KINONDONI YAUNGANA NA HALMASHURI NYINGINE KOTE NCHINI KUADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA
Manispaa ya Kinondoni leo imeungana na Halmashauri nyingine kote nchini, kuadhimisha siku ya mazingira duniani iliyoambatana na kauli mbiu isemayo" Tutumie nishati mbadala kuongoa mfumo Ikolojia"
Akiongea katika maadhimisho hayo yaliyofanyika Kimkoa katika viwanja vya mnazi mmoja, Mkuu wa Wilaya ya Ilala kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe.Ngw'ilabuzu ludigija amesema mazingira ni uhai, hivyo yatunzwe na fukwe pia ziendelee kutunzwa na kusisistiza wakandarasi wa mazingira kulipwa kwa wakati hali itakayowaongezea ufanisi katika kutekeleza Majukumu yao.
Mhe Ngw'ilabuzu amepongeza juhudi mbalimbali zinazofanywa na Halmashauri za mkoa wa Dar es salaam katika utunzaji wa mazingira na kuwataka kuongeza nguvu zaidi katika kuhakikisha mazingira yanalindwa pia.
Aidha zawadi mbalimbali zimetolewa kwa shule, wadau na Mitaa iliyofanya vizuri katika utunzaji wa Mazingira.
Katika maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa na Jiji la Dar es salaam pamoja na Halmashauri zake nne, pia yamehudhuriwa na wadau mbalimbali na kuonesha teknolojia zao zinazotumika katika kuhakikisha mazingira yanatunzwa vizuri "
Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
selectiondc
ReplyDelete