KAMATI YA SIASA YA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA KINONDONI YAMPONGEZA MKURUGENZI KAGURUMJULI KWA KUTEKELEZA KIKAMILIFU ILANI YA CCM 2015 /2020 Posted On: December 12th, 2019 Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kinondoni jana imefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi sita iliyopo katika Kata tano kati ya kata 20 zilizopo katika Halmashauri hiyo. Ziara hiyo ambayo ilikuwa ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya Harlod Maruma, ilihusisha viongozi wengine akiwemo Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Daniel Chongolo, Mstahiki Meya Benjamini Sita, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Dk. Patricia Henjewele, Mbunge wa jimbo hilo Maulid Mtulia, watendaji pamoja na wakuu wa Idara mbalimbali. Aidha kamati hiyo ilitembelea mradi wa Kituo Cha Afya Cha Kigogo kinachojengwa kwa shingili milioni 700 ambapo kati ya fedha hizo shilingi milioni 400 ni pesa kutoka Serikali kuu, shilingi milioni 300 ni pesa zinazotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri. Kamati hiyo ilitembelea mradi mkubwa wa Soko la Kisasa la Magomeni linalojengwa kwa shilingi Bilioni 8.9 ambapo kamati hiyo ilieleza kuwa imeridhishwa na hatua ya soko hilo ilipofikia kwa sasa na hivyo kutumia nafasi hiyo kumpongeza Mkurugenzi Ndugu. Aron Kagurumjuli na watendaji wake. Kamati hiyo pia ilitembelea mradi wa ujenzi wa vyumba sita vya madarasa ya ghorofa shule ya Sekondari Mzimuni, ambapo Mkuu wa shule hiyo , Yahaya Kirondo alisema kuwa kulingana na kasi ya ujenzi unavyo endelea hadi kufikia Januari 2020 wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule hiyo wataanza kutumia madarasa hayo. Aidha kamati hiyo ilitembelea ujenzi wa Zahanati ya Magomeni, Makumbusho ambapo kwa mujibu wa mkandarasi mshauri anayesimamia ujenzi wa Zahanati hizo, alisema kuwa hadi kufikia Aprili 2020 zitakuwa zimekamilika na hivyo wananchi kuanza kupata huduma. Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Daniel Chongolo aliieleza kamati hiyo kuwa, kumalizika kwa Zahanati hizo kutasaidia kuwa rahisishia wananchi kupata huduma za karibu katika Zahanati hizo badala ya kwenda moja kwa moja katika Kituo Cha Afya cha Magomeni au Hospital ya Rufaa ya Mwananyamala. Mhe. Chongolo alisema kuwa, Zahanati hizo pia zitakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Magomeni na maeneo mengine kwa kuwa eneo hilo linawakazi wengi na kwamba ha kukuwa na Zahanati zaidi ya Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala na Kituo cha Afya Cha Magomeni. Miradi mingine iliyotembelewa na kamati hiyo ni ujenzi wa barabara zinazo simamiwa na DMDP ambazo ni Shekilango yenye urefu wa kilomita 3.7, Barabara ya Akachube yenye urefu wa kilomita 0.94, barabaa ya TRA yenye urefu wa kilomia 1.1, barabara ya Sinza Mori yenye urefu wa kilomita 0.93 na Igesa yenye urefu wa kilomita 0.64. Imetolewa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. KAMATI YA SIASA YA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA KINONDONI YAMPONGEZA MKURUGENZI KAGURUMJULI KWA KUTEKELEZA KIKAMILIFU ILANI YA CCM 2015 /2... + Read more »
KINONDONI YAPOKEA VIFAA VYA HOSPITALI KUTOKA VYAMA VYA USHIRIKA Posted On: December 14th, 2019 Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Benjamini Sita amevipongeza vyama vya ushirika vilivyopo katika Halmashauri hiyo kwa kujitolea vifaa vya Hospitali katika Kituo Cha Afya cha Kigogo. Aidha vyama hivyo vimemkabidhi Mhe. Sita Magodoro 30, mashuka na foronya 150 ambapo wamesema kuwa vitasaidia wagonjwa watakaokuwa wanapatiwa matibabu katika kituo hicho. Akizungumza na vyama hivyo kabla ya kukabidhiwa vifaa hivyo, Meya Sita amesema kuwa vitasaidia kuwahudumia wananchi mbalimbali watakao kuwa wanapatiwa huduma katika Kituo hicho cha Afya na kuwasihi wengine kujitokeze kuchangia. Amefafanua kuwa suala la Afya ni pana na kwamba Halmashauri iliamua kujenga Kituo hicho cha Afya ili kuwezesha wananchi kupata huduma kwa haraka na urahisi kutoka maeneo mbalimbali. Ameeleza kuwa, Halmashauri ya Kinondoni inahudumia watu kutoka sehemu mbalimbali ikiwemo Bagamoyo, na kwamba kulingana na wingi huo, imeweza kununua eneo hilo na kujenga Kituo hicho cha Afya na kwamba watu kutoka shemu mbalimbali watapata huduma safi na bora inayokidhi viwango. Ameongeza kuwa” Tumepambana usiku na mchana, na mpongeza sana Mkurugenzi wetu , Ndugu Aron Kagurumjuli na watendaji wote kwa kufanikisha ujenzi wa Kituo hichi cha Afya, ambacho kitahudumia watu sio Kigogo tu , bali kitatoa huduma Ilala, Ubungo, na maeneo mengine kama ilivyo kwa Kituo cha Afya cha Magomeni.” amesema Meya Sita. Hata hivyo Mhe. Sita emesema “ ninawapongeza sana, ninaimani wadau wengine watakapo ona hivi, itawakumbusha kuona kwamba wanawajibu kufanya hivi kama walivyofanya hawa vyama vya ushirika kutambua umuhimu wa afya katika Halmashauri yetu” ameongeza. Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Kilimo, Umwagiliaji, na Ushirika , Ndugu. Salehe Hija amekipongeza kitengo cha ushirika kwa kuandaa vifaa hivyo na kukabidhi katika Kituo hicho cha Afya na kusema kuwa kitendo hicho kitaonyesha njia kwa watu wengine kujitolea. Aidha Hija amesema kuwa vifaa hivyo vilivyotolewa vinathamani ya shilingi milioni 6.7 huku kituo hicho kikiwa na uhitaji wa vitanda 150 ambapo kwa mujibu wa mganga mfawidhi wa Kituo hicho , magodoro hayo yaliyotolewa ni ni sawa na asilimia 20 ya mahitaji hayo. Imetolewa na Kitengo cha Habari na Uhusiano manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YAPOKEA VIFAA VYA HOSPITALI KUTOKA VYAMA VYA USHIRIKA Posted On: December 14th, 2019 Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa... + Read more »
KINONDONI YAZINDUA MAONESHO YA BIDHAA ZA NGOZI VIWANJA VYA TANGANYIKA PACKERS, YAWEKA MKAKATI WA SOKO LA UHAKIKA Posted On: December 12th, 2019 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo amesema kuwa katika kutatua changamoto ya kupata soko la uhakika la bidhaa za ngozi, Wilaya hiyo imejipanga kuwatafutia maeneo wazalishaji wa ndani ambapo wote watakaa sehemu moja kwa ajili ya uzalishaji na uuzaji wa bidhaa hizo. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa maonesho ya bidhaa za ngozi yanayofanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers , Mhe. Chongolo amesema kuwa mkakati huo utasaidia kuinua uhakika wa soko kwa wazalishaji. Amefafanua kuwa maonesho hayo ya bidhaa za ngozi yanafanyika kwa mara ya kwanza katika Wilaya hiyo na kwamba ni lazima kila mwananchi ajenge utamaduni wa kupenda bidhaa zinazozalishwa hapa nchini na kuwataka kuondokana na dhana ya kuona bidhaa zinazotoka nje ndio bora zaidi. “ Ukienda kwenye nchi za wenzetu hasa zilizoendelea, wao wanathamini kwanza cha kwao, cha mwingine badae, nasisi tukifikia hatua hiyo tutafanikiwa sana, lakini tutafikaje hapo ni la zima kuanzia sasa tuamke tuanze kupenda vya kwetu” amesema Mhe. Chongolo. Mhe. Chongolo ameongeza kuwa uwepo wa maonesho hayo utaongeza tija na mipango madhubuti ya kuhakikisha kuwa mpango huo unakuwa endelevu sambamba na kuongeza wigo mpana wa kutangaza bidhaa hizo na wananchi kupenda kuzitumia. “ Uwepo wenu hapa utawezesha wale wananchi ambao wanakuja kununua bidhaa zenu , ndio watakuwa mawakala kwa wananchi wengine ambapo na wao watapenda kuja kununua bidhaa hizi bora na nzuri za kitanzania” ameongeza. Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kawe , Mhe. Muta Rwakatare amempongeza Mhe. Chongolo kwa kubuni na kufanikisha kuwepo kwa maonesho hayo. Ameongeza kuwa kutokana na umahiri aliokuwa nao mkuu huyo wa Wilaya wa kutatua changamoto mbalimbali za wananchi, anaamini kuwa sasa ni wakati wa wajasiriamali hao kunufaika kwani changamoto zao pia zimefikia kikomo. Ameongeza kuwa Rais Dk. John Magufuli amekuwa mstari wa mbele kusisitiza uchumi wa viwanda na kwamba hadi sasa tayari adhma hiyo imefanikiwa kwa asilimia kubwa. Naye Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Dk. Patricia Henjewele amesema kuwa wazo la kuwepo kwa maonesho hayo lilitolewa na Mhe. Chongolo wakati wa maonesho ya nanenane ambapo alihitaji kuandaliwa kwa mpango kazi wa kuwa na maonesho hayo. Amesema kuwa kabla ya kufanyika kwa maonesho hayo, awali yalifanyika mafunzo ya siku nne ambayo yaliendana sambamba na maonesho ya bidhaa hizo kwa siku moja yaliyofanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Maonesho hayo ya siku nne yatafikia kilele Disemba 15 ambapo bidhaa zote za ngozi ikiwemo viatu, mikoba, mikanda na mabegi ya shule ya wanafunzi yanapatikana hapo. Imetolewa na Kitengo cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni KINONDONI YAZINDUA MAONESHO YA BIDHAA ZA NGOZI VIWANJA VYA TANGANYIKA PACKERS, YAWEKA MKAKATI WA SOKO LA UHAKIKA Posted On: December 12th... + Read more »