI BILA KIBALI Posted On: December 2nd, 2020 Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Daniel Chongolo al... + Read more »
KINONDONI YAZINDUA BARAZA LA BIASHARAPosted On: December 1st, 2020Akizindua Baraza hilo, Mwenyekiti wake ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo amesema hili ni jukwaa pekee linatoa nafasi ya kukutana na wadau wa sekta binafsi na kujadiliana fursa zakiuchumi ikiwa ni pamoja na utatuzi wa changamoto utakaoleta tija katika mustakabali wa nchi yetu inayosimamia sera ya uchumi wa kati wa viwanda.Ameongeza kuwa ni chombo kinachoweza kupaza sauti juu ya masuala yahusuyo sekta binafsi na wafanyabiashara kwa minajili ya maboresho yaliyokuwa makwazo katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.Amesema "Ni fursa Muhimu Kama wadau kwakuwa wote tunajenga nyumba moja, tunajenga mustakabali was Nchi yetu, tutakayoyaongea yakajenge Nchi yetu, Tumepata fursa Kama hii tunakwenda kutatua kero zote" Daniel Chongolo.Akiainisha majukumu ya kamati za baraza hilo la biashara katibu wake kwa niaba ya Mkurugenzi ambaye pia ni Mweka hazina wa Manispaa Ndg Maximilian Tabonwa amesema uundwaji wa Baraza hili ni sehemu ya majadiliano kati ya sekta binafsi na sekta ya Umma katika ngazi yaTaifa, Mkoa na Wilaya na kuainisha majukumu hayo kuwa ni kufanya tathmini, kuainisha njia ya utekelezaji wa maboresho, kupendekeza utaratibu wa mfumo, kujadili mahitaji ya rasilimali, kujadili ajenda za mikutano na kufuatilia maombi ya kamati tendaji.Akijibu changamoto iliyoainishwa na wadau kuhusiana na Tax clearance katika kuhuisha leseni za Biashara, Afisa Biashara wa Manispaa hiyo Ndg.Pastori Magodi amesema ni kwa mujibu wa vifungu vya Sheria vinavyomtaka mfanyabiashara au mtu yeyote anayehuisha leseni kulazimika kushirikiana na TRA, ili kupata taarifa za awali kuhusiana na leseni hiyo kwa maana ya kujua kama anadeni la nyuma au la.Naye Meneja TRA Mkoa wa Kinondoni Ndg Masawa Masatu alipokuwa akifafanua hoja iliyoelekezwa kwakwe kuhusiana na masuala ya ulipwaji wa kodi, amewataka wafanyabiashara kuwa makini na vishoka na kuhakikisha wanafuata Sheria zinazowapasa katika ulipwaji wa kodi.Baraza hilo lilipata uwakilishi kutoka Tan Trade, TCCIA, NAKIETE, TRA, Twiga Cement na wafanyabiashara wakubwa na wadogo ambapo walipata nafasi ya kuziainisha changamoto amabzo ni mkanganyiko wa Sheria za Biashara, mwingiliano wa Sheria na majukumu katika utekelezaji, kutokuwepo na uwazi katika taratibu za baadhi ya utekelezaji wa sera katika Biashara, ukiritimba katika kutekeleza Jambo pamoja na mazingira ya biashara kutokuwa rafiki.Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya ya Kinondoni amewataka wafanyabiashara wadogo kukuza kipato chao kwa kutumia njia sahihi ikiwemo uchukuaji wa mikopo isiyo na riba katika mkopo wa asilimia kumi kwa ajili ya wanawake, vijana na walemavu.Imeandaliwa naKitengo Cha Habari na UhusianoManispaa ya Kinondoni KINONDONI YAZINDUA BARAZA LA BIASHARA Posted On: December 1st, 2020 Akizindua Baraza hilo, Mwenyekiti wake ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya ... + Read more »
WAKAZI WA WAZO MJI MPYA WAPATIWA SULUHISHO LA BARABARAPosted On: November 27th, 2020Suluhisho hilo limekuja leo baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo kuzuru eneo lenye bwawa na kushauri kufunguliwa kwa barabara ya muda katika mazungumzo yaliyohusisha wananchi wa mji mpya, wamiliki wa viwanja vilivyopakana na bwawa pamoja na wadau wa maendeleo . Akizungumza na wakazi hao, Mhe. Chongolo amesema kufunguliwa kwa barabara ya muda kutawawezesha wakazi wa wazo mji mpya kufika majumbani kwao, lakini pia kutatoa nafasi ya eneo linalojaa maji kuboreshwa kwa kusambaza kifusi na kuchimba mitaro itakayoelekeza maji katika mkondo wake ili kuzuia athari za uharibifu wa barabara.Amesema " Kwanza tuondoe hatari iliyo mbele yetu, miti ing'olewe ili kuandaa eneo la barabara ya watu kupita ili waweze kufika katika makazi yao, kupatikane kifusi cha kujaza eneo kuyaelekeza maji kufuata mkondo wake, mana suala lililoko hapa ni makubaliano tu, baina ya mwenye kiwanja kilichopakana na bwawa kutoa eneo kwa muda ili waweze kusambaza kifusi kwa ajili ya kupata barabara ya muda, wakati tukiendelea kupata suluhisho la kudumu. jukumu langu ni kuhakikisha wananchi wanapata Amani katika makazi yao" Amesema Chongolo.Aidha amemtaka Bw.Gerald Lusula Mwenye kiwanja Na.392 na Bwana Andrew Peter Mwenye kiwanja namba 393 vyote vikiwa vimepakana na eneo lenye bwawa kutoa ushirikiano katika kuhakikisha suluhu ya pamoja inapatikana kwa kuruhusu kusambazwa kifusi kwenye ukingo wa viwanja ili kupatikana kwa barabara ya muda kwa wakazi wa mji mpya kufika majumbani kwao huku wakiangalia suluhu ya kudumu ya eneo hilo.Katika hatua nyingine ameiagiza kampuni ya Mecco inayojenga barabara ya wazo kutumia scaveta pamoja na greda kusambaza kifusi kitakachotolewa na kiwanda cha wazo ikiwa ni pamoja na mifuko 20 ya cement pamoja na kalvati kwa ajili ya kuboreshwa eneo hilo la bwawa.Awali akiainisha changamoto ya eneo hilo Mhandisi wa Tanroad Bi.Mariam Hassan amesema ni kutokana na kuzuiwa kwa mkondo huo wa maji hali iliyopelekea kutuama na kusababisha bwawa linaloendelea kukua na kuharibu barabara.Imeandaliwa naKitengo Cha Uhusiano na HabariManispaa ya Kinondoni. WAKAZI WA WAZO MJI MPYA WAPATIWA SULUHISHO LA BARABARA Posted On: November 27th, 2020 Suluhisho hilo limekuja leo baada ya Mkuu wa Wilaya ... + Read more »