TIMU YAUNDWA UTATUZI WA MGOGORO WA ARDHI NYAKASANGWE , MANISPAA YA KINONDONIPosted On: August 18th, 2020Wizara ya Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na Manispaa ya Kinondoni imefanikiwa kutatua changamoto ya mgogoro wa Ardhi uliodumu kwa kipindi cha miaka saba katika eneo la Nyakasangwe Kata ya Wazo kwa kuunda timu itakayofanya tathimini kwa awamu ya mwisho.Akizungumza na Wananchi wa eneo hilo, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Wilium Lukuvi amesema kuwa mgogoro huo unaohusisha eneo lenye takribani ekari 2878, umegawanyika katika makundi mawili ambayo ni upande wa wenyemashamba pamoja na wenye makazi wanaokadiriwa kufikia idadi ya watu 3300.“Nimepokea taarifa ya watalamu wangu lakini bado kunamapangufu kiasi, hivyo nimekuja na timu nyingine kutoka makao makuu ya Jeshi la Polisi Dodoma ambao watafanya kazi kwakushirikiana na Manispaa ya Kinondoni watafika huku muwape ushirikiano, kama mtu ulinunua eneo kwa mtu basi uwe na nyaraka zako” amesema Mhe. LukuviAmeongeza kuwa timu hiyo itaanza kufanya utambuzi kutokana na ripoti ya timu ya awali iliyoundwa na kwamba iwapo itabaini kunauvamizi ulifanyika kwa wanchi hao, serikali haitawavunjia nyumba badala yake watapaswa kulipia gharama ya eneo hilo sambamba na mwenyemashamaba halali na nyumba halali .Awali akimkaribisha Mhe. Waziri Lukuvi, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo alisema kuwa kwasasa Manispaa ya Kinondoni imefanikiwa kupima viwanja takriban 9000, hali iliyopelekea kupunguza migogoro hiyo kwa kiasi kikubwa.Mhe. Chongolo amesema Wananchi ambao tayari wameshapimiwa viwanja vyao wanapaswa kuchukua hati zao sambamba na wale ambao maeneo yao hajapimwa kuchukua hatua ili kuepukana na usumbufu wowote unaoweza kujitokeza.Imeandaliwa naKitengo Cha Habari na UhusianoManispaa ya Kinondoni. TIMU YAUNDWA UTATUZI WA MGOGORO WA ARDHI NYAKASANGWE , MANISPAA YA KINONDONI Posted On: August 18th, 2020 Wizara ya Ardhi ,Nyumba na Maend... + Read more »
DC CHONGOLO AMTAKA MKANDARASI ANAYEJENGA SOKO LA TANDALE KUONGEZA KASI YA UJENZI HUOPosted On: August 18th, 2020Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo amemtaka Mkandarasi wa Kampuni ya NAMIS CORPORATE L.T.D ambaye anajenga Soko hilo kuongeza kasi ya ujenzi huo ili Wafanyabiashara waweze kurudi kwenye eneo lao.Mhe. Chongolo amesema hayo alipofanya ziara katika soko la Tandale na kuwakuta wafanyabiashara katika mazingira yasiyo rafiki hali inayopelekea usumbufu wa shughuli zao na kumuelekeza mkandarasi huyo kuongeza kasi ya ujenzi huo ili kuondokana na adha inayowakabili.Amesema lengo la Serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inaboresha miundo mbinu yote ya masoko ili wafanyabiashara waweze kufanya biashara na kuendesha maisha yao na hivyo kuziwezesha Halmashauri kufikia malengo hayo.Amefafanua kuwa mradi huo wa Soko la kisasa unajengwa kwa gharama ya Sh. Bilioni 8.7 fedha ambazo zimetolewa na Serikali kuu na kwamba tayari mkandarasi huyo ameshalipwa fedha zote na hivyo kusisitiza kwamba anapaswa kufanya kazi usiku na mchana ilikukamilisha kazi yake kwa wakati. “Serikali ya Rais Dk. John Magufuli imemlipa mkandarasi pesa zote, hivyo hatudai badala yake sisi