MARUFUKU KUKATA MITI BILA KIBALI
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Daniel Chongolo alipokuwa akiongea na wadau wa sekta binafsi katika Mkutano wa Baraza la Biashara lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa.
Amesema ukataji miti kiholela ni hatari kwa uhai wa binadamu, lakini pia unapunguza uwezo wa ufyonzaji hewa ya ukaa unaopelekea athari za kiafya na kusababisha uharibifu wa mazingira, na kuwataka wahusika waache mara moja kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya yeyote atakayefanya hivyo.
Amesema" Mti unakuwa wako unapoupanda, lakini ukishakuwa, sio wako, hivyo ni marufuku kukata miti bila kibali, lazima upate kibali Cha kufanya hivyo kwa Taasisi husika" Mhe. Daniel Chongolo.
Amezitaka Taasisi, mashirika, mwananchi mmoja mmoja na sekta binafsi kuhakikisha zinapanda miti katika maeneo yao na kuilinda kwa kuitunza ili kuboresha mazingira lakini pia kuimarisha hewa Safi kwa ajili ya afya ya binadamu.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wamiliki wa kumbi za burudani kuhakikisha wanazingatia sheria na misingi ya uendeshaji wa biashara zao kwa kutokuwa kero kwa wengine na kuwataka waache mara moja kupiga kelele za muziki kwani wasipotekeleza hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano.
Manispaa ya Kinondoni.
0 comments:
Post a Comment