BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LAPITISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEOPosted On: January 7th, 2021Baraza hilo chini ya Mwenyekiti wake Mhe.Songoro Mnyonge limeipitisha taarifa hiyo ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo robo ya kwanza Julai hadi Septemba 2020/2021 katika kikao cha baraza kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa.Akipitisha taarifa hiyo Mhe.Songoro amesema taarifa hii ya utekelezaji ni ile ya bajeti inayomalizika miezi michache ijayo hivyo imetekelezwa kwa kiwango cha kuridhisha na kuwataka Madiwani kuorodhesha mahitaji yao katika bajeti ijayo ya 2021/2122."Mimi niwashauri Wahe.Madiwani bajeti tunayotekeleza sasa tumeikuta, imebakiza miezi michache, lakini mchakato wa kuandaa bajeti ijayo tayari umeshaanza katika ngazi ya Halmashauri, hivyo niwaombe Wahe.madiwani twende tukapitie mipango yetu ili tuiingize kwenye mpango wa bajeti" Amesema Mstahiki.Akiwasilisha taarifa hiyo ya utekelezaji katika kikao cha Baraza hilo Katibu wa kikao hiko ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Ndg Aron Kagurumjuli amesema kwa mwaka wa fedha 2020/2021 Manispaa ilipanga kutumia jumla ya shilingi takribani Bilioni 30.5 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.Amesema fedha hizo zimetokana na vyanzo mbalimbali na kuvitaja kuwa ni mapato ya ndani ya Halmashauri, ruzuku kutoka Serikali kuu pamoja na nguvu ya jamii.Katika kikao hicho cha baraza Wahe.Madiwani ambao ni wenyeviti wa kamati za kudumu pia walipata fursa ya kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa shughuli za kamati zao.Taarifa zilizowasilishwa katika baraza hilo ni za kamati za kudumu robo ya kwanza Julai hadi Septemba 2020/2021 ambazo ni taarifa za huduma za Uchumi afya na Elimu, taarifa za kamati ya mipangomiji na mazingira, taarifa za kamati ya kidhibiti UKIMWI, taarifa za Kamati ya maadili na taarifa za Kamati ya fedha na Uongozi.Imeandaliwa na:Kitengo Cha Habari na Uhusiano.Manispaa ya Kinondoni. BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LAPITISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO Posted On: January 7th, 2021 Baraza hilo chini ya Mwe... + Read more »
NI KINONDONI TENA UFAULU WA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2020 MKOA WA DAR ES SALAAMPosted On: December 24th, 2020Manispaa ya Kinondoni imeshika nafasi ya kwanza kimkoa na ya pili Kitaifa kwa ufaulu wa asilimia 98.1 matokeo ya darasa la Saba kwa mwaka 2020.Hayo yamebainishwa na Mstahiki Meya Manispaa ya Kinondoni Mhe Songoro Mnyonge alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari kwa lengo la kuelezea mikakati ya Halmashauri katika kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu wanaingia kidato cha kwanza kwa mwaka 2021.Mhe.Songoro mesema "Kinondoni imeendelea kuongoza katika matokeo yaliyotangazwa, ambapo 13,401 walifanya mtihani wa darasa la Saba mwaka huu na 13,159 wamefaulu na kupelekea ufaulu huo kufikia asilimia 98.1 na kwa ufaulu huo, umeufanya Manispaa ya Kinondoni kuwa ni nafasi ya kwanza Kimkoa na kuwa ya pili Kitaifa, haya ni mafanikio makubwa" Amesema Mstahiki Meya.Ameongeza kuwa kwa wanafunzi 775 wanaosubiri chaguo la pili, Manispaa ya Kinondoni tayari Imekwishajipanga kuhakikisha inakabiliana na changamoto hizo za uhaba wa madarasa zinazopelekea wanafunzi hao kusubiri kwa kujenga vyumba 64 vitakavyoweza kupunguza adha hiyo kwa kiasi kikubwa mara vitakapokamilika.Ameainisha mchanganuo wa ujenzi pamoja na ukarabati wa vyumba hivyo vya madarasa kuwa ni ujenzi wa vyumba vya madarasa 10 sekondari ya