Top ad

Top ad

BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA KINONDONI LAMPONGEZA MKURUGENZI KWA UTENDAJI.

Posted On: November 21st, 2018
 Baraza la Madiwani Manispaa ya Kinondoni, chini ya Mwenyekiti wake Mh.Benjamini Sitta,  kupitia mkutano wake wa Mwaka uliofanyika leo limempongeza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Ndg Aron Kagurumjuli, pamoja na timu yake nzima kwa utendaji mzuri na ushirikiano mkubwa katika kukusanya mapato,  uliopelekea ongezeko la  ukusanyaji wake kufikia asilimia 98%. kwa tathmini ya bajeti ya mwaka 2017/2018.
 Pongezi hizo zimekuja mara baada ya Mkurugenzi huyo kuwasilisha  taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo, taarifa za utendaji kazi,  taarifa za mali za Halmashauri pamoja na tathmini ya bajeti ya mwaka 2017/2018,  iliyoonesha kiasi cha bajeti iliyotengwa, makusanyo kutoka vyanzo vya ndani, mapato pamoja na matumizi, huku ikionesha changamoto na mikakati ya kukabiliana nayo katika suala zima la ukusanyaji wa mapato.

 Amezitaja  changamoto hizo kuwa ni  baadhi ya vyanzo vikubwa vya mapato kuondolewa katika Halmashauri na kupelekwa Serikali kuu, sheria ndogo zinazotumika kutoza ushuru kwenye masoko kupitwa na wakati, kuwepo mikataba isiyozingatia maslahi ya Halmashauri, na kuwepo migogoro ya vibanda katika  masoko na maeneo ya wazi.
 Aidha Mkurugenzi huyo pia ameainisha mikakati ya kukabiliana na changamoto hizo kuwa ni kuziba pengo la vyanzo vya mapato lililofutwa kwa kuanzisha daftari la walipakodi, kuwepo mchakato wa sheria ndogo zilizopitwa na wakati kufanyika upya, kutambua maeneo ya wazi na vibanda vya biashara vilivyopo katika maeneo ya Umma na kisimamia utozaji wake,  kuimarisha mfumo wa upatikanaji wa takwimu za walipakodi na   kufanya mapitio ya mikataba ya sasa ya uwekezaji.


 Katika hatua nyingine katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni Bi Stella Msofe, katika kikao hicho, amemtangaza rasmi Diwani wa Kata ya Kigogo  Mh Mangalu George Manyama kuwa Naibu Meya wa Manispaa hiyo, kwa awamu nyingine tena.
 Imeandaliwa na 
 Kitengo cha Uhusiano na habari. 
 Manispaa ya Kinondoni.

0 comments:

Post a Comment

 
Top