TAMISEMI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA DMDP NA TARURA KINONDONI.
Posted On: June 21st, 2019
Hayo yamethibitika leo wakati Waziri wa TAMISEMI Mhe. Suleiman Jafo alipofanya ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo kwa lengo la kujiridhisha na ubora wake ikiwa ni pamoja na kuangalia hatua za utekelezaji zilizofikwa.
Amesema utekelezaji wa miradi hii kwa mkoa wa Dar es salaam ni ya muhimu sana kwani itatatua kero kubwa walizokuwa wakizipata wananchi hasa yale maeneo waliyokuwa wakisumbuliwa na mafuriko na zile zilizokuwa na uharibifu mkubwa.
"Miradi hii ni muhimu sana kwani inaenda kubadilisha sura ya Dar es salaam, tunachotaka kama Serikali ni kuhakikisha kero kwa wananchi zinaondolewa na hata wale walioko masomoni wakirudi, tuwashike mikono, taswira ibadilike "Amesisitiza Jafo.
Naye Mratibu wa DMDP Manispaa ya Kinondoni Ndg. Mkelewe Tungaraza alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya DMDP amesema dhamira yao kubwa ni kuhakikisha wanaisimamia na kuitekeleza kwa kiwango kinachotakiwa ili ilete tija kwa wananchi husika.
Katika hatua nyingine, Waziri Jafo amewataka wananchi kuhakikisha wanazitunza na kuzifanyia usafi barabara hizo, ikiwa ni pamoja na kuepuka kutupa taka kwenye mitaro kwani kwa kufanya hivyo kutaathiri ubora na Mazingira kwa ujumla.
Kadhalika amewataka wakandarasi kuhakikisha wanakamilisha suala la uwekaji wa alama za barabara hizo,, ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa weledi, kwa kuzingatia vigezo na viwango vya ubora ili miundombinu hiyo iweze kudumu kwa muda mrefu huku ikiendelea kusaidia wananchi.
Katika ziara hiyo aliyotembelea barabara ya Mbezi Makonde, Kilongawima, akachube na makanya pia imehudhuriwa na wakuu wa wilaya ya Ubungo na Kinondoni, wakurugenzi, wakandarasi pamoja na waratibu wa TARURA na DMDP.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Uhusiano na Habari.
Manispaa ya Kinondoni.
0 comments:
Post a Comment