kijitonyama, ukaratabati wa vyumba 7 shule ya Sekondari Magomeni, ujenzi wa madarasa 6 shule ya sekondari ya Benaco na ujenzi was madarasa 6 sekondari ya mzimuni.Mchanganuo mwingine ni ujenzi madarasa 6 shule ya Sekondari Mbezi juu, ujenzi wa madarasa 8 shule ya Bunju tarimo, ujenzi wa madarasa 8 Boko mtambani, ujenzi wa madarasa 5 shule ya sekondari kondo, ujenzi wa madarasa 6 shule ya sekondari Oysterbay pamoja na ujenzi wa shule mpya ya miti mirefu.Aidha amefafanua kuwa ujenzi wa vyumba vya madarasa unaenda sambamba na ujenzi wa hostel itakayoweza kuchukua wanafunzi 320, pamoja na madawati 6000 ambapo kiasi cha tsh milioni180 na laki 5 zimetengwa kwa ajili ya utengenezaji wa madawati hayo ambapo madawati 3210 yamekamilika.Mhe songoro ameeleza kuwa matarajio ya Manispaa ni kuhakikisha ifikapo mwezi wa pili 2021, ujenzi pamoja na ukarabati wa vyumba vya madarasa 64, yawe yameshakamilika tayari kupokea wanafunzi.Jumla ya wanafunzi 13401 walifanya mtihani wa darasa la Saba mwaka huu ambapo wanafunzi 13,159 wamefaulu na 12,384 wameshapata nafasi za kujiunga na kidato cha kwanza na kupelekea wanafunzi 775 kusubiri chaguo la pili.ImeandaliwanaKitengo cha Habari na UhusianoManispaa ya Kinondoni NI KINONDONI TENA UFAULU WA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2020 MKOA WA DAR ES SALAAM Posted On: December 24th, 2020 Manispaa ya Kinondoni imes... + Read more »
NAIBU WAZIRI-OFISI YA WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA NAMNA KINONDONI INAVYOWEZESHA WANANCHI KIUCHUMIPosted On: December 22nd, 2020Hali hiyo imebainika wakati Naibu waziri wa Ajira, Kazi na Vijana Mhe Patrobas Katambi alipofanya ziara kutembelea vikundi vya vijana vilivyokopeshwa vitendea kazi vinavyowasaidia katika shughuli zao za ujasiriamali.Amesema kwa kumpatia kijana kifaa ni uamuzi mzuri unaomwepusha kutumia fedha kinyume na utaratibu na kumuondolea tamaa za matumizi mabovu hali inayompelekea kutokukamilisha malengo mahususi"Niwapongeze pia kwa ajili ya eneo hili la utoaji mikopo, Kinondoni mmeweza kwa kuhakikisha mnasimamia taratibu, Sheria, kanuni na miongozo invyoelekeza kuhusiana na suala hili ngazi kwa ngazi kwani mchakato unaanzia ngazi ya chini hali inayopelekea kupata watu sahihi zaidi wa kuwapatia fedha hizi" Ameongeza Mhe KatambiAkiwa Katika kiwanda cha kutengeneza bidhaa za ngozi cha EZEMA, Naibu waziri huyo ameridhishwa na bidhaa zinazozalishwa kiwandani hapo na kuahidi kuwa balozi wa bidhaa hizo popote atakapokwenda.Aidha amewataka vijana wa kiume kujitokeza kwa wingi kutumia fursa hii kwani takwimu za Sasa zinaonesha kuwa idadi ya wanawake wanaojitokeza kuchukua mikopo ni kubwa zaidi ukilinganisha na vijana.Awali akitoa Taarifa ya utoaji wa mikopo kwa wanawake, vijana na walemavu, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Kinondoni, Bi Halima Kahema amesema wameamua sasa kukopesha vifaa, na viwanda vidogo ili kuwawezesha wajasiriamali kwenda moja kwa moja kwenye uzalishaji.Kadhalika amebainisha kuwa kwa mwaka 2017 wamefanikiwa kukopesha zaidi ya vikundi 5000 na kuwa kwa mwaka huu wa fedha wameshatoa mikopo kwa vikundi 202 ambapo wamepata kiasi cha shilingi Bil 1.3 .Naibu waziri akiwa amembatana na Kamishna wa Kazi nchini ametembelea kikundi cha kutengeneza juisi cha Emitote na kikundi cha kuzalisha bidhaa za ngozi cha EZEMA.Imeandaliwa naKitengo cha Habari na UhusianoManispaa ya Kinondoni NAIBU WAZIRI-OFISI YA WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA NAMNA KINONDONI INAVYOWEZESHA WANANCHI KIUCHUMI Posted On: December 22nd, 2020 Hali hiyo i... + Read more »