ndio tunamdai Soko letu atukabidhi kwa wakati sahihi, wafanyabishara na wananchi wanasubria kwa shauku kubwa sana ukizingatia Soko hili nimuhimu kwa wakazi wa Dar es Salaam, kwasababu litahusika zaidi na biashara ya mazao ya nafaka pamoja na bidhaa nyingine” amesema Chongolo. Awali Meneja kutoka kampuni hiyo iliyopewa kandarasi ya ujenzi wa Soko hilo Mhandisi James Msumari alimueleza Mhe. Chongolo kuwa ujenzi huo utachukua miezi 12 jambo ambalo alionesha kutokuridhishwa na muda huo na kusema kuwa hakuna sababu ya kutumia muda mrefu kwakuwa fedha wanazo hivyo wanapaswa kukamilisha ujenzi kwa makubaliano yaliyoingiwa.Kwaupande wake Mhandisi Msumari amesema wamepokea maagizo na wako tayari kuyatekeleza ili waweze kuondoa changamoto zinazowakabilio wafanyabiashara wa eneo hilo.Imeandaliwa naKitengo cha Habari na UhusianoManispaa ya Kinondoni. DC CHONGOLO AMTAKA MKANDARASI ANAYEJENGA SOKO LA TANDALE KUONGEZA KASI YA UJENZI HUO Posted On: August 18th, 2020 Mkuu wa Wilaya ya Kinond... + Read more »
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA BANDA LA KINONDONI, MAONESHO YA NANENANE KANDA YA MASHARIKI, MKOANI MOROGOROPosted On: August 6th, 2020Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, Bi. Mwanana Msumi, akipata maelezo kutoka kwa Maafisa wa Kitengo cha Uchaguzi Manispaa ya Kinondoni alipotembelea Banda hilo kwa lengo la kujionea maonesho hayo.Mtaalamu wa kutengeneza mfumo wa kisasa wa ufugaji wa Samaki Bwana. Jonas Ndau akitoa maelezo kwa Wananchi waliofika kuona mfumo huo unavyofanya kazi.Afisa Kilimo wa zao la mboga mboga kutoka Manispaa ya Kinondoni, Bwana. Emanuel Chacha akitoa maelezo ya Kilimo hicho kwa kutumia udongo kwa Wananchi waliofika katika Banda la Maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea mkoani Morogoro.Muonekano wa zao la Nyanya lililolimwa kwa kutumia mfumo wa eneo la wazi. Mtaalamu wa ufugaji wa Samaki kwa kutumia njia ya Bwawa la maji kutoka Manispaa ya Kinondoni, bwana Masumbuko Nzingula akitoa maelezo kwa Wananchi waliofika katika Banda la Manispaa hiyo katika Viwanja vya Maonyesho ya Nanenane mkoani Morogoro. Mjasiriamali wa Samaki na Dagaa kutoka Manispaa ya Kinondoni, Bi. Mwajuma Mwinyimbe akitoa maelezo kwa Wananchi waliofika katika banda la Manispaa hiyo viwanja vya maonesho ya Wakulima Nanenane yanayoendelea Mkoani Morgoro.Imeandaliwa naKitengo cha Habari na Mahusiano MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA BANDA LA KINONDONI, MAONESHO YA NANENANE KANDA YA MASHARIKI, MKOANI MOROGORO Posted On: August 6th, 2020 K... + Read more »
MATUKIO KATIKA PICHA BANDA LA KINONDONI MAONESHO YA NANENAE ,VIWANJA VYA TUNGI, MKOANI MOROGOROPosted On: August 4th, 2020Mfumo wa kuzungusha maji kwa ajili ya ufugaji wa Samaki kwa njia ya kisasa unaojulikana kwa jina la Recirculating Aquaculture System (RAS).Mzee ambaye ni mkazi wa Morogoro, akipata maelezo kutoka kwa Maafisa wa Kitengo cha uchaguzi Manispaa ya Kinondoni kuhusu masuala ya uchaguzi alipofika kwenye Banda la Manispaa hiyo katika maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea mkoani Morogoro.Wananchi waliofika katika Banda la Manispaa ya Kinondoni katika kikundi cha Vijana wajasiriamali ambao ni wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Manispaa hiyo wakiangalia bidhaa za viatu vya ngozi katika maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea mkoani Morogoro.Afisa mifugo wa Kampuni ya Ronheana kutoka Manispaa ya Kinondoni akitoa maelezo kwa Maafisa kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi walipopita kutembelea Banda la Manispaa hiyo katika maonesho ya wakulima nanenane yanayoendelea mkoaani Morogoro.Mkurugenzi mwendeshaji wa Kampuni ya Wasambazaji wa Teknolojia ya Jividudu hai (E.M) kutoka Manispaa ya Kinondoni Bi. Gigwa Swai akitoa maelezo kwa mtaaalmu kutoka Manispaa ya Temeke katika Banda la Manispaa ya hiyo katika maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea mkoani Morogoro.Kikundi Cha wajasiriamali wakinamama kutoka Manispaa ya Temeke waliovaa Tishet za kijivu wakibadilishana ujuzi kutoka Kikundi cha wakina Mama wajasiriamali wa Manispaa ya Kinondoni katika maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea mkoani Morogoro.. Maafisa mifugo Bi. Grace Misonge na Bi Ancila Malamshakutoka Halmashauri ya Chalinze wakipata maelezo kuhusiana na masuala ya Kilimo kwa ujumla.Imeandaliwa naKitengo cha Habari na UhusianoManispaa ya Kinondoni. MATUKIO KATIKA PICHA BANDA LA KINONDONI MAONESHO YA NANENAE ,VIWANJA VYA TUNGI, MKOANI MOROGORO Posted On: August 4th, 2020 Mfumo wa kuzun... + Read more »
PROFESA KABUDI AIPONGEZA KINONDONI MAONESHO YA WAKULIMA NANENANEPosted On: August 1st, 2020Waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Profesa Paramagamba Kabudi ametembelea Banda la Kinondoni katika maonesho ya wakulima ya nanenane Mkoani Morogoro nakuipongeza kwakuwa na vitu ambavyo vinavutia watazamaji.Profesa Kabudi amesema katika Banda hilo amevutiwa na Teknolojia ya kilimo Cha mjini na Vijijini ikiwemo kilimo Cha kisasa cha mbogamboga na mazao ya chakula sambamba na ufugaji wa kisasaAmeongeza kuwa kupitia maonesho hayo wananchi wa Dar es Salaam wanakila sababu ya kujifunza teknolojia hizo kutoka Manispaa ya Kinondoni kwakuwa itawawezesha kuendesha shuguli zao za kilimo Cha mijini.Amesema katika Banda hilo pia amevutiwa na wajasiriamli wakina Mama wanaotengeneza bidhaa za nguo kwa kutumia Teknolojia ya kisasa ambao inaongeza thamani ya bidhaa hiyo na hivyo kumpongeza Mkurugenzi Aron Kagurumjuli kwa kuwawezesha wajasiriamali hao." Mkurugenzi nakupongeza wewe pamoja na timu nzima ya Kinondoni, mmefanya kazi kubwa kwenye maonesho hayo, mmewaletea Wananchi mambo mazuri ambapo wanapokuja kuangalia wanaondoka na ujuzi mzuri katika nyanja zote ikiwemo kilimo, ufugaji, usindikikaji wa vyakula na utengenezaji wa bidhaa za nguo za batiki.Aidha ameipongeza Manispaa hiyo kwa kuwawezesha vijana wajasiriamali katika utengenezaji wa bidhaa za ngozi ikiwemo viatu nakusema kuwa mpango huo ni mzuri kwani unaendana sambamba na kauli mbiu ya Serikali ya Viwanda ya Rais Dk. John Pombe Magufuli.Ameongeza kuwa Rais Magufuli anaguswa na vijana ambao wanatumia ujuzi wao kwa ajili ya kuijenga nchi na kwamba Manispaa imeonambali katika kuwawezesha kwenye ufanisi huo ambao unatija kwa Taifa.Imeandaliwa naKitengo Cha Habari na UhusianoManispaa ya Kinondoni. PROFESA KABUDI AIPONGEZA KINONDONI MAONESHO YA WAKULIMA NANENANE Posted On: August 1st, 2020 Waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa Kima... + Read more »
