KINONDONI YA ADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
Posted On: March 9th, 2020
Shehere ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yamefanyika leo katika viwanja vya Lidas ambapo kimkoa mwenyeji na muandaaji wa ma adhimisho hayo ni Wilaya ya Kinondoni.
Katika ma adhimisho hayo, mgeni rasmi ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Poul Makonda ambapo alisindikizwa na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Daniel Chongo, Katibu Tawala Bi. Stella Msofe , Kaimu Mkurugenzi Dk. Patricia Henjewele, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya jamii pamoja na watumishi wanawake wa Halmashauri hiyo.
Aidha Mhe. Makonda aliambatana na wageni wengine ambao ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Dk. Sophia Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sarah Msafiri na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Bi. Sipora Liana.
Madhimisho hayo yalibeba ujumbe ulioeleza kuwa KIZAZI CHA USAWA KWA MAENDELEO YA TANZANIA YA SASA NA YA BAADAE.
Imeandaliwa na kitengo cha Habari na Uhusiano
Halmashauri ya manispaa ya Kinondoni
0 comments:
Post a Comment