HOSPITALI YA SANITAS YAPEWA SIKU SABA KUKAMILISHA MALIMBIKIZO YA MISHAHARA YA WATUMISHI WAKEPosted On: December 22nd, 2020Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri Wizara ya Kazi, Ajira na Vijana Mhe.Patrobas Katambi mara baada ya kuzuru ofisini hapo kwa lengo la kujiridhisha na masuala ya kisera yanayohusiana na ajira, kazi na vijana.Akiwa ofisini hapo, Naibu waziri amebaini watumishi wa Hospitali hiyo kutokupatiwa stahiki zao za kiutumishi ikiwemo mishahara yao kwa kipindi cha miezi 13 sasa kwa kigezo cha kuyumba Biashara kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa corona.Mhe Katambi amesema kulipa mishahara watumishi ni takwa la kikatiba na haliwezi kuvunjwa kwa kigezo chochote kile, hasa ikizingatiwa kaulimbiu ya wizara kwa awamu hii ni "mtumishi alipwe ujira wake kabla jasho halijakauka" lengo likiwa kuhakikisha kwamba mfanyakazi mtanzania anapata haki yake kwa wakati na kulinda ajira za wazawa."Watumishi Hawa wanamahitaji binafsi, wanafamilia zinawategemea na wanatakiwa kulipa Kodi za serikali kupitia mishahara yao, kitendo cha ninyi kutowapa mishahara yao kipindi chote hiki sio tuu kuwakoseshea mahitaji yao ya msingi bali mnakwamisha pia Kodi za serikali" AmeongezaNaibu WaziriAidha Naibu Waziri huyo ameutaka uongozi wa Sanitas kuwapa mikataba isio na ukomo watumishi wanaostahili mikataba hiyo, kuwe na vyama vya wafanyakazi, kuwasilisha nyaraka zinazohusu umiliki wa kampuni ili ziweze kupitiwa upya pia Uongozi uwe na sera mbalimbali hususan ya ajira na ukimwi Ili ziweze kufuatwa kikamilifu katika majukumu ya kiutawala.Kwa upande wake kamishna wa Ajira Nchini Tanzania Brigedia Mbindi amesema ziara hii ni endelevu kwa nchi nzima lengo likiwa ni kuhakikisha sheria na miongozo mbalimbali ya kazi inafuatwa kikamilifu na wafanyakazi wanafanya kazi katika mazingira bora.Naye Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Daniel Chongolo amesema Kinondoni inaendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili waajiriwa wa sekta binafsi hivyo kwa ziara hii kutapunguza changamoto kwa waajiriwa na kuwapa mazingira mazuri wawekezaji katika kutimiza majukumu yao.Katika hatua nyingine Naibu Waziri amepongeza uongozi wa kiwanda cha coca-cola kwanza kwa kufuata kikamilifu sheria za kazi hususan Katika kuwapa kipaumbele wafanyakazi wazawa na kuwapatia mafunzo wazawa Katika yale maeneo ya utaalamu.Katika ziara hiyo, Naibu Waziri ametembelea Hospitali ya Sanitas iliyopo Mikocheni na Kiwanda cha coca-cola kwanza.Imeandaliwa naKitengo cha Habari na UhusianoManispaa ya Kinondoni. HOSPITALI YA SANITAS YAPEWA SIKU SABA KUKAMILISHA MALIMBIKIZO YA MISHAHARA YA WATUMISHI WAKE Posted On: December 22nd, 2020 Agizo hilo lim... + Read more »
MATUKIO KATIKA PICHAPosted On: December 17th, 2020Kamati ya Fedha na Uongozi chini ya Mwenyekiti wake Mstahiki Meya Mhe.Songoro Mnyonge ambaye pia ni diwani wa Kata ya Mwananyamala leo wamefanya ziara ya ukaguzi wa Miradi.Kamati hiyo imefanikiwa kutembelea miradi ambayo vyanzo vyake ni mapato ya ndani pamoja na ruzuku kutoka Serikali kuu.Miradi iliyotembelewa ni ujenzi wa jengo la utawala lililoko katika kata ya Ndugumbi, ujenzi wa uwanja wa mpira wa kisasa Mwenge, na ujenzi wa stendi ya kisasa ya daladala inayojengwa kwa fedha za ndani na Ile inayojengwa kwa fedha za ruzuku kutoka Serikali kuu ni ujenzi wa soko la Kisasa Magomeni na Tandale.Imeandaliwa naKitengo Cha Habari na Uhusiano .Manispaa ya Kinondoni. MATUKIO KATIKA PICHA Posted On: December 17th, 2020 Kamati ya Fedha na Uongozi chini ya Mwenyekiti wake Mstahiki Meya Mhe.Songoro Mnyonge ... + Read more »