Top ad

Top ad

 

KINONDONI YAZINDUA MFUMO WA KUTUMIA SIMU MPANGUSO KUPATA USHAURI WA LISHE (BETTER YOUR HEALTH) KWA WATUMIAJI WA DAWA ZA KUFUBAZA MAKALI YA VIRUSI VYA UKIMWI

Posted On: July 29th, 2020

Akizindua mfumo huo wa kutumia simu mapanguso( smartphone) better your health kupata ushauri wa lishe na  taarifa za hali ya afya na kwa watumiaji wa dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI (vvu) kwa kushirikiana na wadau kutoka  Fabstech, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dr. Samweli lizer kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo amesema ni mfumo mzuri utakaosaidia kutoa taarifa za msingi katika kuhakikisha mtumiaji anazipata ili kuboresha afya yake.

Amesema ni fursa pekee itakayosaidia kundi hili maalumu kula mlo kamili kwa kufuata utaratibu hali itakayosaidia kupungua kwa maambukizi katika jamii.

Akiutambulisha mfumo huo Dr.Linda Mlunde kutoka kampuni ya teknolojia inayojishughulisha na utengenezaji wa mifumo ( Fabstech ltd).amesema ni mfumo rafiki wa kutumia simu kwa  watumiaji wa dawa za kufubaza makali ya VVU  ili kupata ushauri wa lishe na taarifa za afya  zitakazowasaidia kuimarisha afya zao.

Ameongeza kuwa mtumiaji wa mfumo huu atatakiwa kuwa na simu mpanguso ( smartphone) ili aweze kujisajili na ili mtumishi aweze kutumia mfumo atafuata maelezo na kuingiza taarifa zake  kwenye mfumo ambazo ni uzito, urefu, muda na kiasi cha chakula alichokula kwa siku baada ya kuingiza taarifa hizo kwenye mfumo mtumiaji atapata mrejesho kuhusu afya yake ya mwili na ushauri wa lishe kutokana na Hali yake ya afya aliyonayo.

Akieleza jinsi ya kujiunga na mfumo huo wa Better yourHealth Ndg Karimu Iddi kutoka kampuni ya Fabstech ameeleza namna ya kupata mfumo huo katika simu yako kwa kufuata hatua ambazo ni kufungua Playstore-na kupakua app ya chrome, pili Update App ya Chrome, tatu kufungua App ya Chrome na kuandika maneno, betteryouth.co.tz, nne kubonyeza kitufe Cha Go, tano kufuata maelekezo ili kuruhusu mfumo wa better your helath katika simu yako, kujisajili na kuanza kutumia mfumo wa better YH.

Naye Bi.Gisela Mallya ambaye ni mtumiaji wa mfumo wa better your health amesema ni mfumo rafiki na mzuri kwani unasaidia kupata ushauri wa lishe na taarifa stahiki zinazomuwezesha kujua uwiano Kati ya urefu na uzito wake na suala zima la lishe  hali uliyonayo ikiwa ni pamoja na aina yachakula unachotakiwa kula, kiasi cha chakula na wakati gani unaoenda sambamba na nini kifanyike pindi unapohitajika kufanya hivyo.

Uzinduzi wa mfumo huo uliodhaminiwa na PEPFAR, MCC, na WFP, na kusimamiwa na Tanzania data lab, mehudhuriwa na wajumbe kutoka Tanzania Data lab (dLab), CHMT,  watoa huduma wa afya kutoka vituo vya afya, watoa huduma kutoka ngazi ya jamii, Wateja ambao ndio watumiaji wa mfumo na timu iliyotengeneza mfumo wa better your health kutoka kampuni ya Fabstech limited.

Imeandaliwa na

Kitengo Cha Habari na Uhusiano

Manispaa ya Kinondoni

0 comments:

Post a Comment

 
Top