KAMATI YA SIASA YA MKOA WA DAR ES SALAAM, YARIDHISHWA NA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA KATIKA WILAYA YA KINONDONI.
Posted On: May 24th, 2019
Kamati hiyo Chini ya mwenyekiti wake Bi Kate Kamba imeonesha kuridhishwa na maboresho ya miundombinu ya barabara yanayofanyika maeneo ya katikati hususan Tandale, Kijitonyama na Mwananyamala Manispaa ya Kinondoni.
Hali hiyo imedhihirika wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo ukiendelea katika ziara ya Kamati ya katika Manispaa ya Kinondoni, chini ya Mwenyekiti wake Bi. Kate Kamba, iliyofanyika kwa lengo la kujiridhisha na utekelezaji wa ilani unaoenda sambamba na ubora wa miradi inayotekelezwa.
Bi Kate amesema kuwa wakati umefika sasa kwa Kinondoni kuelekeza nguvu katika kuboresha makazi holela wanayoishi wananchi kwani wanaamini maboresho ya miundombinu yakienda sambamba na maboresho ya makazi ndipo tija
itakapopatokana.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bw Maduhu Kazi ameishukuru Kamati hiyo kwa kutembelea Kinondoni na kuahidi kufanyia kazi ushauri na maelekezo yote yaliyotolewa na Kamati hiyo ya Siasa.
Miradi iliyotembelewa katika ziara hiyo ni pamoja na miradi ya barabara, Shule za Msingi na Sekondari, zahanati pamoja na vituo vya Afya.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
0 comments:
Post a Comment