MATUKIO KATIKA PICHA- HAFLA YA PONGEZI KWA WAALIMU KINONDONI Posted On: January 17th, 2020 Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Dk. Patricia Henjewele akionesha tuzo iliyotolewa na Idara ya Elimu kwa ajili ya kumpongeza Mkurugenzi Aron Kagurumjuli kwa kusimamia kikamilifu masuala ya elimu na hivyo kuendelea kupata matokeo mazuri kwenye Halmashauri hiyo. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo akitoa za wadi kwa mmoja wa washindi waliofanya vizuri kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka 2019,wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kinondoni. Mhe. Harlod Muruma. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo, akionesha zawadi aliyotunukiwa na Idara ya Elimu kuonyesha mchango wake katika sekta hiyo, kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Mhe. Harlod Muruma na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Dk. Patricia Henjewele. MATUKIO KATIKA PICHA- HAFLA YA PONGEZI KWA WAALIMU KINONDONI Posted On: January 17th, 2020 Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispa... + Read more »
DC CHONGOLO AWAONYA WAKUU WA SHULE ZA SEKONDARI KINONDONI Posted On: January 17th, 2020 NI KUHUSIANA NA TARATIBU ZA KUWAPOKEA WANAFUNZI KIDATO CHA KWANZA. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo amewaagiza wakuu wa shule zote za Sekondari katika Wilaya hiyo kuacha mara moja tabia ya kuwazuia wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza kuanza masomo kutokana na kutokamilisha mahitaji yao ya shule. Ametoa agizo hilo jana wakati wa sherehe za kuwapongeza walimu kwa ufaulu mzuri wa mitihani ya kumaliza elimu ya msingi kwa mwaka 2019 ambapo Kinondoni imepata ufaulu wa asilimia 97.17 na kuwa ya tatu kati ya Halmashauri 186 kitaifa, hafla iliyofanyika ukumbi wa officers Mess Amesema kuwa zipo baadhi ya shule ambazo zinawazuia wanafunzi kujiunga na masomo kwa kile wanachokidai kutokamilisha mahitaji ya shule na kuzitaka shule za Kinondoni kutojihusisha na tabia hiyo bali kuwa sehemu ya kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano inayotekeleza sera madhubuti ya elimu bila malipo inayoenda sambamba na uchumi wa viwanda. “Kuna baadhi ya maeneo nimesikia kuna wakuu wa shule wanawarudisha nyumbani watoto kwa sababu hawajakamilisha mahitaji yao, kama mtoto hana viatu, sijui nini waache wasome wakati wazazi wao wanawatafutia mahitaji hayo, naomba nisi sikie mwanafunzi amerudishwa nyumbani kwenye wilaya yangu” amesisitiza Mhe. Chongolo. Naye Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe. Benjamini sitta amesema kuwa mafanikio ya kufanya vizuri kwa wanafunzi wa darasa la saba mwaka 2019 kwenye Halmashauri hiyo ni uthibitisho tosha unao onesha namna walimu, wazazi na wanafunzi wanavyoshirikiana kikamilifu katika nyanja ya elimu na hivyo kutoa wito kwa wazazi kuendeleza ushirikiano huo katika usimamizi wa wanafunzi hususani kwenye masuala ya taaluma. Kaimu Afisa elimu wa Halmashauri hiyo, Bi Chitegets Dominick pia alifafanua jumla ya wanafunzi waliosajiliwa kufanya mtihani huo walikuwa 12,619, wavulana 6,115 na wasichana 6,450, huku walioganya wakiwa 12,523, wavulana 6,058 na wasichana 6,465. Katika hatua nyingine Mhe. Chongolo amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Ndugu Aron Kagurumjuli kwa usimamizi mzuri wa elimu na kwamba anatambua jitihada zake za kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanapata elimu bila malipo na kwamba anatimiza kimamilifu majukumu na maagizo yanayotolewa na Rais Dk. John Magufuli Imeandaliwa na Kitengo cha na Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. DC CHONGOLO AWAONYA WAKUU WA SHULE ZA SEKONDARI KINONDONI Posted On: January 17th, 2020 NI KUHUSIANA NA TARATIBU ZA KUWAPOKEA WANAFUNZI... + Read more »