KINONDONI YAZINDUA MFUMO WA KUTUMIA SIMU MPANGUSO KUPATA USHAURI WA LISHE (BETTER YOUR HEALTH) KWA WATUMIAJI WA DAWA ZA KUFUBAZA MAKALI YA VIRUSI VYA UKIMWIPosted On: July 29th, 2020Akizindua mfumo huo wa kutumia simu mapanguso( smartphone) better your health kupata ushauri wa lishe na taarifa za hali ya afya na kwa watumiaji wa dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI (vvu) kwa kushirikiana na wadau kutoka Fabstech, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dr. Samweli lizer kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo amesema ni mfumo mzuri utakaosaidia kutoa taarifa za msingi katika kuhakikisha mtumiaji anazipata ili kuboresha afya yake.Amesema ni fursa pekee itakayosaidia kundi hili maalumu kula mlo kamili kwa kufuata utaratibu hali itakayosaidia kupungua kwa maambukizi katika jamii.Akiutambulisha mfumo huo Dr.Linda Mlunde kutoka kampuni ya teknolojia inayojishughulisha na utengenezaji wa mifumo ( Fabstech ltd).amesema ni mfumo rafiki wa kutumia simu kwa watumiaji wa dawa za kufubaza makali ya VVU ili kupata ushauri wa lishe na taarifa za afya zitakazowasaidia kuimarisha afya zao.Ameongeza kuwa mtumiaji wa mfumo huu atatakiwa kuwa na simu mpanguso ( smartphone) ili aweze kujisajili na ili mtumishi aweze kutumia mfumo atafuata maelezo na kuingiza taarifa zake kwenye mfumo ambazo ni uzito, urefu, muda na kiasi cha chakula alichokula kwa siku baada ya kuingiza taarifa hizo kwenye mfumo mtumiaji atapata mrejesho kuhusu afya yake ya mwili na ushauri wa lishe kutokana na Hali yake ya afya aliyonayo.Akieleza jinsi ya kujiunga na mfumo huo wa Better yourHealth Ndg Karimu Iddi kutoka kampuni ya Fabstech ameeleza namna ya kupata mfumo huo katika simu yako kwa kufuata hatua ambazo ni kufungua Playstore-na kupakua app ya chrome, pili Update App ya Chrome, tatu kufungua App ya Chrome na kuandika maneno, betteryouth.co.tz, nne kubonyeza kitufe Cha Go, tano kufuata maelekezo ili kuruhusu mfumo wa better your helath katika simu yako, kujisajili na kuanza kutumia mfumo wa better YH.Naye Bi.Gisela Mallya ambaye ni mtumiaji wa mfumo wa better your health amesema ni mfumo rafiki na mzuri kwani unasaidia kupata ushauri wa lishe na taarifa stahiki zinazomuwezesha kujua uwiano Kati ya urefu na uzito wake na suala zima la lishe hali uliyonayo ikiwa ni pamoja na aina yachakula unachotakiwa kula, kiasi cha chakula na wakati gani unaoenda sambamba na nini kifanyike pindi unapohitajika kufanya hivyo.Uzinduzi wa mfumo huo uliodhaminiwa na PEPFAR, MCC, na WFP, na kusimamiwa na Tanzania data lab, mehudhuriwa na wajumbe kutoka Tanzania Data lab (dLab), CHMT, watoa huduma wa afya kutoka vituo vya afya, watoa huduma kutoka ngazi ya jamii, Wateja ambao ndio watumiaji wa mfumo na timu iliyotengeneza mfumo wa better your health kutoka kampuni ya Fabstech limited.Imeandaliwa naKitengo Cha Habari na UhusianoManispaa ya Kinondoni KINONDONI YAZINDUA MFUMO WA KUTUMIA SIMU MPANGUSO KUPATA USHAURI WA LISHE (BETTER YOUR HEALTH) KWA WATUMIAJI WA DAWA ZA KUFUBAZA MAKALI YA... + Read more »