MATUKIO KATIKA PICHA- HAFLA YA PONGEZI KWA WAALIMU KINONDONI
Posted On: January 17th, 2020
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Dk. Patricia Henjewele akionesha tuzo iliyotolewa na Idara ya Elimu kwa ajili ya kumpongeza Mkurugenzi Aron Kagurumjuli kwa kusimamia kikamilifu masuala ya elimu na hivyo kuendelea kupata matokeo mazuri kwenye Halmashauri hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo akitoa za wadi kwa mmoja wa washindi waliofanya vizuri kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka 2019,wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kinondoni. Mhe. Harlod Muruma.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo, akionesha zawadi aliyotunukiwa na Idara ya Elimu kuonyesha mchango wake katika sekta hiyo, kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Mhe. Harlod Muruma na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Dk. Patricia Henjewele.
0 comments:
Post a Comment