Top ad

Top ad

 

NI KINONDONI TENA UFAULU WA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2020 MKOA WA DAR ES SALAAM

Posted On: December 24th, 2020

Manispaa ya Kinondoni imeshika nafasi ya kwanza kimkoa na ya pili Kitaifa kwa ufaulu wa asilimia 98.1 matokeo ya darasa la Saba kwa mwaka 2020.

Hayo yamebainishwa na Mstahiki Meya Manispaa ya Kinondoni Mhe Songoro Mnyonge alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari kwa lengo la kuelezea mikakati ya Halmashauri katika kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu wanaingia kidato cha kwanza kwa mwaka 2021.

Mhe.Songoro mesema "Kinondoni imeendelea kuongoza katika matokeo yaliyotangazwa, ambapo 13,401 walifanya mtihani wa darasa la Saba mwaka huu na 13,159 wamefaulu na kupelekea ufaulu huo kufikia asilimia 98.1 na kwa ufaulu huo, umeufanya Manispaa ya Kinondoni kuwa ni nafasi ya kwanza Kimkoa na kuwa ya pili Kitaifa, haya ni mafanikio makubwa" Amesema Mstahiki Meya.

Ameongeza kuwa kwa wanafunzi 775 wanaosubiri chaguo la pili, Manispaa ya Kinondoni tayari Imekwishajipanga kuhakikisha inakabiliana  na changamoto hizo za uhaba  wa madarasa zinazopelekea wanafunzi hao kusubiri kwa kujenga vyumba 64 vitakavyoweza kupunguza adha hiyo kwa kiasi kikubwa mara vitakapokamilika.

Ameainisha mchanganuo wa ujenzi pamoja na ukarabati  wa vyumba hivyo vya madarasa kuwa ni ujenzi wa vyumba vya madarasa 10 sekondari ya kijitonyama, ukaratabati wa vyumba 7 shule ya Sekondari Magomeni, ujenzi wa madarasa 6 shule ya sekondari ya Benaco na ujenzi was  madarasa 6  sekondari ya mzimuni.

Mchanganuo mwingine ni ujenzi madarasa 6 shule ya Sekondari Mbezi juu, ujenzi wa madarasa 8 shule  ya Bunju tarimo, ujenzi wa madarasa 8 Boko mtambani, ujenzi wa madarasa 5 shule ya sekondari kondo, ujenzi wa madarasa 6 shule ya sekondari Oysterbay pamoja na  ujenzi wa shule mpya ya miti mirefu.

Aidha amefafanua kuwa ujenzi wa vyumba vya madarasa unaenda sambamba na ujenzi wa hostel itakayoweza kuchukua wanafunzi 320, pamoja na madawati 6000 ambapo kiasi cha tsh milioni180 na laki 5 zimetengwa kwa ajili ya utengenezaji wa madawati hayo ambapo madawati 3210 yamekamilika.

Mhe songoro ameeleza kuwa matarajio ya Manispaa ni kuhakikisha ifikapo mwezi wa pili 2021,  ujenzi pamoja na ukarabati wa vyumba vya madarasa 64, yawe yameshakamilika tayari kupokea wanafunzi.

Jumla ya wanafunzi 13401 walifanya mtihani wa darasa la Saba mwaka huu ambapo wanafunzi 13,159 wamefaulu na 12,384 wameshapata nafasi za kujiunga na kidato cha kwanza na kupelekea  wanafunzi 775 kusubiri chaguo la pili.


Imeandaliwana

Kitengo cha Habari na Uhusiano

Manispaa ya Kinondoni

0 comments:

Post a Comment

 
Top