KINONDONI YAPONGEZWA KWA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2015-2020, KWA VITENDOPosted On: June 19th, 2020Pongezi hizo zimetolewa na Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni kwenye kikao cha majumuisho baada ya ziara ya siku mbili ya ukaguzi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo.Akizitoa pongezi hizo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya kinondoni Ndg Arold Maruma amesema Kinondoni imeonesha uzalendo katika kuhakikisha ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015 hadi 2020, inatekelezwa kwa vitendo kwa kutumia makusanyo yao ya Ndani, Fedha kutoka Serikli kuu pamoja na Fedha kutoka kwa wadau wa maendeleo. "Kinondoni kwakweli mmeitendea haki ilani ya uchaguzi ya CCM kwa mwaka 2015-2020, miradi mliotekeleza hapa ni mfano wa kuigwa na mmeacha taswira inayoonekana kwa Wananchi." Ameongeza Mwenyekiti.Aidha amebainisha kuwa thamani halisi ya fedha imeonekana Katika miradi hiyo kwani mbali na kutumia fedha za ndani, Serikali kuu na wadau, lakini pia kiasi kilichotumika katika ukamilishaji wake vinaenda sambamba na ubora .Awali akikabidhi ripoti ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa Mwenyekiti wa CCM, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo amesema Kinondoni imeweza kufanikiwa kukamilisha miradi hiyo kutokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya ofisi yake, Ofisi ya Mkurugenzi na Mstahiki Meya.Ameongeza kuwa viongozi hawa wa Manispaa na timu zao wamekuwa na lengo moja la kuiletea Halmashauri hii maendeleo kwa kuwapatia na kusimamia vyema miradi ambayo inakwenda kumaliza changamoto mbalimbali za Wananchi.Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndugu Aron Kagurumjuli amesema kuwa Halmashauri imekuwa na utaratibu wa kutenga asilimia 60 ya mapato yake ya ndani na kuipeleka kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo na asilimia 40 inayobaki kutumika katika matumizi mengine ya kuendesha Halmashauri.Miradi iliyotembelewa na kamati hiyo ni pamoja na ujenzi wa Jengo la Utawala la Halmashauri, Ujenzi wa soko la kisasa la magomeni, Ujenzi wa kituo Cha afya Cha kigogo, Ujenzi wa barabara ya akachube, Ujenzi wa zahanati ya Magomeni, zahanati ya Makumbusho , Ujenzi wa uwanja wa mpira wa kisasa uliopo mwenge na Ujenzi wa stendi ya kisasa ya daladala.Mingine ni ujenzi wa Kiwanda Cha kuchakata taka na kutengeneza mbolea mboji kilichopo mabwepande, Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya iliyopo Mabwepande, Shule ya sekondari ya wasichana ya kidato Cha tano na sita Mabwe Tumaini girls, Upanuzi wa kituo cha afya Bunju na Ujenzi wa shule ya Msingi Mkoani.Imeandaliwa naKitengo Cha habari na UhusianoManispaa ya kinondoni. KINONDONI YAPONGEZWA KWA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2015-2020, KWA VITENDO Posted On: June 19th, 2020 Pongezi hizo zimetolewa n... + Read more »
KINONDONI KUTEMBELEWA NA RC MAKONDA UKAGUZI MIRADI YA MAENDELEOPosted On: June 18th, 2020Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda anatarajiwa kufanya ziara ya siku mbili katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni yenye majimbo mawili, kuanzia Juni 20 hadi 21 mwaka huu itakayohusisha ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayoenda sambamba na utekelezaji wa Ilani ya UchaguziAkizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo amesema kuwa miradi hiyo ni ile iliyotekelezwa kwa kipindi cha Miaka mitano ya Uongozi wa Rais Mhe. Dkt John Pombe Joseph Magufuli, ambayo imetekelezwa kwa fedha ambazo ni vyanzo mbalimbli ikiwemo mapato ya ndani, Serikali Kuu na Wadau.Amesema kwa kufanya hivyo ni kuonesha uzalendo hasa ikizingatiwa miradi hiyo imetekeleza kwa kiwango kilichokusudiwa na kukamilika kwa ubora na wakati uliopangwa.“Miradi hii ambayo Manispaa imetekeleza nikutokana na dhamana ambayo CCM imetupatia na hivi sasa tunakwenda kukiabidhi ,nasio hii tu ambayo tumeitaja , Manispaa ya Kinondoni inamiradi mingi mikubwa ambayo imefanyika ila hii tumeichagua kama alama ya uwasilishwaji wa majukumu yetu” amesema Mhe.Chongolo.Ameitaja miradi ambayo itatembelewa kwa Jimbo la Kawe kuwa ni umaliziaji wa Hospitali ya Wilaya iliyopo Mabwepande, jengo la Mama na Mtoto RCH, nyumba ya watumishi wa Hospitali hiyo, Shule ya Sekondari ya wasichana Tumaini, Kiwanda cha kuchakata taka kilichopo Mabwepande, Kituo cha Afya Bunju, ujenzi wa mantaki matano ya maji yenye ujazo wa mita milioni saba pamoja na Zahanati ya Mikoroshini. Kwa upande wa Jimbo la Kinondoni Miradi itakayotembelewa ni ujenzi wa Kiwanja cha kisasa cha mpira kilichopo Mwenge, Kituo cha daladala Mwenge, Soko la Sinza Africasana, ujenzi wa Barabara ya Moroco mwenge yenye urefu wa kilomita 4.2, Hospitali ya Mwananyamala jengo la Mama na Mtoto, Kituo cha Afya cha Kisasa Kigogo kilichojengwa kwa ghorofa tano, shule ya Sekondari Mzimuni kwa ngazi ya Ghorofa mbili pamoja na Soko la Kisasa Magomeni.Katika hatua nyingine , Mkuu huyo wa Wilaya Kinondoni amesema kuwa Manispaa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeweza kuboresha miundombinu ya sekta muhimu za Afya pembezoni mwa mji iliyopeleke wananchi kupata huduma za afya kwa urahisi, na ile ya elimu kwa wenye uhitaji maalumu hali iliyofanikisha makundi haya maalumu kupata huduma stahiki.Imeandaliwa naKitengo cha Habari na UhusianoManispaa ya Kinondoni. KINONDONI KUTEMBELEWA NA RC MAKONDA UKAGUZI MIRADI YA MAENDELEO Posted On: June 18th, 2020 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda ... + Read more »