Top ad

Top ad

BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LA PITISHA BAJETI YA BILIONI 170.9

Posted On: January 23rd, 2020
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, katika Mkutano wake maalumu wa Baraza  leo  Alhamisi,  tarehe  23 Januari 2020,   limejadili na  kuidhinisha kwa kauli moja  bajeti yake ya  Tshs  170, 918,524,100/= kwa mwaka wa fedha 2020/2021  ambapo  Tshs.42,951,312, 000/= ni za Mapato ya ndani ya Manispaa na Tshs. 127,967,212,100/= ni Mapato ya Ruzuku kutoka Serikali kuu  zikijumuisha Tshs. 57,018,968,680/= kwa ajili ya  mishahara,Tshs.1,689,501,000/= za matumizi mengineyo na Tshs. 69,258,742,520, /= za  miradi ya maendeleo.
 Kiasi cha ,Tshs. 42,951,312,000/= kilichotengwa na  Manispaa ya Kinondoni kutokana na  makusanyo ya  vyanzo vya ndani vya, Manispaa  kinajumuisha  Tshs.883,467,270/=, kwa ajili ya mishahara ,Tshs. 21,353,714,130,000/= kwa ajili ya matumizi mengineyo na Tshs. 20,714,130,000/= kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
  Azungumza wakati wa kupitisha Bajeti hiyo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh Benjamin Sitta amebainisha kuwa ili kuboresha maisha ya wakazi wa Kinondoni, Manispaa imeandaa mpango wa mwaka 2020/2021 na mpango wa muda wa kati 2020/2021 – 2022/2023 unaolenga kukuza uchumi na kupunguza umaskini na kufikia maendeleo endelevu ya kijamii, kiuchumi,na kimazingira kwa wananchi wake.
Meya Sitta ametanabaisha kuwa Ili kutekeleza dhana nzima ya ugatuaji wa madaraka , mpango huo umeshirikisha jamii katika mpango shirikishi kuanzia ngazi ya Mtaa kwa kuzingatia vipaumbele na  mahitaji halisi ya Wananchi katika maeneo yao na kujielekeza katika kutoa kipaumbele maeneo yanayoweza kutoa matokeo ya haraka yatakayosaidia ukuaji wa uchumi kwa haraka na kwa kipindi kifupi.
Ameyataja maeneo ya kipaumbele kuwa ni pamoja na kuboresha na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kuwekeza katika miradi mikubwa ya Kimkakati, kuboresha miundombinu ya Afya, na Elimu,kuboresha hifadhi ya mazingira na ukusanyaji wa taka, kuimarisha ushirikishaji wa jamii katika upangaji na  utekelezaji wa miradi ya maendeleo, na uboreshaji wa mazingira ya wafanyabiashara wadogowadogo kwa kuwajengea masoko katika maeneo mbalimbali.
Ili kufikia malengo yaliyokusudiwa,  Mstahiki Meya amewataka viongozi na watendaji wote kusimamia uimarishaji wa mahusiano mazuri kati ya Serikali ,Mashirika yasiyo ya kiserikali na wadau wengine, kujenga uwezo na ujuzi kwa watumishi katika utoaji wa huduma, kuimarisha utawala bora, uwajibikaji na uwazi sambamba na kujenga uwezo kwa viongozi wakiwemo waheshimiwa madiwani na wenyeviti wa Serikali za mitaa katika kusimamia shughuli za Wananchi.
 Aidha Mstahiki Meya   amewashukuru wadau  wote waliofanikisha bajeti hiyo  zikiwemo kamati  zote za kudumu za Manispaa,  Serikali kuu iliyotenga kiasi kikubwa cha fedha kugharamia  Miradi mikubwa ya kimkakati  ya ujenzi wa soko la Tandale, Soko la Magomeni  uboreshaji wa  Fukwe za Cocobeach na miradi mingine ya sekta mbalimbali inayotekelezwa ndani ya Manispaa ya Kinondoni kwa Fedha kutoka Serikali kuu.

Miradi  iliyotengewa fedha kwa Mapato ya  ndani ya Manispaa katika mwaka wa fedha  2020/2021  ni pamoja na ukamilishaji wa kituo cha  kisasa cha daladala Mwenge kwa  milioni 500, ukamilishaji ujenzi wa uwanja wa mpira Mwenge kwa  milioni 500, ujenzi wa standi ya kisasa ya daladala na soko Tegeta nyuki kwa bilioni 3.5, ujenzi wa kituo cha kisasa cha daladala Bunju B  kwa milioni 600,ujenzi wa maabara, famasia, rediolojia, na ununuzi wa gari la kubeba wagonjwa katika Hospitali ya Wilaya Mabwepande kwa bilioni 1 na ujenzi wa incinerator kubwa kwa ajili ya kuchoma taka za vituo vyote vya kutolea huduma za afya kwa billion 1.5.

Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

0 comments:

Post a Comment

 
Top