Top ad

Top ad

 

BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LAANZA KAZI RASMI

Posted On: December 7th, 2020

Baraza hilo chini ya Mstahiki Meya wake Mhe.Songoro Mnyonge limeanza kazi kwa kupitisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Halmashauri katika kipindi cha kuanzia Julai hadi Octoba 2020.

Akitoa hoja ya kupitisha na kuungwa mkono kwa taarifa hiyo ya utekelezaji kwa Baraza la madiwani Meya Songoro amesema taarifa hiyo ni kielelezo tosha cha majukumu yanayompasa kila diwani kwenye kata yake kuhakikisha anayasimamia na  kuyatekeleza kwa maslahi mapana ya wananchi.

"Waheshimiwa madiwani niwahakikishie Jambo moja, kipindi kilichopita tulifanya kazi kubwa Sana, kwahiyo awamu hii pia tutaendelea pale ambapo tuliishia, kunamiradi mikubwa ambayo inaendelea hivi Sasa, tumeingia rasmi kufanya kazi" Mhe. Songoro Mnyonge.

Awali akiisoma taarifa hiyo ya utekelezaji kwa Baraza la Madiwani, Katibu wa Baraza hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Ndg Aron Kagurumjuli amesema taarifa hii ni ya utekelezaji wa shughuli za Halmashauri zilizofanywa kipindi ambacho baraza hilo halikuwepo.

Ameongeza kuwa mara baada ya kuvunjwa kwa Baraza la Madiwani Julai mwaka huu, Halmashauri iliendelea na utekelezaji wa mpango wa bajeti ya mwaka 2020/2021 na hivyo kufanikisha shughuli mbalimbali za maendeleo hususani katika miradi mikubwa na ya kimkakati.

“ Waheshimiwa madiwani, taarifa hii imeeleza namna ambavyo miradi imefanikiwa na vitu ambavyo vimefanyika katika kipindi ambacho hamkuwepo, kikubwa ni kwamba tumefanya mambo makubwa na hivyo  tunawaahidi kushirikiana kwa pamoja kuyaendeleza yale ambayo yamefanyika” amesema Kagurumjuli.

Katika hatua nyingine Baraza hilo lenye madiwani 30 limeteua wenyeviti na wajumbe wa  kamati za kudumu  ambazo ni kamati ya huduma za uchumi afya na elimu, kamati ya fedha na uongozi, kamati ya Mipangomiji na Mazingira, Kamati ya maadili na kamati ya UKIMWI.

 Imeandaliwa na

Kitengo cha Habari na Mahusiano

Manispaa ya Kinondoni.

0 comments:

Post a Comment

 
Top