MKUU WA WILAYA YA KINONDONI ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA NYUMBA ZA MAGOMENI KOTA
Posted On: October 2nd, 2019
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe Daniel Chongolo ameridhishwa na Kasi ya ujenzi unaoendelea wa nyumba za magomeni kota ambao kwa sasa unaenda kwa Kasi.
Mhe Chongolo amebainisha hayo leo alipotembelea ujenzi huo kwa lengo la kujionea maendeleo ya ujenzi na kuangalia Kama kuna changamoto zozote zinazoukabili mradi huo.
Amesema anawapongeza Sana TBA kwa kutoa ajira kwa vijana zaidi ya 700 wanaoishi maeneo ya karibu ambao wamepata nafasi za ufundi na vibarua, wasambazaji wa vifaa vya ujenzi zaidi ya 30 na watoa huduma wa chakula zaidi ya 38 ambao wanapata mahitaji yao ya kila siku kupitia mradi huo.
Aidha Amepongeza juhudi zao za kupunguza matumizi yasiyo ya lazima kwa kuanzisha kiwanda kidogo Cha kutengeneza matofali, matofali ambayo yanatumika katika kukamilisha ujenzi huo.
Kwa upande wake msimamizi mkuu wa mradi huo Bw Bernard Manyema amesema mradi huo ambao unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba mwaka huu umekamilika katika hatua ya uwekaji wa miundombinu ya awali ya umeme na maji na sasa wanaendelea na zoezi la kupiga lipu nyumba zote.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
0 comments:
Post a Comment