MWILI WA ALIYEKUWA DIWANI WA KATA YA MAGOMENI MH.JULIAN RUSHAIGO BUJUGO UMEAGWA LEO Posted On: October 23rd, 2018 Mwili wa aliyekuwa diwani wa Kata ya Magomeni kwa kipindi cha miaka kumi na nne(14), Mh.Juliani Rushaigo Bujugo umeagwa leo katika viwanja vya Manispaa ya Kinondoni. Akiongoza shughuli hiyo iliyohudhuriwa pia na viongozi wa vyama na Serkali, Mstahiki Meya wa Manispaa ya kinondoni Mh.Benjamini Sitta amesema, Kinondoni imepoteza mpiganaji, mpenda haki, mtetezi wa wanyonge, lakini pia mzalendo. "Bujugo alikuwa mzalendo, alikuwa ni mtu aliyependa kuona mambo yanakwenda, wanyonge wanapata haki, hata siku ambayo usiku wake mauti inamkuta, Mh Bujugo alikuja ofisini kwangu mchana kwa swala la walemavu wa magomeni kuhusiana na ada ya usajili wa kikundi wanayotozwa" Amezungumnza Meya Sitta. Shughuli hii ya kuuaga mwili wa marehemu Julian Rushaigo Bujugo imehudhuriwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Ndg Aron Kagurumjuli, wakuu wa idara na vitengo, wananchi wa kata ya Magomeni, pamoja na viongozi wa vyama na serikali, akiwemo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bi.Kate Kamba, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Ndg. Harold Maruma, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda, pamoja na Baraza la Madiwani la Manispaa ya Kinondoni. Bwana ametoa, bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi Amen. Imeandaliwa na, Kitengo cha Habari na Uhusiano. Manispaa ya Kinondoni. MWILI WA ALIYEKUWA DIWANI WA KATA YA MAGOMENI MH.JULIAN RUSHAIGO BUJUGO UMEAGWA LEO Posted On: October 23rd, 2018 Mwili wa aliyekuwa di... + Read more »
WAKULIMA NA WAFUGAJI KOTE NCHINI WAMETAKIWA KUZINGATIA UBORA WA BIDHAA WANAZOZALISHA ILI KUENDANA NA UHITAJI HALISI WA SOKO Posted On: October 16th, 2018 Ni agizo lake Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Omari Mgumba alipokuwa kwenye maadhimisho ya siku ya chakula duniani yenye kaulimbiu isemayo "Dunia bila njaa 2030 inawezekana", yaliyoadhimishwa kimkoa katika kituo cha kilimo Malolo, Kata ya Mabwepande, Manispaa ya Kinondoni. Amesema maadhimisho haya yanayoadhimishwa tarehe 16/10 ya kila mwaka ni maadhimisho yenye lengo la kuonesha umuhimu wa kukabiliana na baa la njaa, kwani kauli mbiu ya mwaka huu inasadifu hayo na inatakiwa kutekelezwa kwa wakulima wetu kufanya kilimo cha uzalishaji unaozingatia mahitaji, upatikanaji na ubora wa bidhaa ili kukabiliana na changamoto ya Masoko. "Tulime kwa kuzingatia mahitaji, ubora, na masoko, kwani ubora ndio utakaosababisha bidhaa zetu ziuzike kwa urahisi". Amesisitiza Naibu Waziri. Aidha Naibu Waziri huyo pia amewataka wasindikaji wa vyakula kuanzisha chama kikuu cha ushirika kitakachowaweka pamoja na kuwawezesha kupata mikopo kutoka kwenye mabenki na kubadilishana uzoefu utakaowasaidia kuongeza tija katika uzalishaji. Awali akitoa taarifa kwa Naibu Waziri, Mratibu wa wa maadhimisho hayo kwa Manispaa ya kinondoni ambaye pia ni Mkuu wa idara ya Kilimo Ndg Salehe Hija amesema kwa sasa kituo kinafanya utafiti wa ipi mbegu bora itakayoongeza tija katika Kilimo na kusaidia kupata mazao yanayohitajika hasa kwa wateja. Maadhimisho hayo yaliyoadhimishwa kimkoa katika Kata ya Mabwepande Manispaa ya Kinondoni na kushirikisha wajasiriamali, wakulima na wasindikaji kutoka Halmashauri ya Ubungo, Ilala, Kigamboni na Temeke, pia yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama na Serikali, kadhalika na wadau mbalimbali kama vile KOICA na NMB. Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na uhusiano Manispaa ya Kinondoni. WAKULIMA NA WAFUGAJI KOTE NCHINI WAMETAKIWA KUZINGATIA UBORA WA BIDHAA WANAZOZALISHA ILI KUENDANA NA UHITAJI HALISI WA SOKO Posted On: Oc... + Read more »
TUITHAMINI SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI KAMA JAMII, ILI TUWE SEHEMU YA KUIENZI KWA VITENDO Posted On: October 11th, 2018 Ni maneno yake katibu Tawala Wilaya ya Kinondoni Bi.Stella Msofe alipokuwa akizungumnza katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike, yenye kauli mbiu isemayo "Imarisha uwezo wa mtoto wa kike, tokomeza ukeketaji, mimba, na ndoa za utotoni" yaliyofanyika katika viwanja vya Tanganyika packers, vilivyoko Kata ya Kawe Manispaa ya Kinondoni. Amesema siku inayoadhimishwa tarehe 11/10 kila mwaka, inatakiwa kuenziwa kwa jamii kuwa sauti ya kukemea uovu na kupinga unyayasaji wa mtoto wa kike, hasa unapohisi mazingira aliyopo mtoto huyo, mifumo iliyopo katika jamii husika, si rafiki kwa maisha na afya yake "Kuwa mtoto wa kike kwanza ni neema na zawadi kutoka kwa Mungu, lakini pia ni ushindi tosha kwani akielimika mmoja, ni jamii nzima imeelimika, hivyo kusikufanye kushindwa kitimiza ndoto zako, mtoto wa kike unapaswa kujiamini, weka bidii katika vitu unavyoviamini kuwa vya maendeleo katika maisha yako na jamii inayokuzunguka na hakikisha unayasimamia" Amesisitiza Katibu Tawala Msofe. Ameongeza kuwa Jamii inayonafasi kubwa ya kuhakikisha haki, misingi na wajibu kwa mtoto wa kike vinazingatiwa na kupinga vikali ukiukwaji wa mifumo na tamaduni zinazowakandamiza watoto wa kike. Awali akitoa taarifa mbele ya katibu tawala huyo, Mratibu wa mradi wa ulinzi na usalama wa mtoto Manispaa ya Kinondoni Bi.Haika Harison, amezitaja changamoto zinazowakabili watoto wa kike kuwa ni ukeketaji, mimba za utotoni na ndoa za utotoni, na kuitaka jamii kuhakikisha inakuwa mstari wa mbele katika kumlinda mtoto wa kike. Maadhimisho hayo yaliyoadhimishwa kwa kushirikiana na mashirika binafsi ya Save the Children, na People's development forum yamekutanisha wanafunzi 180 kutoka shule 5 za Manispaa ya Kinondoni ambazo ni shule ya Sekondari Mikocheni, kawe, Mbezi ndumbwi pamoja na shule ya Msingi Changanyikeni na Makongo juu. Imeandaliwa na kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. TUITHAMINI SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI KAMA JAMII, ILI TUWE SEHEMU YA KUIENZI KWA VITENDO Posted On: October 11th, 2018 Ni maneno yak... + Read more »