KINONDONI YAINGIA MKATABA NA KAMPUNI MBILI UJENZI WA BARABARA, BILIONI 34.2 KUTUMIKA. Posted On: March 10th, 2020 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni leo imesaini mkataba na Kampuni mbili za China kwa ajili ya ujenzi wa mradi mkubwa wa barabara zenye urefu wa kilomita 12 ambapo jumla ya kiasi cha Tsh. Bil. 34.2 zitatumika kwenye mradi huo. Kampuni ambazo Manispaa ya Kinondoni imeingia mkataba wa ujenzi huo mara baada ya kutangazwa tenda ni Stecol Corporation pamoja na China Ralway Seventh Group Limited. Mkataba huo umesainiwa na Mstahiki Meya Mhe. Benjamini Sitta, na kushuhudiwa na Kaimu Mkurugenzi Dk. Patricia Henjewele pamoja na Kaimu Mhandisi wa Manispaa Mkelewe Tungaraza. Akizungumza mara baada ya hafla ya utiwaji wa saini wa mkataba wa mradi huo, Meya Sitta amefafanua kuwa ujenzi huo utahusisha barabara ya Magomeni mapipa hadi urafiki ambayo inaurefu wa zaidi ya kilomita saba (7), Makumbusho, Mwanamboka, na barabara ya Muhimbili ambazo zinaurefu wa zaidi ya kilomita tano (5). Aidha Meya Sitta ameeleza kuwa ujenzi wa barabara ya Magomeni Mapipa na Urafiki inajengwa na Kampuni ya Stecol Corporation kwa gharama ya Tsh. Bil. 18.7 huku barabara ya Makumbusho, Mwanamboka na Muhimbili ikijengwa na Kampuni ya China Ralway Seventh Group Limited kwa gaharama ya Tsh. Bil.15.5. Mhe. Sitta amemshukuru Mkurugenzi Aron Kagurumjuli kwa kuhakikisha barabara hizo zinajengwa na kwamba maendeleo ambayo yanafanyika katika Manispaa hiyo yanatokana na juhudi kubwa ya utendaji kazi wake. “ Nampongeza Mkurugenzi wetu, anafanya kazi kubwa leo hii tunakwenda kuleta maendeleo makubwa ya barabara katika Manispaa yetu, hivyo mradi huu utakuwa sehemu ya kutatua changamoto zilizopo katika Halmashauri yetu” amesema Meya Sitta. “ Leo ni siku ya kihistoria katika Manispaa yetu, tumesaini mikataba mikubwa miwili kutoka kampuni mbili tofauti , mikataba hii nisehemu kubwa ya mradi wa DMDP, ambao unakwenda kutatua changamoto ya barabara kwenye Halmashauri yetu , hivyo ninampongeza sana Mkurugenzi wetu Kagurumjuli” amesema Meya Sitta. Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa DMDP ambaye pia ni Kaimu Mhandisi wa Manispaa, Mkelewe Tungaraza amesema kuwa mradi huo utaanza Aprili mwaka huu na unatarajiwa kukamilika kwa muda wa miezi 15. Imeandaliwa na Kitengo Cha habari na Mahusiano Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YAINGIA MKATABA NA KAMPUNI MBILI UJENZI WA BARABARA, BILIONI 34.2 KUTUMIKA. Posted On: March 10th, 2020 Halmashauri ya Manisp... + Read more »
KINONDONI YA ADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI Posted On: March 9th, 2020 Shehere ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yamefanyika leo katika viwanja vya Lidas ambapo kimkoa mwenyeji na muandaaji wa ma adhimisho hayo ni Wilaya ya Kinondoni. Katika ma adhimisho hayo, mgeni rasmi ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Poul Makonda ambapo alisindikizwa na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Daniel Chongo, Katibu Tawala Bi. Stella Msofe , Kaimu Mkurugenzi Dk. Patricia Henjewele, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya jamii pamoja na watumishi wanawake wa Halmashauri hiyo. Aidha Mhe. Makonda aliambatana na wageni wengine ambao ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Dk. Sophia Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sarah Msafiri na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Bi. Sipora Liana. Madhimisho hayo yalibeba ujumbe ulioeleza kuwa KIZAZI CHA USAWA KWA MAENDELEO YA TANZANIA YA SASA NA YA BAADAE. Imeandaliwa na kitengo cha Habari na Uhusiano Halmashauri ya manispaa ya Kinondoni KINONDONI YA ADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI Posted On: March 9th, 2020 Shehere ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yamefan... + Read more »