Ushauri huo umetolewa leo na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mh.Benjamini Sitta katika kikao cha majumuisho ya ziara hiyo baada ya kutembelea miradi ya elimu kilichofanyika katika ukumbi w mikutano wa Manispaa.
Amesema kamati ya huduma za uchumi, afya na elimu ndio injini ya Halmashuri kwani inagusa sekta muhimu za uchumi na afya ambazo moja kati yake isipoenda sawia basi hakuwezi kuwa na mafanikio.
Amesema" Hii kamati ya Huduma za Uchumi ni ya muhimu sana, lakini mmejikita sana kwenye miradi ya elimu, mnasahau sekta muhimu ya uchumi na afya, mimi nadhani wakati umefika sasa muje na mikakati mipya ya kukuza uchumi kwa kuibua vyanzo vipya vya mapato" Mh Sitta.
Akipokea ushauri huo kutoka kwa mstahiki Meya, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Thadeus Massawe ameahidi kuufanyia kazi, yeye pamoja na timu yake nzima, na kumshukuru Mstahiki Meya kwa ushauri huo wenye tija kwa Halmashauri yetu.
Kamati hiyo katika ziara yake, imetembelea na kukagua miradi mitatu ya shule ambayo ni ; shule ya Msingi na awali Liberman iliyopo Kawe, Shule ya awali Del Paul iliyopo Wazo na Shule ya awali Mbweni Heights iliyopo Mbweni.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
0 comments:
Post a Comment